Ngoja nikuelekeze kisha tusipoelewana utajua mwenyewe.
Nina kichwa chepesi sana kuelewa na kushika mambo. Hili ondoa shaka.
Tuendelee.
Nimefuatilia hoja zako za picha na madai ya maigizo na hitimisho langu ni kuwa wewe umejikita kwenye picha ambazo ni za kutengeneza ili kumpa taswira rahisi ya uelewa msomaji asiye mwanasayansi na ukatoa hitimisho kuwa ni maigizo.
Safi kabisa nashukuru kwa kukiri kwako ya kuwa hizo ni taswira bunifu.
Kingine sijajikita tu katika picha kama umenisoma vizuri nimejikita kadhalika katika uhalisia.
Hii ni sayansi na ina kanuni na hatua zake zake kufikia hitimisho juu ya jambo fulani.
Kadhia inayo elezewa hapo haina njia nyingine mbadala zaidi ya kufika sehemu husika zaidi ya hapo ni makadirio na ndiyo maigizo yenyewe.
Kama waliweza kutoa hitimisho kwanini waliweka picha bunifu na si picha halisi.
Sasa mfano tukiachana na picha ukatumiwa namna wanavyogundua kuwa sayari fulani ina mazingira yanayofanana na dunia ukaletewa zile namba, dots na signals ungeelewa?
Hoja hii haina haja ya kuletewa dots wala nini ni jambo la kueleweka wazi wala halihitaji signals,ni sawa sawa na wanavyolezea maji kwa mujibu wa kemia jambo ambalo maji ni kitu naarufu na hakihitaji kiarifisho (definition) ya kisayansi ndiyo maana wanakosea.
Swali la msingi kwanini waelezee kwa dots au signals jambo ambalo kama kweli wamelidiriki ni kuthibitisha tu. Ni sawa sawa na wewe useme umemuona Ali,kisha kisha umuelezee kwa mtindo ambao hauna uhusiano na Ali.
Umeshawahi kuona mtu akihojiwa polisi akawa anatoa maelezo ya namna mhalifu alivyo halafu kuna mtu anamchora, kisha baada ya hapo inatoka picha inayofanana na mhalifu jinsi alivyo?
Mfano wako haingii hapa sababu sharti la kwanza ni mtu husika amemdiriki mtu husika na wala hapakuwa na haja ya kumchora mtu huyo. Na ushahidi huu hauna mashiko mpaka muhusika adirikiwa yaani picha hufanana na watu hufanana pia. Kwahiyo akiyemuona fulani lazima akamuonyeshe huyo fulani.
Lakini kinachofanana na fulanindi chenyewe hicho.
Sasa hizi taarifa zinazotumwa na vyombo vya anga ni mfano wa huyo mtu na kuna wachoraji wanaochora ili taswira ya picha itokee kurahisisha ile taarifa.
Ngoja nikusaidie kitu kimoja ushawah kuthibitisha au kuhakiki ya kuwa kuna chombo chochote kimewahi kufika kwenye sayari nyingine ? Au unaweza kuthibtisha juu ya uwepo wa Sayari nyingine zaidi ya Dunia ?
Hujiulizi kwanini watu hawajaenda tena mwezini tangu yale maigizo ya Neil ? Wanasingizia bajeti ni kubwa imeshipatia miaka zaidi ya 30 sasa bado tu hawajajipanga kwenda tena ?
Sasa uhalisia upo na tunaishi nao haya maigizo watawaigizia nyinyi msio fikiri na kuhoji na kuhakiki mambo.
Unajua kuwa ubongo wako unatafsiri vipi kuwa huyu ni mtu fulani baada ya kumwangalia?
Najua.
Bila wewe kujua kwa haraka sana ubongo wako unapima alama za urefu wa pua, upana wa mdomo, umbali kutoka pua na mdomo, upana wa paji la uso, mzunguko wa jicho n.k kisha unatoa hesabu kamili na kutuma taarifa za utambuzi kuwa huyu ni fulani ila wewe unachoona ni taswira ya picha yenye rangi ambayo unatengenezewa na huo huo ubongo ili kukurahisishia huo utambuzi.
Hizi stori achana nazo jikite katika hoja ya msingi.
Rangi unazo wewe sio ile object au mtu unayemuangalia. Ubongo wako kupitia macho yako unageuza namba na taarifa za kitu ili wewe ukitambue kwa mfumo wa rangi na picha au tuseme video. Sasa hichi ndicho wakifanyacho wanasansi mpaka unaziona picha ambazo unahisi ni maigizo.
Usiidharau teknolojia na kuiita maigizo,nilikuwa nafuatilia historia ya ugunduzi wa ndege kuna watu walikuja na theory kuwa binadamu angetakiwa kupaa angezaliwa na mabawa tuache kumkufuru muumba. Leo binadamu wanapaa.
Hizi stori mzee achana nazo jenga hoja na kosoa hoja na hakiki hoja na thibitisha hoja.
Nakuuliza swali dogo ukitaka kupima tungamo ya kitu au kipenyo cha kitu sharti ni lipi au masharti ni yapi ?