#COVID19 Kuna siku Watanzania watapanga foleni za kilomita kadhaa ili kuchanja

Labda chanjo ya UKIMWI ila sio hii ya mafua
 
Tushazisikia sana hii gonjera, nenda kawaimbie watoto. Ni ushauri tu. Otherwise you are just wasting your time.
 
Utungaji huu, wengi wameanzisha uzushi kama huu. Mtaani kwetu hivi, kule vile. Umesikia chanjo inaweza sababisha kuganda damu unaamua kutunga "mtaani kwetu."
Ila mtu akisema mtaani kwao kila siku watu wanakufa na corona unaamini.
 
Sema kwa muda mrefu ilionekana hakuna umuhimu sana kwa watoto kuchanja sababu walionekana hawako kwenye risk. Sijui kama imebadilika. Na wanachanjaje watoto bila consent ya mzazi?
Chanjo ya jj ambayo inakua administered TZ ni kwa 18+
 
Kwa hiyo vifo vya 3% kwa aiborne disease unaona si kitu. Pengine labda sijui lengo lako. Wewe unapinga chanjo sababu ugonjwa umekuzwa?
Issue ya ugonjwa kukuzwa hilo ni jambo moja na kuhusu hizi chanjo za majaribio ni suala lengine pia. Wewe hujui hofu iliyotengenezwa kwenye corona imechangia kuleta athari kwa kiasi gani.
 
Yap, wengi wazushi. Hawajui hata kwanini hawataki kuchanja. Wanaamua kuunda hadithi.
Tatizo mi wewe ambae unachagua katika hizo hadithi ni zipi uzisikilize kwa sababu ndio unachotaka kusikia na zipi hutaki kusikiliza kwa sababu si unachotaka kusikia, leo akija mtu akisema tu mtaani kwao kila siku wanazika watu kwa corona basi hutomuona mzushi wala hutomuhoji kajuaje kuwa hivyo vifo vyote ni vya corona.
 
Wapinga chanjo hawataki kukubali ushahidi wa wazi kuwa chanjo inasaidia. Wanatunga stori mbadala kuonyesha kuwa chanjo inaua.
 
Haiwezi kutokea kwa sababu si kila anayeambukizwa anakufa au kuugua
 
Variants ni nyingi. Ikitokea variants ambayo haisikii hii chanjo ya J&J ntaenda tena kuchanja. Na ntaendelea kujikinga na Corona sababu kuna variants zingine na chanjo siyo 100%
Sawa, utaendelea kuchanja tena na tena na tena na tena na tena hadi utakapokufa au sio?

Na vipi kuhusu kama utakapoachanja, utaacha kuvaa barakoa, utaweza kujichanganya, hautagua, hautaambukizwa, hautaambukiza wengine na hutakufa kwa Corona?

Na je kuhusu side effects zake za muda mfupi, muda wa kati na za muda mrefu, ni zipi?
 
Team samia huyu hawezi kukujibu atapita kama hajaona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…