Kuna mzee wa miaka 90 kasema tangu azaliwe hajawahi kuona Uchawi

Kuna mzee wa miaka 90 kasema tangu azaliwe hajawahi kuona Uchawi

Red black

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2019
Posts
18,719
Reaction score
60,636
Leo nimepata wasaa wa kupiga story na mzee wa kiafrica akanimbia kwa umri wake wa miaka 90 hajawahi kuona uchawi toka amezaliwa anasikiaga tu.

Just imagine mzee wa miaka 90 hajawahi kuona hicho mnachosema magic
 
Si kwasababu uchawi lazima uwepo

Ila tunapata maana ya maisha kamili pale yanapoishia..!?

Maisha ni kujilisha upepo katika umaana wake mpumbavu

Ikiwa hii itaitwa kujifariji katika kutafuta maana katika kisicho na maana basi iwe jinsi ilivyo

Ila maisha yana ziadi ya yanayoishi hii ni bayana ya moyo sio kikokotoo

Kuna ziada_itungie kisa chochote cha wendawazimu lakini ziada itabaki ilipo na ni afya ya akili
 
Huo uchawi unaonekana? Mtu anaweza kugusa
Kwangu mimi kugusa na kutogusa si hoja.

Kwa sababu.

1.Kuna vitu vipo na hatuwezi kuvigusa.
2. Kuna vitu havipo na hatuwezi kuvigusa.
3. Kuna vitu havipo na tunafikiri tunaweza kuvigusa.
4. Kuna vitu vipo na tunaweza kuvigusa.

Kwa hiyo kugusa au kutogusa hakuthibitishi kitu kipo au hakipo.

Mimi huwezi kunigusa lakini nipo. Wewe kutoweza kunigusa haimaanishi sipo.

Kitu cha msingi zaidi kwanza ni ku define, uchawi ni nini?

Unapoona kitu, unajuaje huu ni uchawi na si jambo ambalo hujalielewa tu?
 
Leo nimepata wasaa wa kupiga story na mzee wa kiafrica akanimbia kwa umri wake wa miaka 90 hajawahi kuona uchawi toka amezaliwa anasikiaga tu.

Just imagine mzee wa miaka 90 hajawahi kuona hicho mnachosema magic
Je vingine vyote vilivyoko duniani amewahi kuviona? Je uchawi unaonekana kwa macho?
Una rangi gani
Una vipimo gani nknk
 
Uchawi/Ulozi vitu ambavyo mimi nimewahi hakiki kuwa vipo. Sio lazima na wewe msomaji wa comment yangu uamini hivyo. 😁
 
Je vingine vyote vilivyoko duniani amewahi kuviona? Je uchawi unaonekana kwa macho?
Una rangi gani
Una vipimo gani nknk
haya maswali wewe ndio ulipaswa ujibu mzee wa kilingeni
 
Hakunaga uchawi...haihitaji kuthibitishiwa na mzee ishu ndogo kama hiyo
 
Back
Top Bottom