Kuna Mwanamke nampenda humu hadi Malaika wa Mbinguni wanajua, je nivunje ukimya ili afurahi?

Nafurahi sana kuona jinsi Wapendwa wangu wote ( nikimaanisha Members wenzangu wa JamiiForums ) jinsi mnavyoonyesha ushirikiano wenu mkubwa wa kuwepo na Mimi hadi hivi sasa na pia kukubali kunivumilia hadi hiyo Saa 4 hadi Saa 6 usiku wa leo ambapo nitavunja sasa rasmi ukimya. Na hii ni dalili njema sana Kwangu kwamba kumbe inaweza pia ikafika hiyo Saa 4 hadi Saa 6 usiku nisiwataje na nikiwaomba mnisubirie hadi Kesho Saa 3 na Nusu hadi Saa 5 Kamili bado mtaendelea tu kunipa ushirikiano wenu wa uvumilivu uliowatukuka. Ndiyo maana ninawapenda mno Wapendwa. Imarisheni tu huu uvumilivu wenu na endeleeni hivi hivi kuwa na subira.
 
Naona wale wasio na Umri huo kati ya 30 hadi 35 nilioutaja na ambao ndiyo huyo Mlengwa wangu anaangukia wameshaanza Kujitenga wenyewe kama mafuta yakiwa katika maji.
 
Mie pia sijambo Kaka. Nimefurahi kukuona leo.

Na kweli unachungulia tu sababu umekuwa adimu mno.

Haya bana Kaka uwe na jioni njema.
Inapendeza sana kusikia upo vyema sister.. Nitajitahidi nipangilie mambo yangu nisikosena tena jukwaani

Jioni njema kwako pia..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…