Kuna ndugu wengine wakija kwako ni changamoto sana

Kuna ndugu wengine wakija kwako ni changamoto sana

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Kule chooni unapomaliza shughuli zako, huwa kuna zoezi la kuflashi ama kumwaga maji ili choo kiende, ila amini usiamini kuna choo hata uki flashi mara ngapi kitaibuka tu, hakunaaga utofauti na aina ya watu hawa.

- Kuamka saa tatu ama nne asubuhi.

- Muda mwingi ni kuchati, kupeleka playstation ya watoto chumbani kwake kucheza na marafiki zake, kupiga stori vijiwen, n.k

- Karidhika, umemtafutia kazi mshahara laki 3 hataki kisa ni saa 1 asubuhi hadi saa 1 jioni, weekend ni off , anadai kuna kazi ka apply serikalini anasubiri selection.

- Kaja kusalimia ila ni mwaka sasa unaenda na hajishughulishi.

- Chakula hata hakijawekwa mezani, yeye anaenda kupakulia huko huko jikoni.

- Kurudi usiku saa 2 ama 3

- Kuomba omba hela wakati kazi hataki
 
Ugeni hukomea siku 3. Baada ya hapo huyo ni aidha mwenyeji ama mlowezi.

Anakuwa mwenyeji pale anapojishughulisha hata kwa kusadia kazi za ndani.

Mlowezi ni kama hao ulioandika, hao huwa ni plain and simple kupewa nauli na kuambiwa warudi walipotoka. Huwa sio ombi ni taarifa/amri.
 
Ili usikosane nae, tafuta hata wiki, mpigishe jaramba la kwenda shamba daily. Asipoomba nauli, muajiri kama kibarua wako
 
Ili usikosane nae, tafuta hata wiki, mpigishe jaramba la kwenda shamba daily. Asipoomba nauli, muajiri kama kibarua wako
Huu ushauri upo level ya juu sana, sana unastahili pongezi. Safi Bangida

Ni kimjinimjini tu ndio wanapopata hizi kesi ila sio vijijini, vijijini mgeni akija mtalima pamoja, au mtapukuchua mahindi pamoja yaani raha tu. So unaweza kuiga kuona ni nini kinafanya ugeni kijijini uwe raha kuliko huu wa kimjinimjini.

Nyumbani kwako weka vitegauchumi vya kinyumbaninyumbani, kibustani, kaduka, kuuza barafu, ufugaji labda tukuku, mbuzi au ngombe wa maziwa kashughuli kadogo kauzalishaji mali. Home based economy

Na hii ni kwa upendo kabisa hata ndugu zako wakija wanajiskia vizuri kuwa na vishughulishughuli wanachangia. Sijui kuhusu wengine ila waliokulia vijijini suala la kukaa tu mchana kutwa huwa halimithiliki!! So unaweza kufanya hivyo ili wewe na yeye wote mjiskie vizuri na amani.
 
So unabuni mradi mzima ili kumfanya mtu akubali kufanya kazi?

Mi nakuambia uondoke tu.
 
Ukiona unachukia wageni Kuna mambo mawili tu yanayosababisha hilo 1.Uchumi wako Ni mgumu aukidhi Kuwahudumia 2.Una roho Mbaya.
Tuwapende Binadamu wenzetu.
 
Kama bado anaweza kusoma mlipie kozi yoyote
Ila hasira na matusi yatakufanya uwe na BP tu
Arudi alikotoka kama kazi amekataa
 
Roho mbaya tu, si mmlaze vyumba vya nje huko na choo cha nje huko huko,
 
Hata akipata kazi akapange. Ni Mimi na mke wangu + watoto. Siwezi kuhudumia zaidi ya hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa ukijilimit hivyo, utakuwaje mtu mkubwa? Great person

Ili uwe mkubwa zaidi ni mpaka pale utakapokubali kubeba majukumu zaidi. Hata hivyo sikupingi, kuridhika na ulichonacho nayo sio mbaya.
 
Back
Top Bottom