Boss la DP World
JF-Expert Member
- Dec 12, 2021
- 2,318
- 8,464
Huyu mwamba alikuwa anafahamika sana kwa kupata mitihani ya form two iliyovuja na alikuwa anaipata ile yenyewe, alikuwa na moyo wa kuwapiga pindi wenzake na kuwakaririsha majibu, akiingia kwenye chumba cha mtihani anafeli kwa kishindo, yaani F zote, wenzake wanafaulu.
Alikuwa ni mtoto wa mwalimu wa Primary, mama yake aliamini katika elimu na elimu pekee, alianza primary kijijini kwao, akafaulu sekondari ya kijijini kwao alivyofika form II akafeli mara 2 mfululizo akafukuzwa (miaka hiyo ilikuwa ukifeli mara 2 unatimuliwa)
Mama yake akamtafutia nafasi City Secondary - Dodoma mjini, ni shule ya private, mwamba akafeli mara 2 akatimuliwa, mamayake akafanya mchongo akapata shule ya Central, akafanya mtihani akafeli mara 2, mama yake akacheza makaratee, akapata nafasi shule ya Jamhuri jamaa bila ajizi akajiunga akafeli mara 2.
Mama yake akampeleka chuo cha Donbosco pale Dodoma akasomea plumbing akawa fundi bomba (huenda mama yake aliona mabomba mengi ni ya duara kama namba 0)
Mshikaji sahivi anaendelea na ufundi na anaishi maisha ya standard nzuri tu. Siamini kama kuna mtanzania amemzidi huyu mwamba kwa experience ya kidato cha 2.
Mwenyewe anaamini NECTA walikuwa na kisa naye.