Kuna muda mapenzi yanahitaji uwe na roho ngumu ili yaende sawa

Kuna muda mapenzi yanahitaji uwe na roho ngumu ili yaende sawa

Nimekuelewa mkuu hii kanuni naitumia sana yaan mie sasa sipo kwenye naz wala firigisi mie ni jiwe jiwe tuuu nje ngum ndan ngum ukileta za kuleta tupaa kuleee[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] sinaga jam na mapenz landa hapo badae naeza kuwa kanazi kwa mbaaaali ila sio maini kabisaaaa[emoji23]
 
Roho ngumu ndio, ukiwa mlaini sana utateseka yatakupeleka puta yakufanye zombi. Moyo upondeke, ujione haufai uyachukie mapenzi wakati ni makitu matamu tu. Chagua kua nazi (nje ngumu ndani laini) au firigisi (nje laini ndani ngumu) ukiwa maini umekwisha.

Kwenye mapenzi ukiwa na moyo laini sana utateseka, ukiangalia watu wanaoteswa ni watu wenye mioyo laini, wenye mapenzi, unyenyekevu nk yani mtu moyo laini hadi akikosewa anaomba msamaha yeye. Ndugu zangu wa kiumeni roho ngumu sijui mmemuuzia nani hadi siku hizi mapenzi yanawaliza kama watoto hamkuaga hivi eti!!

Enzi hizo nikiwa sijachagua kuwa Nazi, jamaa mmoja alinipeleka puta alininyoosha, namzimia mbaya nae anajua anazimiwa basi simu nimtafute mie nikichuna anachuna, akiwa na kiu ndo anicheki kwa yale makopa nikiitwa natamani kupaa naona gari itanichelewesha. Pozi zikazidi mara simu asipokee uuuh sikomi napiga tu napiga tu mwisho nkajiona fala. Namba yake fyeka, picha msg na kila kitu fyekelea mbali nikauchuna japo naugulia siku inaisha ila kwa tabu oooh.

Wiki tatu zikakata wote kimya, najifanya Nazi nje mgumu ila huku ndani naugua, mara akaibuka na "hi" yani hi tu ikanitia nyegeee nyegezi mapenzi jamani mmmh nikakaushaa zikapita siku kadhaa ikaingia simu namba ngeni sio za Tz inaita mara mbili naicheki tu ya tatu nikapokea "mambo" kumbe ni yeye nikajifanya simjui "poa we nani", najibu kikauzu sauti ya kike nikaiacha kabatini mie flani kajitambulisha, huku moyo umejaa furaha ila najibu kawaida "okay ahsante" akaguna naona alikua haamini akajichetua nimesafiri nikirudi nitakucheki nami "ok" na simu nikakata utadhani nimepiga mie nikasikia rahaa makopa kopa nayaona. Nikawa narudi kwa ile namna naicheki tu nasmile sipigi wala nini.

Kesho yake akaanza upya I miss you much bla bla nikamjibu me too anashukuruuu ooh thanks, much thanks, nkajisemea pambafff kumbe kupendana unajua ila ule ulaini wangu ndo unakupa kiburi tukaanza kupendana tena ila moyo mlaini nikaudelete bora niugulie huko pembeni ila muda huo naweka roho ya nyau.

Nikamkumbuka jamaa yangu anavoliaga na mapenzi, mlaini hadi anaboa utadhani sio mwanaume. Ni vile tu kwenye mapenzi ya watu inatakiwa kuwa na ushauri neutral nisijekua mchawi kalaba hapo baade, mke nae kishamjua jamaa laini basi anamfanyia mapicha picha kosa afanye yeye na bado aombwe msamaha. Jamaa akinipa story anajitutumua yule mwanamke atanikoma nami nampoza jamani mapenzi uvumilivu kumbe namjua mwanaume maini tu hana lolote ataenda kuomba msamaha. Ukiona zengwe zinazidi punguza ulaini

Angalizo, za kuambiwa changanya na zako kabla hujaamua kuwa Nazi au firigisi angalia na mtu wako yukoje usijejifanya mgumu akapeperuka. Usikute alikua anakutafutia sababu umejifanya mgumu kumbe ndo umejikatia tiketi.
Alamsik
Sorry mkuu kuna sehemu ulikomenti as a man nikakuuliza mbona jina ni ke ukasema ni me,leo hapa unapost as ke,Duuh anyway labda unajinsia 2
 
wahoo big ideas
mim mwenyew dem wang wa kwanza alinitesag kinom lakin baada ya hapo wag na watesa kinom
 
Back
Top Bottom