Kuna shida gani Tanzania ikitangaza rasmi kuisaidia Congo kupambana na M23? Tuna Viongozi wa namna gani?

Umaskini wetu ni upi mkuu? Au una maanisha umaskini wa akili au umasikini wa viogozi wenye huruma na mali za uma?
Umaskini ni neno pana kwa family level Kuna county level....

Umaskini kwa country level ndio nao uzungumzia Kama hatuwezi kutoa huduma buree za afya , huduma ya maji safi na salama Bado iinatusumbua, Kuna wanafunzi wanakaa Chini sababu ya uhaba wa madawati bila kusahau upungufu wa walimu na vitabu.
Bado kwenye hii nchi Kuna raia wengi hawana uwezo wa ku meet basic needs ambazo ni food, shelter & clothes

Alaf jamaa anashaur twende vitani tuka isaidie Kongo na kuanzisha military base hapo mashariki ya Kongo uoni kua ni recklessness kuenda vita vya jirani wakati wewe mwenyewe hujiwezi...kikubwa twende kusaidia Kongo Kama jumuiya sio Kama Tanzania as Tanzania.

Mfano vita vya somalia Tanzania haikupeleka jeshi somalia Ila wakenya walipeleka na walikipata pata kutoka al shababu
 
Sisi hatujiwezi kivipi?

Siamini kama hatujiwezi. Tumekosa tu viongozi wenye akili na wanaojua kuset vizuri priorities
 
Nikijibu kuwa umasikini wetu ni akili zetu wenyewe nitakosea?kivipi?

imagine mnanunua v8 ufisadi kila kona tena wa mabilioni halafu bado unaamini kuna umaskini? hayo mabilioni yanayoliwa na kunua v8 hayatoshi kunua dawa? huwa unafuatilia kwani ripot ya CAG?
 
Baada ya Vita vya Kagera tukawa hoi bin taaban kiuchumi !
Mwalimu akatuambia tujifunge mikanda kwa miezi 18 hali itarudi kama kawaida !
Akaja Sokoine akatuambia huenda Mwalimu alikosea kidogo kutamka, tunatakiwa kujifunga mkanda kwa miaka 18 😳🙄 !

Vita isikie kwa wenzio !
Sisi bado Masikini tunatakiwa kwanza tueneze nishati safi na salama mpaka vijijini ili watu waache kukata miti kwa ajili ya kupata mkaa wa kupikia !

Vita hapana labda tukivamiwa !
 
mbona Rwanda inafaidika na hiyo vita alafu sisi mnatuambia huwezi kwakua ni masikini? 2013 tuliipiga m23 kwa utajiri upi tuliokawa nao?. tatizo Letu ni waoga sana
 
Huyu kichwa ngumu hatakuelewa mwambie aende akipage yeye na familia yake
 
Tulikuwa hoi kwa sera mfu za Nyerere sio sababu ya vita
 
mbona Rwanda inafaidika na hiyo vita alafu sisi mnatuambia huwezi kwakua ni masikini? 2013 tuliipiga m23 kwa utajiri upi tuliokawa nao?. tatizo Letu ni waoga sana
FIB(FORCE BRIGADE INTERVENTION)-UN
 
Ukitangaza vita na March 23 umetangaza vita Rwanda,kumbuka Rwanda ni mshilika mwenzetu wa EAC na kibiashara katika Bandari ya Dar es salaam.
Ukikurupuka kuiendea hiyo vita itatughalimu kiuchumi.
 
NCHI HII KUNA MIJIZI CCM
 
Ukitangaza vita na March 23 umetangaza vita Rwanda,kumbuka Rwanda ni mshilika mwenzetu wa EAC na kibiashara katika Bandari ya Dar es salaam.
Ukikurupuka kuiendea hiyo vita itatughalimu kiuchumi.
Kati ya Rwanda na Congo nani mshirika wetu mkubwa zaidi wa kibiashara?

Kwani Congo hayupo EAC?


Tena tukiangalia kihivyo tunapata sababu zaidi za kuingia vitani
 
Hapo kwenye report ya CAG unajua kua ukinunua kitu mfano computer,madawa, mifuko ya cement,fridge, gari, kulipa vibarua bila kua na evidence/ Receipt....
CAG akija at report kua Kuna embezzlement kumbe pesa ilitumika Kama ulivyo elekezwa Ila hakukuwa na evidences/ receipt

Ndipo Ile zana inapo pata nguvu kua MALI YA SERIKALI INALIWA KWA RISITI 😊😊☺️☺️☺️
 

Kukomboa Ardhi yetu.
hyo sio sababu ya Mwalim kutangaza vita.sababu zilizofanya Mwalim nyerere kutangaza vita ni uhasama wa kibinafsi kati ya Mwalim Nyerere na Iddi Amin,,Mwalimu alikuwa akiamini sana kwenye sera ya ujamaa tofauti na Iddi Amini ambaye yeye alikuwa akiamini mfumo wake binafsi ambao ulijikita kwenye udikteta..Sababu nyingine ni uvunjifu wa mikataba ya Amani kati ya Tanzania na uganda iliyopo pelekea uhusiano mzuri ulio kuwepo mwanzo kuzorota baada ya tu ya idd amin kuchukua nchi mwaka 1971 kwa mapinduzi ya kijeshi na kumtoa Milton obite,Mwalim alikataa kutambua utawala wa idd Amin ndio maana alitoa hifadhi kwa Milton obite na wapinzani wa Iddi Amini..Swala la kagera ilikuwa ni sababu ndogo sana..na ile vita ili tugharimu sana Tanzania japo tulimnyuka Idd Amin ila haikuwa na tija
 
Kati ya Rwanda na Congo nani mshirika wetu mkubwa zaidi wa kibiashara?

Kwani Congo hayupo EAC?


Tena tukiangalia kihivyo tunapata sababu zaidi za kuingia vitani
Hao M23 kama Hamasi tu utapiiiiga wanarudi Rwanda wana chili pale kidogo wanalianzisha tena .
Utawala wa Kikwete tulienda tukawatimua,Ngongoti anammaindi Jk walivyo jipata wamerudi tena.
Watatufilisi wapuuzi hao
 
Ukisema Tz nchi masikini maana yake hakuna reasource zozote ambazo kivyovyote vile haziwezi kutukwamua na kututoa kwenye umaskini. Imagine nchi yako hii ina madini kila kona,ges mbuga za wanyama na mistu nk halafu pamoja na elimu hizi tulizo nazo tunakubali na kupokea maneno ya wanasiasa ambao wanaimba Tz nchi masikini ili wapige kw mgongo huo miaka 4 tu nyuma jpm alisema nchi hii sio maskini na kweli tuliona sasa hii akili ya kusema sisi ni masikini inatoka wapi mkuu?

Nchi kama libya ilikuwa na mafuta tu lakini Tazama neema waliyokuwa nayo watu wake hayo yote waliyapata kwa sababu ya kuwa na kiongozi makini mwnye uchungu na raia na nchi yake kwa ujumla
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…