Sasa kama unajielewa kaa mbali na watumishi wenye sermon mbovu kama wale. By the way kwanza watumishi wa Mungu wa kweli ni wengi sana, Mungu tu atakuongoza utampata bora na mwenye mafundisho sahihi.
shida ni kwamba, awali watu wengi huwa wanaitwa na Mungu, wana Mungu na wanaoperate kwa Nguvu za Mungu. along the way, tamaa ya pesa inaingia, kiburi na kutotii sauti ya Mungu kunakuja, dhambi hasa ya uzinzi na zingine zinafungua milango ya mashetani yanayowaingia, Mungu anaondoka, anawaacha wakiwa peke yao, ndipo sasa wanageukia njia ya shetani, na kutumia akili na elimu za kidunia kujaribu kuokoa roho jambo lisilowezekana. mwisho, ndio wanakuwa wapigaji tu ila awali walikuwa watu wa Mungu. simnyooshei kidole mtu. hata hao kina mzee wa upako na wengine wengi, usijefikiri awali hawakuwa watu wa Mungu, ni kwamba wamekengeuka na Mungu amewaacha waendelee na tamaa zao na aina ya maisha waliyochagua, na Mungu ameenda kwa wengine, Mungu ana watu wengi, ukileta kiburi kwake anakuacha anaenda kwa mwingine.
kwenye historia, Sauli Mfalme wa Israel alipendwa sana na Mungu, aliongozwa na Mungu, siku aliposhindwa kutii Sauti ya Mungu, Mungu alimwacha, akawa anaishi kwa akili zake mwenyewe hadi ikafika mahali akaenda kuagua kwa waganga, mtu aliyekuwa anasaidiwa na Mungu ikafikia hatua akageukiwa kwa mashetani kuomba msaada na direction.
wakati huo huo, Mungu alishaenda porini huko kwa kijana hata watu wasiyemdhania, Daudi akiwa machungani, akampaka mafuta kwa mkono wa Samweli, hivyo Sauli aliishi kitambo tu akiwa mfalme ambaye Mungu amemwacha, na Daudi aliishi kitambo tu akiwa amepakwa mafuta kuwa mfalme lakini bado yupo machungani. Mungu aliendelea kuwa naye hadi siku alipopigana na Goliath, kitambo tu akiwa rafiki wa Jonathan akiishi ikulu kwa saulu, ikulu ambayo Mungu alishampaka mafuta yeye ndio akae, alipowindwa na Sauli akaishi ukimbizini na maporini kwa miaka kadhaa....
ndio maana tunasema, hawa manabii na apostles wa uongo wameibuka, Mungu amewaacha, ila amejipakia mafuta watu wake halisi ambao katu huwezi kuwadhania, wale waliodharaulika ambao kwa macho ya kibinadamu huwezi amini kama watachukua tochi ya injili kuangaza kote ambako hawa wauza mafuta wamechafua, na Mungu atajitetea mwenyewe kama alivyojitetea kwa Daudi mbele ya Goliati.
I am not a pastor, lakini jambo ninalohakikishiwa ni kwamba, uchungaji hautakiwi kuwa sehemu ya kupata kipato cha utajiri, hata ukipata hela basi ziwe zinafanya kazi ya injili. vilevile, hautakiwi kuenenda kwa mwili, bali kwa Roho, that means, hata kuhubiri usihubiri kimwili, lazima Roho Mtakatifu ahusike, maneno yako hata kama yana elimu namna gani, yana saikolojia namna gani, una kipawa cha kuongea mbele za watu namna gani kama hayana Nguvu za Mungu, hayawezi kuokoa roho, ila popote alipo Roho wa Mungu lazima mguso na badiliko la wokovu wa Mungu lionekane, kwa wanaonielewa wamenielewa.