Kuna shida gani Tanzania ikitangaza rasmi kuisaidia Congo kupambana na M23? Tuna Viongozi wa namna gani?

Kama
hatujui au hatuwezi kuzisimamia Rasilmali zetu ndio umasikini wenyewe wa kujitakia !
Wengine walikubali Nchi kupewa asilimia 3 kwenye Dhahabu !
Mwamba alisemaga tumepigwa 😳🙄 !
 
Kwanini sasa Drc wasitumie vizuri hizo pesa walizonazo kulijenga vizuri jeshi lake Ili liweze kuilinda nchi yao ?
DRC ni kubwa kweli kweli hata barabara tu sehemu kubwa ya Nchi hakuna kabisa !
Sehemu kubwa kwenye madini ndio Vita hazina ukomo !
Mpaka Mbilikimo wana majeshi yao 😅🤣 !
 
Suluhu ya kijeshi kwenye huo mzozo haiwezi kuwa ya kudumu.
 
..
Suluhu ya kijeshi kwenye huo mzozo haiwezi kuwa ya kudumu.

..suluhisho la kijeshi linaweza kupatikana ikiwa viongozi wa nchi za Kiafrika watakuwa imara, wakweli, na wazalendo.

..mgogoro wa DRC una hila na usaliti mkubwa wa viongozi wa Afrika kwa muda mrefu sasa.
 
..anachosema mtoa mada ni kwamba Tanzania haipaswi kuwa VUGUVUGU katika masuala ya kisiasa, na kiusalama, ktk nchi zinazotuzunguka. Tuamue kuwa upande wa M23, au upande wa serikali, bila kificho wala kuona haya.

Kwahiyo tukiacha kuwa vuguvugu TZ itapata faida gani kiuchumi toka Congo maana kunufaika kiuchumi ndo main point ya OP.
 
Wewe unafikiri kwa nini Membe alikufa kifo cha kutatanisha vile,Membe ndo alikuwa anasimama bila kificho kabisa kumpinga Kagame
 
Kwahiyo tukiacha kuwa vuguvugu TZ itapata faida gani kiuchumi toka Congo maana kunufaika kiuchumi ndo main point ya OP.

..tukiacha kuwa vuguvugu vita ya DRC itamalizika na tutaweza kushirikiana nao kiuchumi, na kijamii, kuendeleza nchi zetu.
 
Congo haina pesa za kuwalipa wenye uwezo wa kuwasaidia.
Tatizo kubwa la kongo haikuwekeza kwenye kuimarisha ulinzi na kuimarisha majeshi ndio maana inapigwa na kuzidiwa nguvu na kanchi kama Rwanda
 
Ingekuwa ni nafasi nzuri kwenda kutumia silaa pamoja na kuzifanyia majaribio.
 
..tukiacha kuwa vuguvugu vita ya DRC itamalizika na tutaweza kushirikiana nao kiuchumi, na kijamii, kuendeleza nchi zetu.

Kwani sasa hatushirikiani?

Changamoto za kufanya biashara Congo iliyopo vitani na Zambia, Malawi au Uganda zenye amani ni zile zile.

Itakua hujamuelewa OP.
 
Mambo ya nchi hayaendi kimihemuko, mkuu, kuna mambo mzito ya kupima kwanza pande zote , haya mambo tuwaachie wenye dhamana yao JWTZ
 
Wanyarwanda ni waovu, mashetani wasio faa. Congo sio kwao ila wameamua kuwa vibaraka wa wazungu kwa kumwaga damu za wakongo wasio na hatia ili kupora madini ya Zaire na kuwauzia wazungu. Watanzania 43 wamezungukwa karibu na airport ya Goma na hawajui wataponaje. Wakikutwa si ajabu wakauwa wote. Wamesikika wakiomba msaada wa serikali ya Tanzania kwa clip waliyoirusha. Hao ni pamoja na madereva wa malori makubwa, wafanya biashara nk.
 
Hatuwez kuwapeleka wanajeshi wetu wakafe kisa ujinga
 
..mbona Rwanda na Uganda wanasaidia waasi lakini hawafi njaa?
hawa wanaleta visingizio tu, nchi kichaa kama congo eti nayo tunashindwa kujifunzia kunyoa. wakati Rwanda nchi ya juzi inaweza vizuri kabisa sisi tunaweza nini sijui?.

kiufupi siyo kwamba sisi watu wa amani sana la hasha sisi ni mbumbumbu, tumezubaa sana.
 
Unajmjua mtu mwenye Uwezo wa kutoa Hiyo Amri...!?
 
Inasadikika Tanzania ndiyo nchi ilitoa msaada wa hali na mali kuhakikisha nchi zote za kusini mwa Africa zinapata uhuru, je ni faida gani tz ilipata mpaka leo, na nchi hizo kwa sasa zinatupita kiuchumi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…