Najaribu kuwaza namna tunavyonufaika na huu mfumo kandamizi unaofanya maisha yako na yamwengine kuwa mikononi mwa wengine .
Najaribu kuwaza namna unavyojihakikishia usalama kwenye mfumo wa namna hii .
Najaribu kuwaza namna unavyojihakikishia usalama kwenye family yako kuwa hakutatokea mwenye akili timamu atakaekua kuwa na tabia ya kuhoji na kudadisi ,unadhani nini itakujakuwa hatima zao? .
Nikukumbushe tu , siyo wote wanaopinga huu mfumo nikwamba hawanufaiki nao ,No ila wanayatenda hayo kwa maslahi mapana ya Taifa .
Wengi wa aina yako ni wale wasiyonufaika moja kwa moja zaidi ya ushamba maandazi au upungufu wa ufahamu .
Muhimu kujua sauti za watu ni sauti za Mungu ,imebakia siku moja ngoja tukae kwa kutulia.