Kuna siku utakutana na Mungu ukiwa peke yako

Isaya 55:7,8
MUNGU ni mkamilifu mkuu!
 
Mungu yupo?
 
Ni kweli kabisa mkuu
Mimi nawaachia mjadala maana mimi siamini hayo mambo ya Mungu
 
Amen... Noted! Be blessed. Mkuu kwa kutukumbusha hilo!!! Maisha ni UBATILI mtupu!
Amina mkuu 🙏🏽 Ni kweli kabisa. Maisha ni mafupi na mali, cheo na umaarufu ni vya kupita. Cha muhimu ni kumcha Mungu, kutenda mema na kuacha alama njema kabla ya safari kuisha. Barikiwa sana mkuu.
 
Mungu yupo kwenye akili ya mtu 😅
😅 Inawezekana ukawa mtazamo wako mkuu, lakini kwangu uwepo wa Mungu hauishii kwenye akili ya mwanadamu. Kila mmoja ana uhuru wa kuamini au kutokuamini. Muhimu tuheshimiane.
 
😂 Husemi uongo ndugu yangu. Kifo hakibagui tajiri wala maskini. Ila somo kubwa ni hili: tafuta mafanikio ukiwa hai, yafurahie kwa kiasi, saidia wengine, na usisubiri kifo cha tajiri ndipo ujifariji. Maisha ni safari, kila mmoja ana nafasi ya kupambana na kuboresha hali yake.
 
Kila mtu ana uhuru wa kuamini anachoona kina maana kwake. Mimi naamini Mungu yupo, na wewe una haki ya kutokuamini. Cha muhimu tuheshimiane katika tofauti zetu za imani.
Nasubiria atakuja kukujibu Kwa hoja gani Kwasababu wewe umrmjibu vizuri sana.
 
Nakubaliana na uhuru wa kukosoa, lakini tusichanganye kutokuwa na ushahidi wa kisayansi na kusema jambo ni uongo. Imani na sayansi vina maeneo tofauti. JF ni sehemu ya mjadala; hoja ikiletwa hadharani ikosolewe kwa hoja na heshima, bila kumdhalilisha mwenye imani.
 
Ubatili aliuleta mwanadamu kupitia dhambi mkuu
Mungu mkamilifu, kwa nini aumbe binadamu wasio wakamilifu ambao waliweza kuleta dhambi na ubatili?

Mungu mkamilifu, Alishindwaje kuumba binadamu wema na wakamilifu tu, ambao watakuwa wakamilifu siku zote na wakati wote?
 
Hata illusions na hallucinations vipo kwenye akili ya mtu.

Ndio maana mtu akisema Mungu yupo, lazima athibitishe.

Ili tuthibitishe yupo kweli.

Na sio illusions zake tu.
Ni kweli kwamba hisia au uzoefu wa mtu pekee hauwezi kuwa ushahidi wa kutosha kuthibitisha uwepo wa Mungu. Lakini kwa upande mwingine, kutokuwepo kwa ushahidi unaokuridhisha wewe hakumaanishi moja kwa moja kwamba Mungu hayupo. Hoja ya msingi ni kutofautisha kati ya imani, madai na ushahidi—kila upande una haki ya kuuliza ushahidi na kuhoji hoja za upande mwingine.
 
ok.🐒
 
Mungu mkamilifu, kwa nini aumbe binadamu wasio wakamilifu ambao waliweza kuleta dhambi na ubatili?

Mungu mkamilifu, Alishindwaje kuumba binadamu wema na wakamilifu tu, ambao watakuwa wakamilifu siku zote na wakati wote?
MUNGU alimuumba mwanadamu mkamilifu aliye huru na maamuzi ya kufikiri... na hakuumba roboti la kumtii tu kwa shurti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…