mjingamimi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2015
- 42,209
- 51,004
Ukienda anga za juu kabisa huko.Sasa kama tofali ni kubwa kuliko Dunia. Eti wanatuma kifaa kilichotoka Duniani kikagonge hilo. Lidubwana. [emoji849][emoji1787][emoji848][emoji848]. Si litakivuruga hiko kifaa chenu chenye ukubwa hata hafiki wa nchi moja.... Au wanamabomu mazito ya kuvunja hilo lijiwe ambalo ni kubwa snaaaa kiasi kwamba Dunia ni kama mchanga???
Sasa kama tofali ni kubwa kuliko Dunia. Eti wanatuma kifaa kilichotoka Duniani kikagonge hilo. Lidubwana. [emoji849][emoji1787][emoji848][emoji848]. Si litakivuruga hiko kifaa chenu chenye ukubwa hata hafiki wa nchi moja.... Au wanamabomu mazito ya kuvunja hilo lijiwe ambalo ni kubwa snaaaa kiasi kwamba Dunia ni kama mchanga???
Nyinyi nikimaanisha waislamu, na sio lazima mpaka uwepo wewe miongoni mwa hao watu waliosema hivyoUliposema nyinyi mimi umenitoaje katika tamko nyinyi ?
Wakati naanza kukupa maelezo ya hoja yangu nilisema hivi ndugu mubarrid:Nina kichwa chepesi sana kuelewa na kushika mambo. Hili ondoa shaka.
Tuendelee.
Safi kabisa nashukuru kwa kukiri kwako ya kuwa hizo ni taswira bunifu.
Kingine sijajikita tu katika picha kama umenisoma vizuri nimejikita kadhalika katika uhalisia.
Hii ni sayansi na ina kanuni na hatua zake zake kufikia hitimisho juu ya jambo fulani.
Kadhia inayo elezewa hapo haina njia nyingine mbadala zaidi ya kufika sehemu husika zaidi ya hapo ni makadirio na ndiyo maigizo yenyewe.
Kama waliweza kutoa hitimisho kwanini waliweka picha bunifu na si picha halisi.
Hoja hii haina haja ya kuletewa dots wala nini ni jambo la kueleweka wazi wala halihitaji signals,ni sawa sawa na wanavyolezea maji kwa mujibu wa kemia jambo ambalo maji ni kitu naarufu na hakihitaji kiarifisho (definition) ya kisayansi ndiyo maana wanakosea.
Swali la msingi kwanini waelezee kwa dots au signals jambo ambalo kama kweli wamelidiriki ni kuthibitisha tu. Ni sawa sawa na wewe useme umemuona Ali,kisha kisha umuelezee kwa mtindo ambao hauna uhusiano na Ali.
Mfano wako haingii hapa sababu sharti la kwanza ni mtu husika amemdiriki mtu husika na wala hapakuwa na haja ya kumchora mtu huyo. Na ushahidi huu hauna mashiko mpaka muhusika adirikiwa yaani picha hufanana na watu hufanana pia. Kwahiyo akiyemuona fulani lazima akamuonyeshe huyo fulani.
Lakini kinachofanana na fulanindi chenyewe hicho.
Ngoja nikusaidie kitu kimoja ushawah kuthibitisha au kuhakiki ya kuwa kuna chombo chochote kimewahi kufika kwenye sayari nyingine ? Au unaweza kuthibtisha juu ya uwepo wa Sayari nyingine zaidi ya Dunia ?
Hujiulizi kwanini watu hawajaenda tena mwezini tangu yale maigizo ya Neil ? Wanasingizia bajeti ni kubwa imeshipatia miaka zaidi ya 30 sasa bado tu hawajajipanga kwenda tena ?
Sasa uhalisia upo na tunaishi nao haya maigizo watawaigizia nyinyi msio fikiri na kuhoji na kuhakiki mambo.
Najua.
Hizi stori achana nazo jikite katika hoja ya msingi.
Hizi stori mzee achana nazo jenga hoja na kosoa hoja na hakiki hoja na thibitisha hoja.
Nakuuliza swali dogo ukitaka kupima tungamo ya kitu au kipenyo cha kitu sharti ni lipi au masharti ni yapi ?
Huu ujinga mwingine sasa,suala la mwezi wa ramadhani ni waislamu wote hufunga isipokuwa walio kwenye dharura na ramadhani ni nguzo katika nguzo ya uislamu.Nyinyi nikimaanisha waislamu, na sio lazima mpaka uwepo wewe miongoni mwa hao watu waliosema hivyo
Nikisema mwezi wa ramadhani waislamu wanafunga, hiyo ina maana kila muislamu lazima awe amefunga?
Kwa hiyo wasiofunga wote katika hicho kipindi ni lazima wawe na dharula?Huu ujinga mwingine sasa,suala la mwezi wa ramadhani ni waislamu wote hufunga isipokuwa walio kwenye dharura na ramadhani ni nguzo katika nguzo ya uislamu.
Mintarafu ulilolisema si nguzo wala si tawi katika dini bali ni waislamu wachache wajiitao watetezi hudai hilo. Ndiyo maana kauli yako si sahihi na mfano wako si sahihi sababu umeweja lisilo husika.
Naam.Kwa hiyo wasiofunga wote katika hicho kipindi ni lazima wawe na dharula?
kwa research gani?Naam.
Kwa mujibu wa kaida za kiusuli.kwa research gani?
Kaida za kiusuli hufanya survey kila nyumba?Kwa mujibu wa kaida za kiusuli.
Inaonekana hujaelewa nini nilichokiandika ndiyo maana ukauliza swali lisilo hitajika. Hili ni swali la pili umeuliza na umekosea kuuliza,la kwanza ni hilo kuhusu research,unaongelea research katika suala la kaida ?Kaida za kiusuli hufanya survey kila nyumba?
Mimi nimehoji kutaka kujua majibu yaliyopatikama exacly kupitia research na sio makadirioInaonekana hujaelewa nini nilichokiandika ndiyo maana ukauliza swali lisilo hitajika. Hili ni swali la pili umeuliza na umekosea kuuliza,la kwanza ni hilo kuhusu research,unaongelea research katika suala la kaida ?
Sasa unafanyaje research juu ya kitu ambacho hujui misingi na hukumu zake zikoje ?Mimi nimehoji kutaka kujua majibu yaliyopatikama exacly kupitia research na sio makadirio
Hoja yangu inahusu kujua majibu kwa research kuhusiana na waislamu ambao hawafungi katika hicho kipindi kwanini wote wawe na dharula?
Mi nimekuuliza, hizo statistics zako kua wasiofunga huwa na dharula ni based kwenye research au ni personal speculations zako tu?Sasa unafanyaje research juu ya kitu ambacho hujui misingi na hukumu zake zikoje ?
Hizi hatua za research/ tafiti mmefundishwaje huko mavyuoni ?
Hili nimeshakujibu tayari ndiyo maana nikashangaa tafiti zenu mnazifanyaje ? Yaani unachokiandika katika Uislamu wetu hakipo na nashangaa zaidi kuniuliza kuhusu takwimu. Vijana muwe mnasoma haya mambo siyo mnakurupuka.Mi nimekuuliza, hizo statistics zako kua wasiofunga huwa na dharula ni based kwenye research au ni personal speculations zako tu?
Umenijibu wapi kuonesha research uliyofanya kila nyumba iliyokuwa na waislamu ambao hawakufunga walipatwa na dharula?Hili nimeshakujibu tayari ndiyo maana nikashangaa tafiti zenu mnazifanyaje ? Yaani unachokiandika katika Uislamu wetu hakipo na nashangaa zaidi kuniuliza kuhusu takwimu. Vijana muwe mnasoma haya mambo siyo mnakurupuka.
Tuwaache wenzetu wapambane [emoji16][emoji16]Title yako imekaa kishabiki shabiki na kiumbea umbea mno. Unnecessary sensationalism! (Afadhali mods wameibadilisha!)
Wanasayansi wanaamini kuwa huko nyuma dunia ilishawahi kugongwa na mawe haya makubwa (asteroids) na wana ushahidi huo. Jiwe la mwisho ni hili lililoua viumbe wengi duniani na kuondoa ufalme wa akina dinosaurs; na wanyama wengine lukuki.
Mawe haya yanasafiri kwa kasi ya ajabu na yanapopiga uso wa dunia yanavuvumua vumbi na uchafu mwingi ambao unaweza kubakia angani kwa miaka mingi. Vumbi na uchafu huu huenea dunia nzima na kuziba miali ya jua kabisa kabisa mpaka dunia inaingia katika kile wanachokiita deep freeze. Ina maana dunia inaganda kabisa na kutandwa na barafu kwa vile hakuna mwanga wa jua kwa muda mrefu. Na bila mwanga wa jua ina maana hakuna photosynthesis wala nishati ya aina yo yote. Matokeo yake ni vifo vya jumla kwa viumbe wengi.
Yapo mawe yanayoonyesha kuwa yatakuja kuipiga dunia huko mbele ya safari na NASA wana kitengo maalum kinachoshughulika na tatizo hili na mpaka sasa kuna nadharia tatu zilizopendekezwa kuweza kujiponya siku ikigundulika kuwa kuna jiwe linatujia huko:
1. Kurusha chombo chenye uzito na nishati maalum na kwenda kuligonga hilo jiwe huko angani likiwa mbali na dunia. Lengo hapa siyo kulisambaratisha bali ni kujaribu kulisukuma kidogo (nudge) ili liweze kuacha njia yake ya mzunguko (orbit) na hivyo kuliepusha kugongana na dunia.
2. Kurusha rocket yenye nguvu iliyobeba bomu kubwa la nyuklia na kwenda kulitandika hilo jiwe na kulisambaratisha. Hii hata hivyo inaweza tu kuishia kulimega hilo jiwe katika vipande vingi ambavyo vinaweza kuleta hatari zaidi duniani. Na kukitokea mushkeli wakati wa kurusha hiyo rocket hilo bomu linaweza kuturipukia hapa hapa duniani na kuleta madhara makubwa.
Ili kuepuka kulimega vipande vipande lipo pendekezo la kwenda kulipua bomu hilo karibu na jiwe hilo. Ile nguvu ya mripuko (boom) inaweza kutosha kulisukuma kidogo hilo jiwe likiwa zima na kuliondoa katika orbit yake.
3. Kurusha chombo chenye mionzi mikali ya laser na kwenda kujaribu kulimulika jiwe hilo na mionzi hiyo. Mawe haya mengi yana barafu iliyoganda na likipigwa na mionzi mikali kwa muda barafu inaweza kuyeyuka na hivyo kupunguza uzito wake na hii, wanadai, inaweza kusababisha liondoke kwenye orbit yake inayolifanya ligongane na dunia.
Hata bila kuyeyusha barafu yake, mionzi hii ya laser inaweza kufanya kazi sawa na utando wa buibui na hivyo kulisogeza jiwe hilo polepole nje ya orbit yake na hivyo kuepusha mgongano wake na dunia.
NASA leo wamerusha chombo kujaribu nadharia ya kwanza kama inafanya kazi kwa sababu dunia kupigwa na asteroid nyingine ni suala la muda tu. Elon Musk anarusha maroketi haya kila leo hatusikii cho chote lakini leo umeshusha ushabiki wa kufa mtu eti anga lilibadilika. Lilibadilika wapi? Labda kama ulikwenda kushuhudia wakati roketi hilo likirushwa huko California. Ni wazi hii habari hukuiandika mwenyewe na umefanya plagiarism mahali fulani (BBC Swahili) na sina uhakika kama una ufahamu wa kutosha na habari yenyewe pamoja na implications za kiujumla za kinachozungumziwa.
Wakati tunahangaika na tozo, ufisadi wa kutisha, kutengeneza madawati, kujenga nyumba za walimu, kujenga vyoo vya shimo vya kutosha mashuleni, ushirikina, ukosefu wa umeme na maji, siasa za hovyo za kuoneana hizi, wenzetu huko hawalali wanahangaika na mambo kama haya mazito. Tuombe wafanikiwe kwa sababu siku moja pengine wataweza kuokoa maisha ya viumbe hapa duniani. Hata wakishindwa wao pia wanahangaika kutafuta makazi katika sayari zingine huko wanaweza wakaondoka zao na kutuacha hapa siku mambo yakibumburuka!
N.B: Bajeti ya NASA kwa mwaka huu wa fedha ni dola bilioni 23.3. Bajeti nzima ya nchi yako kwa mwaka huu wa fedha ni kiasi gani?