Kuna ofisi ukizitembelea unakuta 'staff' wake wanatia huruma sana kwa kweli

Kuna ofisi ukizitembelea unakuta 'staff' wake wanatia huruma sana kwa kweli

Watu wana maisha Duni, hivyo wanajaribu kuvumilia tu

Wanasema mtumikie kafiri upate Mtaji wako

Sawa kabisa mkuu.

Ndio maana mimi nikataka kuweka hoja yangu kwamba, ajira pia ni soko huria. Huwezi kumlazimisha mtu alipe 310,000/= wakati huenda gharama za uzalishaji, usambazaji, marketing na kodi za serikali pia zinambana hivyo ili apate faida kidogo inabidi abanane na wafanyakazi. Hapo bado wafanyakazi hawajamuibia, kumpa hasara kwa uzembe n.k na sisi watu weusi tunajijua mambo yetu tuna tamaa sana na tunapenda short cut.

Pia nafahamu waajiri wanyonyaji pia lakini soko linaendeshwa na principle of demand and supply. Kukiwa na watu wachache walio tayari kufanya kazi huko maviwandani kwa wahindi, lazima watapandisha ili kuwavutia watu waache kilimo na ufugaji vijijini waje mjini.

Serikali haina cha kufanya hapo.​
 
Waache Wachina/Wahindi waendelee kuwanyonya ndugu zetu

Serikali si imelala

Kwa mujibu wa maelekezo ya Serikali, kima cha Chini cha mshahara kilipaswa kuwa 310,000 lakini wapo wafanyakazi kwenye hivyo viwanda vya Wahindi/Wachina wanalipwa 150,000 Kwa Mwezi, hapo nauli ya mfanyakazi

Ukija wafanyakazi wa ndani, nao wanalipwa elfu 30 hadi 50

Kwa kweli hali mbaya mno
Bora hata mfanyakazi wa ndani hamsini inakuwa ni keshi,sasa hawa wa laki na nusu ukodi chumba,ule na ununue mahitaji mengine.
 
Kuna Mthailand anasema"Africa ni eneo sahihi la kutafutia mtaji".

Wa Asia wanakuja mikono mitupu kisha wanadhaminiwa na balozi zao taasisi za fedha za nje au za ndani kisha wanaanza kazi.
 
Bora hata mfanyakazi wa ndani hamsini inakuwa ni keshi,sasa hawa wa laki na nusu ukodi chumba,ule na ununue mahitaji mengine.
Ni kweli, huyo wa kazi za ndani ana uhakika wa kunywa chai, chakula cha Mchana, na dinner.

Kwahiyo akisema asevu, anaweza kuwa na Salio kubwa mwisho wa Mwaka kuliko huyo mfanyakazi wa Mhindi anayelipwa laki 1.5 Kwa Mwezi 🙌
 
Ni kweli, huyo wa kazi za ndani ana uhakika wa kunywa chai, chakula cha Mchana, na dinner.

Kwahiyo akisema asevu, anaweza kuwa na Salio kubwa mwisho wa Mwaka kuliko huyo mfanyakazi wa Mhindi anayelipwa laki 1.5 Kwa Mwezi [emoji119]
Uhakika
 
Leo bana nilikua nataka bidhaa flani ila kwa bei ya jumla,so jamaa angu flani akaniunganisha na hao sijui ni wahindi au wachina wale nikaenda kwenye hiyo office kupata hiyo bidhaa.
Kwanza getini ile unaingia tu mlinzi anakuomba buku la maji.
Ukiingia ndani unakuta staff muda wa lunch wamelala chini ya miembe huku wengine wanatungua maembe kwa mawe,wengine muda wa lunch wanakula mihogo na energy drinks.
Dah,nimesikitika sana kwa kweli.
Uko njombe? Maana maeneo yà kutungua maembe kwa mawe mjini kama dar hayapo!
 
Back
Top Bottom