Kuna siku utakutana na Mungu ukiwa peke yako

1995_No_Ku_Fake

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2026
Posts
1,561
Reaction score
3,328
Wakuu, kuna jambo nimekuwa nikilitafakari sana.

Katika maisha haya tunahangaika kutafuta pesa, heshima, mali, nafasi na kutambulika. Tunajenga nyumba, tunanunua magari, tunatafuta followers na tunataka watu wajue tumefanikiwa.

Lakini kuna siku kila mmoja wetu ataondoka hapa duniani akiwa hana chochote alichokusanya.

Utakutana na Mungu ukiwa peke yako.

Hakutakuwa na marafiki wa kukusifia, pesa za kukusaidia, cheo cha kukulinda wala mali za kukufuata.

Kilichobaki ni matendo yako.

Ulimsaidia nani ulipokuwa na uwezo?
Ulimsamehe nani?
Ulimuumiza nani bila sababu?
Ulimnyanyasa nani kwa sababu ulikuwa na uwezo?
Na pale ulipokuwa huna kitu, uliwezaje kubaki na moyo wa kumtegemea Mungu?

Nadhani wakati mwingine tunahitaji kupunguza mbio za dunia na kujitazama ndani.

Maisha ni mafupi sana. Leo tunazungumza, kesho mtu anaulizia ulikuwa wapi.

Tafuteni dunia, lakini msimsahau Mungu. Tafuteni mafanikio, lakini msipoteze utu. Na mkipewa uwezo, tumieni kuwainua wengine.

Mwisho wa safari, tunarudi pale tulikotoka.

Mungu atupe mwisho mwema, moyo safi na maisha yenye maana. Ameen.
 
SAWA MKUU!
 
Fedha,Magari na Majumba ni vitu vya kupita tu,
Ila hakikisha kua vinapitia na kwako kabla mauti hayajakukuta,
Hatukuumbwa ili tuteseke wala kuteseka sio sifa,

Masikini hua wanafarijika sana wakikumbuka kua hata tajiri nae atakufa,

Au nasema uongo ndugu wananchi?
 
Kila mtu ana uhuru wa kuamini anachoona kina maana kwake. Mimi naamini Mungu yupo, na wewe una haki ya kutokuamini. Cha muhimu tuheshimiane katika tofauti zetu za imani.
Wala hukatazwi kuwa na imani yako kwa huyo Mungu.

Kwa sababu kuamini, unaweza kuamini hata uongo.

Imani ni jambo la binafsi la faragha.

Lakini ukileta imani yako hapa Jamii forums. Unakuwa umeiweka imani yako public.

Tunaweza kuichambua na kuikosoa.

Ndio maana mtu akiamini Mungu yupo kimya kimya huko alipo, well and good.

Lakini ukileta imani ya huyo Mungu hapa JF ambayo ni public forum, lazima tuikosoe.

Kwa sababu hapa sio kanisani au msikitini.

Hapa tunataka ukweli wenye uthibitisho.

Na sio imani za kusadikika tu.
 
Hata illusions na hallucinations vipo kwenye akili ya mtu.

Ndio maana mtu akisema Mungu yupo, lazima athibitishe.

Ili tuthibitishe yupo kweli.

Na sio illusions zake tu.
Nimesema hivyo nikiwa na maana Mungu yupo kwenye akili ya mtu

Kwa maana unaweza kumtengeneza
Kwenye akili yako na ukaamini yupo

Au usimtengeneze ukaamini na asiwepo kabisa inshort ni wewe tu

For me nipo 50/50
Kama yupo sawa ✔️
Kama hayupo fresh ✔️
 
Kuamini, mtu anaweza kuamini hata uongo.

Na akili ya mtu inaweza kutengeneza uongo na ika uamini uongo huo.

Kuamini tu, hakufanyi kitu kiwepo kweli.

Hatuhitaji kuamini kwa imani.

Tunahitaji kujua kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho.

Ukweli sio jambo la imani.

Ukweli ni jambo la uhakiki na uthibitisho.
 
Hapana mkuu..
Utasemaje maisha ni ubatili ikiwa unaamini maisha haya yaliwekwa na Mungu mkamilifu unayeamini yupo?

Huoni contradiction hapa?

Kama unasema maisha ni ubatili, basi hata huyo Mungu, unayeamini yeye ni muumbaji wa maisha haya, na yeye pia anakuwa batili.

Kwa sababu maisha hayawezi kuwa ubatili kama yaliumbwa na Mungu mkamilifu.

Kama maisha ni ubatili, it means hata huyo Mungu muumbaji wa maisha anakuwa batili.

Mungu mkamilifu hawezi kuumba maisha ambayo ni ubatili.

Unless otherwise, Mungu huyo hayupo na maisha ni ubatili.

Kwa sababu Mungu mkamilifu hayupo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…