Kuna office nimeitembelea leo,office nzima mpaka mkurugenzi hawajui kuongea Kiingereza

Kiingereza ni lugha tu kama lugha zingine mfano Kimatumbi, kisukuma kiswahili n.k

Mnafundishwa kimatumbi shuleni? Maana mtu unasomea kingereza shuleni ila huna uwezo wa kukutumia, Sasa cha nini kujisumbua...
 
Aliekwambia ukurugenzi ni kujua kiingereza nani.
Ni kukosa kujiamini tu...Mimi mtu akija kwangu ataongea Kiswahili kama hataki atajua mwenyewe! Kama lafudhi yao huipati vizuri ndio ufanye Siri! Mwambie aongee kwa hatua😐
 
Wew unaejuwa kiingereza unawazidi nini hasa?!
 
Ni kawaida mkuu, sio wote ni wazuri kwenye kingereza hasa cha kuongea tena na wenye lugha yao.

Mngekua mnaandika na yeye anajibu labda angeweza ila sio kuongea papo kwa hapo
 
Ach
Acha ulimbuke dogo.
 
Acha utumwa wa kifikra, ulivyo mshamba unashangaa mtanzania kutokujua kiingereza ila hushangai wageni wako kutokujua kiswahili!
Kingereza ni lugha ya kimataifa
 
Vituko ni vingi kwemye maofisi wanapotembelea wageni. Huko mashuleni ndio utashangaa zaidi mkuu wa shule na makamu wake kukimbia na kukuachia msala uzungumze kiingereza na wageni wanaokuja shuleni. Nasema inaudhi sana na kukera bosi kuingia mitini kisa hajui kuongea kiingereza vema wakati amesoma mpaka form six hadi chuoni na degree anayo. Pumbavu sana, wakiambiwa wakasome ufundi VETA na hizo degree zao povu linawatoka na kudai wamedharauliwa
 
unashanga mkurugenzi wa ofisi wakati rais wa China taifa kubwa duniani katika kila kitu na yeye pia hajui kingereza
China hawahitaji sana English lakini wewe Mswahili unahitaji sana English.
 
Jeni Mhagama
 
mura kyagata nomonto waweito ole serengeti tantoli emelemo..
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Though I can not speak much English
 
Wachina hawahitaji Kingereza sana, wao ni mojawapo ya utamaduni wa kale zaidi duniani, wana watu bilioni 1.4, ni uchumi namba mbili kuwa ukubwa duniani.
 
Hukumu za mahakama zinaandikiwa Kingereza
 
unashanga mkurugenzi wa ofisi wakati rais wa China taifa kubwa duniani katika kila kitu na yeye pia hajui kingereza
Nilitaka kuandika kama wewe umeshanisaidia.Xi Jipin wa China,Putin wa Urusi wote hawa hawajui kingereza lakini mataifa yao yako juu.
 
Kiswahili chenyewe kwa wengi bado ni tatizo mtu anasema karamu badala ya kalamu, awachezi badala ya hawachezi au ridhiki badala ya riziki.
 
Acha ubwege, nchi kama Spain, Italy, France au ukienda kusini mwa Ubelgiji, kule madaktari, wanasheria na hata wafanyakazi waserikalini hawajui kiingereza.
Uongo, hizo nchi zote raia akisoma Kingereza lazima akijue vizuri sana.
Macron anaongea Kingereza kizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…