Kuna nini NIDA hadi vitambulisho havitoki tena?

Kuna nini NIDA hadi vitambulisho havitoki tena?

Nchi zetu changa zinapelekeshwa kila siku na ubeberu. Ukiwepo mpango wowote wenye maslahi kiuchumi kwa umma ila unakinzana na maslahi ya ubeberu au vikaragosi vyao unakwama.

Ni vigumu mtu kuamini sababu zinazotolewa kila siku kwanini mpango wa Serikali kuwapatia wananchi wake vitambulisho vyenye ubora mkubwa kukwama. NIDA kuna jambo.

Inaelekea kila Mkurugenzi mpya akiwekwa anakutana na jambo. Hebu niambieni mbona vitambulisho vya wapiga kura kwa ubora huo huo vinakamilika lakini vitambulisho vya Taifa vinasuasua. Kuna watu hawataki kila mtanzania atambulike kwa maslahi yao mabaya kwa taifa.

Ni muda sasa wa kutimua panya wanaotafuna mradi wa vitambulisho vya taifa usiende unavyotakiwa. Mabilioni yanapotea bila faida kamili iliyokusudiwa kwa mradi wa vitambulisho vya Taifa.

E0NhMwdXIAAW0HL.jpeg
 
Tangu mwaka juzi sijapata hiyo ID. Mwaka jana nikaenda pale Kawe kufuatilia.
Mama niliemkuta pale ile nampa tu kikaratasi lenye jina langu aangalie akanijibu kwa lisauti hilo kuwa hakijatoka, hata hakucheki kwenye kompyuta. Nyuma yake maboxi mengi yamejaa hizo ID. NIDA washenzi sana.
Nikatafuta full nakala kwa network zangu, nimeki-laminate na inanisaidia kwa sasa.
Nisaidie na Mimi nipate hiyo nakala
 
Umeuliza swali hili upate majibu au umeleta mada ili uwaseme mabeberu?.maana hata hujui tatizo ni nini umekazania kuwananga watu.inawezekana ulikua na hoja ila umeshindwa kuiwakilisha umeishia kusema watu bila kua na uhakika.sasa kwa hali hiyo sidhani kama unaweza kupata majibu sahihi toka kwa wahusika.
 
Nakumbuka siku naenda kuchukua changu tulikalishwa masaa matatu hakuna kitu kinaendelea,
Ila kuna watu wanafika wanachukua wanaondoka, tukaanzisha mtiti ndio wakatulia na kutuhudumia lakini walikua wajizungusha makusudi kumbe wanataka rushwa.

Hii nchi Rushwa haiwezi kuisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wakati wa Mwendakuzimu sio
 
Nchi zetu changa zinapelekeshwa kila siku na ubeberu. Ukiwepo mpango wowote wenye maslahi kiuchumi kwa umma ila unakinzana na maslahi ya ubeberu au vikaragosi vyao unakwama.

Ni vigumu mtu kuamini sababu zinazotolewa kila siku kwanini mpango wa Serikali kuwapatia wananchi wake vitambulisho vyenye ubora mkubwa kukwama. NIDA kuna jambo.

Inaelekea kila Mkurugenzi mpya akiwekwa anakutana na jambo. Hebu niambieni mbona vitambulisho vya wapiga kura kwa ubora huo huo vinakamilika lakini vitambulisho vya Taifa vinasuasua. Kuna watu hawataki kila mtanzania atambulike kwa maslahi yao mabaya kwa taifa.

Ni muda sasa wa kutimua panya wanaotafuna mradi wa vitambulisho vya taifa usiende unavyotakiwa. Mabilioni yanapotea bila faida kamili iliyokusudiwa kwa mradi wa vitambulisho vya Taifa.
Havitoki tena kwa wanaoanza kujiandikisha au hata kwa sisi ambao tulishapata namba?
 
Wanabana matumizi. Wanatoa namba tu siku hizi
 
Wameona hamna Baja kuendelea kutoa wakati yule Mwamba alishatoa tamko kua havihalalishi uraia, so havina matumizi tena, tuendelee kutumia vya kupigia kura.
 
Kuwa kijana na uaminifu vinafananaje?
Vijana watakaojua wajibu wao.

Vijana wazalendo.

Vijana watakao hakikisha shughuli kwa ajili ya maendeleo ya watu...na sio kuwaza pesa tuu.

Vijana wenye focus + speed ya kazi.

Vijana watakaopewa kazi na kuifanya kwa muda stahiki...au hata kabla ya muda wenyewe.

Ndio maana huwa nasema kunahitajika wapatikane wa namna hii,alafu mataasisi kama hayo yanafumuliwa wanawekwa damu mbichi.

Hope umenielewa.
 
Dr Magufuli kafa kila mtumishi sahivi kila anajiona yey ni raisi unategemea nin hapo.
Mkuu ni vyema ukaacha mahaba na mtu na uongee kwa kushirikisha vyema ubongo wako, unataka kuaminisha umma kua hayati ni bora kuliko yoyote na hakuna atakaeweza tena??? Kibaya zaid kinachofanyika kwa kundi lile ni kutafuta makosa kwa kila hali ili kum prove wrong Rais Samia, kuna mapungufu mengi sana huko mlipopaamini!!
 
Tangu mwaka juzi sijapata hiyo ID. Mwaka jana nikaenda pale Kawe kufuatilia.

Mama niliemkuta pale ile nampa tu kikaratasi lenye jina langu aangalie akanijibu kwa lisauti hilo kuwa hakijatoka, hata hakucheki kwenye kompyuta. Nyuma yake maboxi mengi yamejaa hizo ID. NIDA washenzi sana.

Nikatafuta full nakala kwa network zangu, nimeki-laminate na inanisaidia kwa sasa.
naomba mbinu kaka, umeifanyaje hyo!??
 
Kunywa maji ya kutosha kwanza then mabeberu hawajazuia wala hawatoi vitambulisho vya Nida. Acheni visingizio vya kishamba eti mabeberu !
Hilo swali kalize Nida au Wizara na watendaji wake.
 
Kweli hata suala hili tunaingiza mabeberu? Inchi hii bora lile paka lilikufa tu. Maana lilituharibia wtmatu mfano wako.
 
Dr Magufuli kafa kila mtumishi sahivi kila anajiona yey ni raisi unategemea nin hapo.
Hii dhana ya kizamani. Tuweke mifumo na uwajibikaji. Anayepewa dhamana halafu anazingua, anawajibishwa. Mambo gani ya kupigiana kelele tufanye kazi wakati sisi ni watu wazima? hatuoni aibu?
 
Back
Top Bottom