watu kibao
JF-Expert Member
- Mar 25, 2025
- 466
- 1,663
Kama ilivyo kawaida, Ijumaa huwa napenda kwenda kupumzisha akili moja baridi, moja moto kwenye viwanja. Lakini leo hali ilikuwa tofauti kidogo. Rafiki yangu mmoja aliniomba nimpe kampani twende kwenye kiwanja ambacho yeye amekizoea.
Sikuwa na shida, tukasafiri pamoja hadi huko. Tulipofika, tukaanza kupiga stori huku tukifurahia vinywaji. Ghafla nikamuona jamaa mmoja ambaye zamani nilijua alikuwa na “crush” kwa ex wangu. ndie aliekuja kumuoa baada ya mimi kumuacha.
Cha kushangaza zaidi, kumbe ni rafiki wa yule jamaa niliyekuja naye. Wakaamkiana kwa staha, kisha kila mmoja akarudi kwenye meza yake. Ilipofika muda wa kuondoka, nikamweleza rafiki yangu kuhusu historia yangu na yule jamaa.
Ndipo akanishangaza kwa kuniambia kwamba huyo jamaa alianza kunywa mwaka jana tu, wakati zamani hakuwa mlevi hata kidogo. Pia huwa ana tabia ya kuondoka usiku wa manane somtimes analala gesti.
bila kujali. Kwa jinsi alivyonieleza, asilimia kubwa naamini mabadiliko haya yametokana na mwanamke aliyemuoa, yaani ex wangu. Huyu binti ana tabia za aina yake.
Tatizo lake sijawai kulijua ila yeye kumtuma kitu hata kama ni jukumu lake anaone anapelekeshwa, tuliwahi
Mifano ni hii
Kuna muda nilikuwa namwambia andaa msosi ataniwakia "kwani wewe huna mikono, siwezi kukaa na kitu rohon nakwambia ukweli kama utakasilika ni wewe"
Unaweza kumuelewesha kitu kwa upole anaanza kujibu kwa sauti kubwa yupo kwenye mode ya kutaka kupigana atasema "kwetu hakuna mnyonge na unajibiwa kama ulivyouliza unarudishwa kama ulivokuja"
Ilibidi niachie kamba tu, niliona hapo sio pahala pangu, baadae nikasikia kaolewa na yule jamaa mwenye crush kwake, nilishasema huyo alieoa ajipange kisaikolojia.
Nilipogundua tabia hizo siwezi kuishi nazo, nikaamua kuachia ngazi. Baadaye nikasikia ameolewa na yule jamaa niliyemwona leo, nilishasema mapema, huyo jamaa inabidi awe imara kisaikolojia maana safari aliyochagua si nyepesi. Kilichotokea leo kimenithibitishia nilichokitamka zamani. Maisha yanajifunza yenyewe, na muda mwingine kimya ni kinga.