Kuna siku utakutana na Mungu ukiwa peke yako

Hoja ya problem of evil ni nzito, lakini si uthibitisho wa kimantiki kwamba Mungu hayupo. Inaonyesha changamoto ya kueleza kwa nini Mungu mwenye uwezo na wema aruhusu uovu. Lakini kusema “uovu upo, hivyo Mungu hawezi kuwepo” kunahitaji kwanza kuthibitisha kwamba Mungu angekuwa hana sababu yoyote ya kuruhusu uovu.

Hapo ndipo mjadala wa kweli ulipo—si kwamba lazima uchague Mungu au mantiki.
 
wameongeza mkanganyiko usio na maana
Si mkanganyiko usio na maana; ni swali zito linalotaka kuunganisha imani, mantiki na tatizo la uovu.

Changamoto ni jinsi unavyolitafsiri, si kuwepo kwa swali lenyewe.
 
Hivi mama etu atakuwa na urithi kidogo kwenye yale majimali ya zimbabwe?
 
Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hana sababu ya kuruhusu uovu.

Hakuna hoja ya kimantiki inayoeleweka ya Mungu huyo kuruhusu uovu.

Kama ipo, iweke hapa tuijadili.
 
Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hana sababu ya kuruhusu uovu.

Hakuna hoja ya kimantiki inayoeleweka ya Mungu huyo kuruhusu uovu.

Kama ipo, iweke hapa tuijadili.
Hoja yako ina nguvu kama msingi wake ni kwamba “Mungu mwenye uwezo wote na upendo wote hawezi kuwa na sababu yoyote ya kuruhusu uovu.” Lakini hapo ndipo mjadala ulipo: kutokujua sababu ya Mungu kuruhusu uovu si sawa na kuthibitisha kwamba hakuna sababu.

Kama unaonyesha kimantiki kwamba uwepo wa uovu unapingana moja kwa moja na uwepo wa Mungu huyo, niletee hoja hiyo tuijadili.
 
Hata hivi vitu ulivyoelezea hapa huenda visiwepo kwa sbabu hakuna na hakitokuwapo na mru atakayeenda na kurudi kwa ajili ya mrejesho baada ya kwenda huko.

Ishi jinsi unavyoweza,ukitaka gari,nyumba nzuri,followers n.k ni wewe na maamuzi yako ISIPOKUWA ishi kama wanavyoishi wengine na chagua kama walivyochagua wengine.

Ok ukitaka kuwa shekhe,mchungaji,pornstar,mafia na yeyote utakaye NI WEWE pia.
 
Uhuru wa kuchagua ni wako, lakini kila uchaguzi una matokeo yake. Kutokuwepo kwa mrejesho wa mtu aliyekufa hakuthibitishi kwamba hakuna maisha baada ya kifo.

Hapo ndipo imani, ushahidi na falsafa zinapotofautiana.
 
Uhuru wa kuchagua ni wako, lakini kila uchaguzi una matokeo yake. Kutokuwepo kwa mrejesho wa mtu aliyekufa hakuthibitishi kwamba hakuna maisha baada ya kifo.

Hapo ndipo imani, ushahidi na falsafa zinapotofautiana.
Kwahiyo unataka kusema wote imani yetu ni kama yako mkuu🤔?
 
Sisi tulikubali lini au uliambiwa na maandiko kuwa adam ndo alikula tunda
Yaani shetani alitaka nafasi yake akamtupia duniani alafu unasema tulitaka
Asante... kabla sijakujibu ngoja nikuulize kwanza ilinijue nakujibu upande upi...

Binadamu ametokana na nini unavyofahamu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…