Teleskopu
JF-Expert Member
- May 5, 2017
- 702
- 767
Israeli wamechanja kuliko ncho yoyote duniani. Lakini ndio wanapigwa na korona kuliko nchi zingine. Hivi sasa wanaongelea kuchoma booster ya nne.Kwa hali ninavyoiona ya hii Korona kuondoka na watu, kuna siku watanzania watapanga foleni za kilomita kadhaa ili wapate chanjo.
Nilienda kupata chanjo siku ya jumanne. Nilikuwa niko peke yangu na mtoa chanjo. Tulizungumza mambo kirefu sana. Nilikaa pale kama nusu saa hivi. Mbaya zaidi wafanyakazi wa afya wengi sana nao wanakwepa kuchanja. Jamaa fulani alinipa uchambuzi kuwa wafanyakazi wengi wa afya kinachowafanya wasichanje ni uoga wa sindano!!
Kingine nilichokiona, unapewa cheti cha mkononi na kingine unaweza download. Inaonekana kama umedhamiria kutochanja ila unataka upate cheti, unaweza 'ukachonga' na mtoa chanjo ukapata cheti.
Mbaya zaidi serikali nayo imechukulia mzaha hili suala. Gwajima, Dr anaenda kumpa Steve Nyerere ubalozi wa chanjo. Ataelimisha nini watu juu ya chanjo?
Siku inakuja watu watapanga foleni za kilomita kadhaa ili kupata chanjo
SWALI ni kuwa, je, kinachowasumbua ni korona kweli au ni hizo chanjo?
Hiki ndicho kitakachotokea kwetu. Kadiri wanaochanjwa wanavyoongezeka, na wagonjwa nao watakuja kuongezeka. Halafu tutaambiwa kovidi imeongezeka. Kwa sababu ya hofu, wasiojua kinachoendelea ni kweli watapanga foleni. Hapo ndipo tutakuwa tayari tumeingia kwenye mtego uliosetiwa, ambao hivi sasa unatenda kazi israeli, uingereza nk.