..Utaratibu ni kwamba wabunge wanateuliwa na vikao vya chama.
..hata kama "wabunge" hao walipewa "baraka" na Mwenyekiti, na wakaandikiwa barua na Katibu Mkuu, bado ubunge wao sio halali kwasababu hakuna kikao cha Chadema kilichopitisha maamuzi ya kuwateua.
..Na kwa bahati nzuri, au mbaya, wengi wa waliokwenda bungeni ni wajumbe wa vikao vyenye mamlaka ya kufanya uteuzi wa wabunge. Kwa msingi huo wengi wanaelewa kwamba kilichotokea ni kinyume na taratibu na sheria.
..Kuna wakati Spika Ndugai alikataa kupokea barua toka kwa Katibu Mkuu wa Chadema kwa madai kwamba haikutokana na maamuzi ya vikao vinavyotambulika vya chama hicho. Sasa imekuwaje safari hii Spika anakiuka utaratibu aliojijengea awali?
..Katika suala hili Tume ya Uchaguzi na Spika wa Bunge walipaswa kuzingatia maamuzi ya vikao vinavyotambulika vya chama ktk uteuzi wa wabunge wa viti maalum wa Chadema.
..Ni bahati mbaya sana Tume ya Uchaguzi na Spika wameziba masikio hata pale walipoelekezwa na Chadema kwamba chama hakikuhusika ktk kuteua wabunge wa viti maalum.
NB:
..Halima na wenzake wangemhitaji Mbowe kama wangekuwa wanapitisha mambo yao ktk vikao vya chama. Hiki kilichotokea hakikuhitaji "baraka" za Mbowe, sana sana kilihitaji collusion kati ya Halima na kundi lake, Tume ya Uchaguzi, na Spika wa Bunge.