Kuna Sauti inanijia kwamba huenda wabunge 19 wa CHADEMA wana baraka za Mwenyekiti kwa makubaliano maalumu kutotoboa siri

Kuna Sauti inanijia kwamba huenda wabunge 19 wa CHADEMA wana baraka za Mwenyekiti kwa makubaliano maalumu kutotoboa siri

..Utaratibu ni kwamba wabunge wanateuliwa na vikao vya chama.

..hata kama "wabunge" hao walipewa "baraka" na Mwenyekiti, na wakaandikiwa barua na Katibu Mkuu, bado ubunge wao sio halali kwasababu hakuna kikao cha Chadema kilichopitisha maamuzi ya kuwateua.

..Na kwa bahati nzuri, au mbaya, wengi wa waliokwenda bungeni ni wajumbe wa vikao vyenye mamlaka ya kufanya uteuzi wa wabunge. Kwa msingi huo wengi wanaelewa kwamba kilichotokea ni kinyume na taratibu na sheria.

..Kuna wakati Spika Ndugai alikataa kupokea barua toka kwa Katibu Mkuu wa Chadema kwa madai kwamba haikutokana na maamuzi ya vikao vinavyotambulika vya chama hicho. Sasa imekuwaje safari hii Spika anakiuka utaratibu aliojijengea awali?

..Katika suala hili Tume ya Uchaguzi na Spika wa Bunge walipaswa kuzingatia maamuzi ya vikao vinavyotambulika vya chama ktk uteuzi wa wabunge wa viti maalum wa Chadema.

..Ni bahati mbaya sana Tume ya Uchaguzi na Spika wameziba masikio hata pale walipoelekezwa na Chadema kwamba chama hakikuhusika ktk kuteua wabunge wa viti maalum.

NB:

..Halima na wenzake wangemhitaji Mbowe kama wangekuwa wanapitisha mambo yao ktk vikao vya chama. Hiki kilichotokea hakikuhitaji "baraka" za Mbowe, sana sana kilihitaji collusion kati ya Halima na kundi lake, Tume ya Uchaguzi, na Spika wa Bunge.
 
Kwa jinsi ulivyoandika wewe utakuwa kiongozi wa juu wa Chadema unayetaka kututoa nje ya mada ya mleta mada

mleta mada ana hoja nzito ambayo wewe unahangaika kutaka ku i divert tuhamie kwingine
Wewe unaakili mbovu. Kila kinachoandikwa unaweka 'spin'yako mwenyewe unayoitaka.

Naona leo nimekupa 'privilege' kwelikweli, heshima usiyostahili kwa kujibishana nawe kiasi hiki.

Nakuachia uwanja uendelee kama kawaida yako.
 
Mkuu vichwa vingi unavyodili navyo reasoning ipo very low. Angalia maswali wanayouliza majibu yapo wazi sana. Watu hawajui Ila fukuza ya wabunge ilikuwa zuga. Ndugai alisema alipokea barua toka kwa Mnyika ikiwa imesainiwa, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi akadhibitisha. Kama sio kweli mbona Mnyika hajawahi kwenda mahakamani kudai sahihi yake imefojiwa..!???????

..Hata kama Mnyika aliandika barua, bado wabunge hao sio halali kwasababu hawakuteuliwa na vikao halali vya chama/chadema.

..Spika kama ana barua toka kwa Mnyika alitakiwa akamshitaki kwa kulidanganya Bunge kwa kuandika barua ya kugushi ya uteuzi wa wabunge viti maalum.
 
Mbona hili tunasema kila siku?

Ni vile tu Mbowe ana wafuasi mbumbumbu, lakini wangekuwa wanajielewa wangeshaagutuka zamani.

Kwa action hii ya kizalendo, unamuunga mkono Mbowe au unaungana na BAVICHA kupinga?
 
CCM ndio waasisi wa haya yote. Ila dawa ya haya yote ni katiba mpya tu itakayompa nguvu mwananchi kumwajibisha mtumishi yeyote wa umma
Mkuu ata katiba ya sasa ipo wazi katika ili.Soma ibara ya 8(1)d Serikali itawajibika kwa wananchi
 
Naona hili sasa sio jukwaa la siasa tena, ni jukwaa la hisia, mods badilisheni jina.

Upuuzi unaachwa unatamalaki sana humu.
"JUKWAA LA SIASA"?

Kuna umuhimu kwa wahusika wa JF kufikiria kwa makini sana wazo hili ulilolianzisha hapa.
 
Kwa action hii ya kizalendo, unamuunga mkono Mbowe au unaungana na BAVICHA kupinga?
Mbowe linapokuja suala la hela huwa haangalii mtu usoni.

Ukikumbuka ishu ya Lowasa kuwasili chadema, unaona kabisa hakuna linalo shindikana kwa Mbowe.

Kwahiyo mimi niko upande wa bivicha kumpinga Mbowe tena aondolewe kwenye hiyo nafasi
 
..Hata kama Mnyika aliandika barua, bado wabunge hao sio halali kwasababu hawakuteuliwa na vikao halali vya chama/chadema.

..Spika kama ana barua toka kwa Mnyika alitakiwa akamshitaki kwa kulidanganya Bunge kwa kuandika barua ya kugushi ya uteuzi wa wabunge viti maalum.
Hapo umejitutumua kuelewa na kujibu!??.. Kuna tatizo mahali kwenye vichwa vyenu,vikao vya chama vinamuhusu nini Ndugai!?. Kama vimefanyika usiku wa manane au online afatilie!?. Jukumu lake ni kupokea barua yenye list ya wateuliwa toka kwa katibu mkuu na kuifanyia kazi FULL STOP. Vikao havimhusu kabisa. Ondoa uchama kichwani utanielewa.
 
Hata mimi nawaza hivyo.

Hata lile kanusho la kutopokea ruzuku hata siliamini. [emoji21]
Kwani unaamini Nini kutoka chadema labda tuanze hapo. Na je Kuna kitu unaweza kukiamini kikisemwa na chasema au huamini chochote?
 
Hapo umejitutumua kuelewa na kujibu!??.. Kuna tatizo mahali kwenye vichwa vyenu,vikao vya chama vinamuhusu nini Ndugai!?. Kama vimefanyika usiku wa manane au online afatilie!?. Jukumu lake ni kupokea barua yenye list ya wateuliwa toka kwa katibu mkuu na kuifanyia kazi FULL STOP. Vikao havimhusu kabisa. Ondoa uchama kichwani utanielewa.

..Spika Ndugai ana utaratibu wa kujiridhisha kuhusu masuala ya vikao vya chama, kabla hajachukua maamuzi yanayomhusu Mbunge.

..Nakuomba urejee tukio la Spika wa Bunge kuikataa barua ya KM Chadema kumfukuza Cecil Mwambe kwasababu haikuwa na reference ya kikao halali cha chama.

..Again, anayeteua wabunge wa viti maalum wa Chadema siyo Katibu Mkuu wa chama, bali ni kamati kuu ambayo bado haijakaa kufanyia uamuzi suala hilo.
 
Kwani unaamini Nini kutoka chadema labda tuanze hapo. Na je Kuna kitu unaweza kukiamini kikisemwa na chasema au huamini chochote?
Inategemea ni kitu gani!

Siwezi kusema siamini Chochote tokea CHADEMA.
 
Sasa hapo tatizo ni upinzani au ni utawala mbovu ulioshika dola na kuua upinzani kwa nguvu ya dola
Upinzani umeuliwa na mfumo wa uongozi wa serikali kuu hili nalikubali lakini pia hata njaa za sisi wapinzani zimechangia kudumaza harakati za wapinzani wa kweli. Mifano ndo hiyo akina halima mdee na wenzake. Akina silinde akina Lijualikali akina Selasini hao wote walikuwa ni wapinzani kwanini nishindwe kusema upinzani umejaa wachumia tumbo hata kama mimi pia ni mpinzani ila sioni aibu kuyatamka hayo
 
Ungeandika kiswahili tu maana sijaelewa
Tatizo sio katiba mpya clean your house first opposition you need to do some house cleaning of your house but as a CCM member I know you don't want to clean your house
 
Upinzani umeuliwa na mfumo wa uongozi wa serikali kuu hili nalikubali lakini pia hata njaa za sisi wapinzani zimechangia kudumaza harakati za wapinzani wa kweli. Mifano ndo hiyo akina halima mdee na wenzake. Akina silinde akina Lijualikali akina Selasini hao wote walikuwa ni wapinzani kwanini nishindwe kusema upinzani umejaa wachumia tumbo hata kama mimi pia ni mpinzani ila sioni aibu kuyatamka hayo

..ukisema upinzani umejaa wachumia tumbo unakuwa unawaonea.

..kuna wapinzani wengi tu ambao hawajafanya upuuzi walioufanya wakina Lijualikali, Silinde, na Mdee.

..kwa upande wa Selasini yeye amehamia Nccr, hajasaliti na kwenda CCM, hivyo humuita mchumia tumbo nadhani siyo haki.
 
Back
Top Bottom