Kuna siri gani kati ya Wachaga na Mwisho wa Mwaka?

Kuna siri gani kati ya Wachaga na Mwisho wa Mwaka?

Hoa ndio wachaga wakienda huko mbali na kula skukuu pia hufunzwa jinsi ya kujibagua mbele ya jamii nyengine wasiokuwa wachagga.
 
Wengi wanakomaa kuwa wachagga tunaenda kufanya matambiko ili wafanikiwe kibiashara....well nijuavyo ni kuwa hakuna binadamu anayependa umaskini wa kipato au makazi duni...so kinachozuia makabila mengine msiende kutambika kwenu ni nini?
 
Je ni matambiko ndo yakafanya Kilimanjaro nchi nzima iongoze kwa kuwa na shule nyingi za msingi na sekondari na hata vyuo vikuu hadi vijijini zaidi ya mkoa mwingine wowote? Hayo matambiko pia yakaifanya KLM isikosekane kwenye topten ya matokeo ya kidato cha nnne na cha sita kila mwaka tangu Uhuru?? Huko kutambika kukafanya pia KLM kuwe na infrastructure nzuri I'm terms of roads na mengineyo?? Ajabu sana....basi matambiko yao ni ya kuigwa kama ni hivyo.
 
Wachaga wengi wanaishi nje ya mkoa wao kutokana na uhaba wa ardhi. Pia ni wachapakazi sana hasa katika kutafuta hela.
Siku za nyuma wengi wa wanaume wa kichaga waliwaacha wake zao migombani na wa kutafuta pesa mbali.
Wachaga wengi ni wakristo na pia hupenda mila zao.
Wengine wamejenga nyumba zao kule nzuri tu.
Mambo haya yanachangia sana kuwasukuma kwenda walau mara moja kwa mwaka nao December wakati wa krismasi
 
Ni kipindi muafaka kukutana na ndugu na jamaa kufurahi pamoja. Pia ni kipindi cha kutambulishana. Kuna watoto wengi wamezaliwa sehemu tofauti na hawawajui ndugu wengine so muda mwafaka kuwatambulisha kwa ndugu ili wafahamiane wasije oana. Pia mazingira ya uchagani ni mazuri sana kwa mapunziko. Yanavutia sana. ukianzia na mlima KLM, migomba, kahawa, miti miti, nyumba nzuri zilizopambwa na maua na fance za maua, ukoka au nyasi zilizo katwa vizuri kuelekea nyumba za watu, barabara nzuri, mbege, lafuzi nzuri ya wachaga nk

Inapotokea ndugu wa kichaga wameoana na hata kuzaa mtoto, hii uwa inasuluhishwa vipi kwa mila ya huko?
 
Jamani mnisaidie hili swali, mbona hawa wenzetu wanapenda sana kusafiri kwa mkupuo kipindi hiki cha mwisho wa mwaka hasa Krisimasi,mtueleze huko moshi kuna kitu gani cha tofauti na mikoa mingine?
Mnasababisha hadi nauli zinapanda bila sababu yoyote ile.

cc miss chagga

Babu hio kitu ni worldwide sio wachaga tu,kumbuka wengi wao sio wazawa wa dar sasa kuna tatizo gan watu wakijipangia wakti maalumu kurudi nyumbani.Wachina nao hurudi vijijini kwao kipindi cha chinese new year tena mwaka jana miji mikubwa yote yachina haikuwa na watu wote wamerudi bush kula sikukuu
 
Last edited by a moderator:
Wewe wadanganye wasiojua uchagani, hakuna kabila linaongoza kwa ushirikina kama wachaga. Huku mgombani mmewafanya ndug zenu matahira vyakutosha.
 
Wachaga kwa matambiko na ibada za mizimu ndio wenyewe. Hiki ni kipindi cha kupeleka vitovu vya watoto waliozaliwa nje ya kwao, ndio kipindi cha kutoa makafala kwa mali walizochuma, ndio kipindi cha kutambika, ndio kipindi cha kupata baraka toka kwa wazazi na mengine mengi yaliyojificha. MAMBO HAYA SIO KWA WACHAGA WOTE kuna wanaofata mkumbo tuuu.
 
Kikuyu na mchaga tabia zinafanana bila shaka, nao wanatabia ya kurudi makwao msimu huu, tabia za kusaka manoti wanafanana pia
 
mbna sisi hatuwashangai nyie wazaramo mlivyokalia mdundiko tuu hamna maendeleo yoyote wachaga wamevamia mji wenu nyie mkakimbilia huko matako.ni mwa dunia
 
Jamani mnisaidie hili swali, mbona hawa wenzetu wanapenda sana kusafiri kwa mkupuo kipindi hiki cha mwisho wa mwaka hasa Krisimasi,mtueleze huko moshi kuna kitu gani cha tofauti na mikoa mingine?
Mnasababisha hadi nauli zinapanda bila sababu yoyote ile.

cc miss chagga
sisi tunapenda kushirikiana wakati wa sikukuuu tunakaa pamoja tunakula pamoja.. na ni jambo linalotijengea ushrikiano kwa ndugu kukaa pamoja..... [na pia inafanya tunapata changamoto pale unapoona mwenzio kaja na land cruser we unakipasso lazima mwakani uweke mikakati ya kumfikia mwenzio} kamfano tu hako
 
Kikuyu na mchaga tabia zinafanana bila shaka, nao wanatabia ya kurudi makwao msimu huu, tabia za kusaka manoti wanafanana pia

Haha!Tabia ya kusaka manoti tena?Si hiyo ni tabia ya kila mtu?Kweli wakikuyu tunafanana na wachagga kabisa lakini mnayosema kuhusu tambiko kwa wenzenu,wakikuyu tambiko zinafanywa hadharani eneo za mlima Kenya.Tambiko hizi si kwa mizimu bali ni kwa mungu wetu Mwenee-nyaga,makao yake Mlima Kenya.Wazee wakikiyu wanapatana chini ya mti mtakatifu mugumo(fig tree) na kutoa kafara kwa kumchinja kondoo pamoja na pombe yetu ya kienyeji muratina ilotengenezwa kwa asali
kama kafara kwa Mweene-nyaga.Mti huu mtakatifu wa mogumo ukikuyuni haukatwi kamwe wala kutumiwa kamba mbao ukianguka uguse ardi inakuwa ni shiida na tambiko lazima zifanywe na kafara ya kondoo kutolewa na wazee huku wanaume wote wakishurutishwa kutofanya ngono kwa wiki hiyo nzima ya tambiko.Wanawake hawakubaliwi kukaribia mti huu mtakatifu wa mugumo.Tamaduni zetu hizo.Sijui za wachagga zikoje.
 
Wachagga wamebarikiwa na ndiyo sababu wanatajwa katika ukoo mmoja katika Biblia. Soma Hesabu 3: 20
 
Wachagga wamebarikiwa na ndiyo sababu wanatajwa katika ukoo mmoja katika Biblia. Soma Hesabu 3: 20

Duh!Jombaa,wakikuyu pia hivo hivo,ata mambo ya kuabudu mungu aliye na makao mlima Kenya kama tu wayahudi wakati wa Musa alipokuwa anapanda mlimani kuongea na Mungu.Pia kuna jambo wanahistoria wamelifatilia kwa sana ile mtoto anapozaliwa Ukikuyu utasikia wamama wakipiga ngemi za kumkaribisha mtoto kwa nguvu,aaaririririririri,mara tatu kwa mtoto msichana,mara nnne kwa mtoto wa kiume.Imefananishwa na aylee,aylee,aylee wanavyosema wayahudi kwenye sinagogi yaani asifiwe asifiwe asifiwe(yahweh).
 
Sasa mkuu inabidi uje Rombo siku moja tuongee....una mengi ya kufanana na sisi so kuna haja ya kukutana na Ku share experience.....Karibu Rombo maana si kila kitu cha kuweka hapa...
 
Sasa mkuu inabidi uje Rombo siku moja tuongee....una mengi ya kufanana na sisi so kuna haja ya kukutana na Ku share experience.....Karibu Rombo maana si kila kitu cha kuweka hapa...

Shukra kwa mwaliko jombaa siyuko mbali na Rombo niko kazi karibu na mpaka kati ya Namanga na Tarakea maeneo ya Kajiado.Inaniuma sana sitaweza kuwa na wenzangu kwa bibi kule eneo za mlima Kenya kunaitwa mukurwe-ine hii krismasi,ndugu na dada zangu wote na 'cousin' zangu wanaelekea huko tarehe 24 wanarudi tarehe mbili Nairobi,mimi hadi tarehe mbili niko kazini.Mwaliko wako ntafatilia shugli zikipungua lakini.Shukran.
 
Back
Top Bottom