Ifikie wakati tuache usimba na uyanga kwenye timu ya taifa. Kwanza kuhusu Mauya binafsi mimi hua simwelewagi na mara nyingi hata ukiingizwa sub kipindi cha pili unaona Yanga wanavyokata upepo. Mauya bado sana, ila kuhusu Kibwana kuwa ndiye chanzo cha goli kisa tu Mwenda katoka na kuchukua nafasi yake hilo nakataa. Kipindi cha kwanza ambapo huyo Mwenda alikuwepo, Taifa stars tungeshafungwa magoli yasiyopungua mawili, ashukuriwe Manura kwa kufanya kazi ya ziada. Kwahiyo hata kipindi cha kwanza huyo Mwenda alizidiwa na Manura kusahihisha makosa ya mabeki wake