Kuna shida gani Tanzania ikitangaza rasmi kuisaidia Congo kupambana na M23? Tuna Viongozi wa namna gani?

Leo tunajenga reli ya SGR kwa dhumuni ifike Mashariki mwa Congo. Swali ni Je hiyo reli itakuwa na faida kama Mashariki mwa Congo kukiendelea kuwa vitani namna hii?

Tuache suala la reli. Hivi Je Viongozi wetu hawajui tunaweza faidika kiuchumi endapo leo hii tukiwasaidia wazi Congo kwenye vita yao dhidi ya M23?

Marekani, Uingereza na Ujerumani wanatoa msaada mkubwa kwa Ukraine kupambana na Urusi. Msaada ule sio msaada kama msaada ni mkopo ambao Ukraine watazilipa nchi zile kwa miaka mingi ijayo!

Tuseme Viongozi wetu hawa hawaoni kuwa tunaweza kutoa msaada wa kijeshi kwa Congo sisi kama Tanzania ( Sio chini ya mwamvuli wa SADC au AU au EAC) na tukautumia kama mkopo kwa nchi ya Congo ambapo baadae watatulipa hata kwa karne nzima na tukafaidika kiuchumi?

Hivi nchi hii kuna Think Tanks? Ni kina nani hao Think Tanks? Wana Mchango gani positively kwa maendeleo ya Taifa?
Nisaidie kujua faida ya
1. Kujitangaza nje ya mwamvuli wa UN
2. faida ya kuisaidia congo ndani au nje ya mwanvuli wa UN
3. Hasara ya kutoisaidia congo
 
Faida ni sisi kuingia makubaliano moja kwa moja na Taifa la Congo kwa terms tunazoziona zina manufaa kwetu.

Hasara ni sisi kuikosa hiyo fursa ambayo endapo tukiitumia inaweza kuwa mwanzo wa Sera mpya za kiuchumi zitakazotufaidisha mara Mia kulilo huku kutegemea misaada!
 
456486196_10234405729831667_7368265567281035086_n.jpg

Waziri wa ulinzi wa Tanzania akiwapimia M23 kwa mbaaaalii!!!
Wabongo mnafikiri vita ni kama mechi za mpira kati ya Bonyokwa FC na Kinesi...

Hapo unacheza na maisha ya watu Bob. Kweny vita hakunaga adui mdogo, ukienda kichwa kichwa unapasuka tuu vizur.

Lazima ujiulize hapo kuna ya nchi ngapi lkn yote mambo ni magumu sana. Hapo mkenya yupi, msauz yupo, AMISOM IPO. Mbongo mwenyew alishawahigi kwenda hapo watu wamerudishwa sanduku.
 
Mbona mwaka 2012 tuliingia Congo na kuwatoa M23?

Au umezaliwa mwaka 2015?
 
Hatuwezi kufanya hvyo, kwanza ungechimba ujue chanzo cha hayo machafuko, ujiulize hao M23 wanatoa wapi nguvu walionayo?, Ujiulize kwann hao mabepari wamenyamaza miaka yote wakat huaga ndo wakwanza kusemaga wanatuma jeshi kwenda kutuliza ghasia?, Ujiulize kwanini Alshabab wa Somalia wanaitwa Magaidi halafu M23 wanaitwa Waasi?, Ilihali wote wanashika silaha na wanaua wasio na hatia?, Unadhani hawaoni?
Wanaona vizur sn kuliko hata wewe na wao wanajijua kuwa ndio wafaidikaji wa kwanza kutoka kwa hao M23 na vikosi vyote vinavyoondoa amani Kongo kuliko hata hao Rwanda. Rwanda anatumika tuu kama chambo ila nyuma ya pazia naye anatumwa,
Hao wakubwa ndio wanaotoa silaha na mahitaji yote kwa vikundi hvyo. Tunaambiwa kuna madini ambayo yanatumika ktk masuala ya teknolojia (vioo vya computer, simu n.k) ambayo yapo kongo na sio kwengine popote. Jiulize wanatutengenezea vifaa hvyo na kuja kutuuzia huku ni akina nani?,
Wanahakikisha Serikali ya Kongo haisimami imara kamwe maana ikiwa na machafuko hvyo wao wanachukua madini buure kabisa, ila Serikali ikipewa nguvu inaamisha Vikosi vyote vitaondoshwa Kongo na Kongo inajijenga na ili wayapate madini hayo itawabidi waje kama wawekezaji na wafuate sheria na matakwa ya Serikali ikiwemo Kodi n.k, so wanaona ni bora kuwe na machafuko ili wayachukue bure. Sasa Tanzania aseme anaenda kusaidia kongo maana yake anakwenda kupigana na wale wanaompa mikopo na misaada kila siku, kwanza ataambiwa rudisha kwato nyumbani na ukae utulie, akikaza fuvu watamnyoosha taratibu tuu, (VIKWAZO)!?.
Naomba kuwasilisha.
 
Mkuu

Baelezee/ Tueleze

Baambie/ Tuambie
Kwanza ujue vile vikosi vya ulinzi wa aman haviendi Bora viende ,kisa Jirani ana vita ,Kuna sheria na utaratibu

Ili waande km walivyoenda mwaka 2012 inabidi baraza la Usalama likae na itoe idhini na Hy idhini Iwe ktk zile chapter walizokubaliana .
 
Hatuwezi kufanya hvyo, kwanza ungechimba ujue chanzo cha hayo machafuko, ujiulize hao M23 wanatoa wapi nguvu walionayo?, Ujiulize kwann hao mabepari wamenyamaza miaka yote wakat huaga ndo wakwanza kusemaga wanatuma jeshi kwenda kutuliza ghasia?, Ujiulize kwanini Alshabab wa Somalia wanaitwa Magaidi halafu M23 wanaitwa Waasi?, Ilihali wote wanashika silaha na wanaua wasio na hatia?, Unadhani hawaoni?
Wanaona vizur sn kuliko hata wewe na wao wanajijua kuwa ndio wafaidikaji wa kwanza kutoka kwa hao M23 na vikosi vyote vinavyoondoa amani Kongo kuliko hata hao Rwanda. Rwanda anatumika tuu kama chambo ila nyuma ya pazia naye anatumwa,
Hao wakubwa ndio wanaotoa silaha na mahitaji yote kwa vikundi hvyo. Tunaambiwa kuna madini ambayo yanatumika ktk masuala ya teknolojia (vioo vya computer, simu n.k) ambayo yapo kongo na sio kwengine popote. Jiulize wanatutengenezea vifaa hvyo na kuja kutuuzia huku ni akina nani?,
Wanahakikisha Serikali ya Kongo haisimami imara kamwe maana ikiwa na machafuko hvyo wao wanachukua madini buure kabisa, ila Serikali ikipewa nguvu inaamisha Vikosi vyote vitaondoshwa Kongo na Kongo inajijenga na ili wayapate madini hayo itawabidi waje kama wawekezaji na wafuate sheria na matakwa ya Serikali ikiwemo Kodi n.k, so wanaona ni bora kuwe na machafuko ili wayachukue bure. Sasa Tanzania aseme anaenda kusaidia kongo maana yake anakwenda kupigana na wale wanaompa mikopo na misaada kila siku, kwanza ataambiwa rudisha kwato nyumbani na ukae utulie, akikaza fuvu watamnyoosha taratibu tuu, (VIKWAZO)!?.
Naomba kuwasilisha.
Wengi wanachukulia easy tu...Kwa nje unaona ni vita ya waasi M23 na DRC ila ndani ni haya usemayo
 
Leo tunajenga reli ya SGR kwa dhumuni ifike Mashariki mwa Congo. Swali ni Je hiyo reli itakuwa na faida kama Mashariki mwa Congo kukiendelea kuwa vitani namna hii?

Tuache suala la reli. Hivi Je Viongozi wetu hawajui tunaweza faidika kiuchumi endapo leo hii tukiwasaidia wazi Congo kwenye vita yao dhidi ya M23?

Marekani, Uingereza na Ujerumani wanatoa msaada mkubwa kwa Ukraine kupambana na Urusi. Msaada ule sio msaada kama msaada ni mkopo ambao Ukraine watazilipa nchi zile kwa miaka mingi ijayo!

Tuseme Viongozi wetu hawa hawaoni kuwa tunaweza kutoa msaada wa kijeshi kwa Congo sisi kama Tanzania ( Sio chini ya mwamvuli wa SADC au AU au EAC) na tukautumia kama mkopo kwa nchi ya Congo ambapo baadae watatulipa hata kwa karne nzima na tukafaidika kiuchumi?

Hivi nchi hii kuna Think Tanks? Ni kina nani hao Think Tanks? Wana Mchango gani positively kwa maendeleo ya Taifa?
tulikuwa tunamhitaji mtu kama kikwete, ili alete heshima kwenye mazingira. hadi tumepoteza heshima kama polisi wa eneo hili la africa.
 
Nadhani JK angekuwa Rais hadi leo by today tungekuwa na Military Base Goma na Kivu na angechukua huu ushauri haraka sana
 
tulikuwa tunamhitaji mtu kama kikwete, ili alete heshima kwenye mazingira. hadi tumepoteza heshima kama polisi wa eneo hili la africa.
JK yupo na ana ushawishi mkubwa tu serikalini kama raisi mstaafu pekee aliyebaki.
 
Kuwa na ushawishi ni tofauti na kuwa mfanya maamuzi. JK is a soldier na kipindi kile alikuwa anafanya maamuzi kama mwanajeshi mbobevu na kiongozi kweli.

Alisahau tu kuingia mkataba wenye maslahi kwa Tanzania na DRC. Saivi tungekuwa na Military Base kule na wanatulipa mafweza kibao.
 
Mbona tulimsaidia mwaka 2012 na hatukupigwa?
Huo ujinga hatufanyi tena, hatuwezi kurisk askari wetu kwa watu wasiolielewa. Tatizo la kongo jeshi lao halina umoja wanasalitiana, wanauza taarifa kwa adui sasa hapo si unatafuta kifo cha kijinga.
 
Kwanza saivi napendekeza tukatoe msaada au tuingie pale kwa maslahi ya kiuchumi?

Jaribu kutofautisha. We unadhani Urusi anavyoenda Bukrina Faso na Niger anaenda kutoa msaada? Au alivyo na vikosi vyake Syria au Libya unadhani kule anatoa msaada?
 
Back
Top Bottom