Yatazungumzwa mengi sana kuhusu Simba lakini kiukweli matatizo ya Simba mwaka huu sio Kanoute wala kiungo kwa ujumla. Matatizo makubwa matatu ya Simba ambayo yatawatesa sana Simba mwaka huu ni:-
1. Washambuliaji wa kati. Simba wanatengeneza nafasi nyingi sana kila mechi lakini hawana mshambuliaji wa kati mwenye uwezo wa kutumia nafasi hizo. Wanakosa mshambuliaji mwenye matumizi sahihi ya kichwa na miguu. Boko na Kagere wanaonekana umri umeaanza kuwa kikwazo na pia wana tatizo la "control". Mugalu sijui yeye huwa ana wasi wasi gani kwani huwa anafanya kila kitu kwa usahihi lakini linapokuja suala la kuutumbukiza mpira ndani ya nyavu hapo ndipo utamchukia. Chama na Luis walikuwa wanawafichia sana madhaifu yao ndio maana viongozi wa Simba hawakuligundua hili na hata hawakuhangaika kusajili mshambuliaji wa maana.
2. Timu nzima ipo "slow " sana, morali ipo chini sana na timu haichangamki kutafuta ushindi kwa nguvu mpaka waone aidha wamefungwa au waone muda unakaribia kwisha. Mpira ni mchezo wa makosa na ili umfunge mwenzio ni lazima umuwahi kabla hajajipanga vizuri. Sasa kwa aina ya uchezaji wa Simba wa sasa wa taratibu timu kupata ushindi ni ngumu sana kwani wakati wao wanaanza taratibu unakuta timu pinzani imeshajipanga vizuri kuzuia. Aina ya uchezaji wa taratibu ilikuwa inawezekana wakati Simba ikiwa na "play station" mbili Chama na Miquisone kwani wakishirikiana na Bwallya walikuwa wana uwezo wa kupiga pasi kwa usahihi kuanzia nyuma mpaka kwenye goli la mpinzani na kufunga au kutoa pasi za mwisho. Sasa wakati wanaume hao wawili hawapo bado benchi la ufundi linataka timu icheze katika mfumo ule ule wakati hawana wachezaji wenye uwezo kama Chama na Miquisone. Kiufupi Simba ina wachezaji wazuri lakini ni namna gani tu benchi la ufundi litakuwa na ubunifu wa mbinu, kubadili mifumo na kujua mchezaji gani atumike kwenye mechi ipi. Mfano mdogo sana ni jinsi Ajibu alivyoingia jana na kubadilisha kabisa mchezo jana timu ikaanza kutengeneza nafasi za magoli kitu ambacho kilikosekana kabisa kwa muda tangu Chama na Miquiosone waondoke.
3. Upigaji wa kona, krosi na faulu. Yaani ni kama benchi la ufundi huwa halifundishi chochote mazoezini jinsi ya kupiga hii mipira. Laiti kama Simba wangekuwa na mtu maalum aliyeandaliwa basi wangekuwa hawahitaji nguvu nyingi sana kupata magoli. Kwa mfano kwenye mechi ya jana kama sio ubunifu binafsi wa Ajibu na Mohamed Hussein mechi ingeisha bila bila japo Simba ilipata faulu zaidi ya kumi karibia na goli la Namungo. Kwenye krosi napo pana shida sana kwani mawinga na mabeki huwa wanapiga krosi ambazo hazina nguvu kabisa kiasi inakuwa rahisi mabeki kuziondoa au hata mshambuliaji akifanikiwa kuzigusa kwa mguu au kichwa basi zinakuwa hazina kasi ya kuingia golini.
Ni mtizamo tu.