Demi huo ukorofi kwa wewe fikra zako kwenye jambo hili zikoje, swali la msingi kushakiwa msingi wake ni nini? Ni kufanya kosa kisheria au kufanya jema kikanuni? It's a common sense
Juzi kati hapa mmewachukua wanaume ambao mmewatuhumu ni mashoga wakapelekwa muhimbili kwa vipimo, na ikatangazwa hadharani wamekutwa na mashimo...baada ya muda wakaachiwa huru hawana kesi tena.
Basi tu wabongo tumezubaa lkn wale jamaa walidhalilishwa kama wangeamua kufungua kesi wangeshinda.
Unafiki kama huu mtaufanya hadi lini? Kama jambo halina solution ni bora kukaa kimya.
Huyu mzungu umemtaja hapa nakwambia umempa promo ya kutosha, na vidume vitamiminika kwake kupata huduma.
Kama angekuwa na kosa la wazi wazi basi asingekuwepo hapo SUA miaka yote hiyo kama ni kweli anafanya huo upuuzi...
Ni kwamba wameona hawana grounds za kumshtaki watapoteza muda wao..
Ingekuwa anabaka au anawafanyia watoto wadogo siku nyingi angeshtakiwa. Lakini sheria ya ushoga ya Tanzania imekaa kinafikinafiki kwasababu serikali kama serikali haipingi ushoga bali madili ya Tanzania ndo yanapinga.
Watu wazima na akili zao wajifungie chumbani kufanya yao tutathibitisha vipi?
Wangefanya tendo hadharani ingekuwa rahisi kuwakamata sasa kwa situation kama hiyo uliyosema unataka watu wafanyeje?
Yule askari wenu wa zenji pamoja na videos za ushahidi kaachiwa huru kaonekana hana kosa sembuse huyo mzungu anayejifungia chumbani.
Hii vita ni ngumu na kuiongelea kama hivi ni kuipaisha. Kikubwa tuwalee watoto wetu katika njia sahihi angalau inaweza kuwaepusha .