Kuna siri gani kwa watu kufunga biashara zao siku ya Jumanne?

Kuna siri gani kwa watu kufunga biashara zao siku ya Jumanne?

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Salaam Wakuu,

Ifikapo Jumanne kwa Dar es salaam imekuwa ni siku ya shida kupata huduma mbalimbali katika maeneo ya biashara.

Maeneo kama Saloon, Baa na maduka ya bidhaa mbalimbali yanafungwa katika siku hii.

Je, kuna siri au sababu yoyote kwa jambo hili? Anayefahamu naomba kuelimishwa.
 
Aiseee imenikuta mm leo hyo, sikuwah kunotice before, yan maduka kibao yamefungwa hadi mama muuza vitafunwa nikajiuliza au ndo mambo ya valz day jamn.
 
Kila lile ambalo halipendi Binadamu hapa duniani, basi liliwekwa siku ya Jumanne.
 
Sijui kama kwenye biashara Kuna hilo Jambo, ila nakumbuka enzi hizo nipo shule,siku ya juma nne ilikuwa siku mbaya kwangu. Ila pengine labda ilikuwa ni imani tu ya kijinga.

Unashangaa ghafla mwalimu amekuja kukagua homework na mimi sijafanya,unaweza kukaa siku nzima usipige kelele ila ikatokea muda umegeuka nyuma tu unaongea na mtu,monitor mnagongana macho na monitor Kisha unaona anaandika jina lako katika list ya wapiga kelele. Na hiyo siku mwalimu atataka tu majina ya wapiga kelele ili awazibue. Wanasema jumanne mganga hapigi ramli.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Kwa mara ya kwanza nilimsikia Donald Trump kabla hajawa Rais kwenye Kipindi cha The Apprenticeship, kuwa Jumanne uwa ni siku slow sana kwenye biashara zake.
 
Kuna mahali kulikuwa na saluni ya kike, kila jnne huwa hafungui ofisi, ila sasa yule dada ni shangingi flani hivi na anapenda kuagua,, yawezekana na hao wapo kundi moja na huyu
 
Watu na imani zao

Au ni karismatic wameenda kwenye maombi
 
Kwa Leo labda sababu ni Valentino day
Ila kwa siku nyingine inasemekana jumanne hua ni siku ngumu Sana kirizki
 
Usikute ndiyo siku maalum ambapo mashetani, mapepo na majini ya kina namna hutoka mashimoni na mapangoni na chini ya bahari ili kwenda kupunga upepo na kubadili mvao kwa ajili ya assignment mpya ya baba mkuu wa uasi na uongo.
 
Ni sayansi tu kwamba watu wengi humaliza nguvu walizokusanya weekend kwa siku ya Jumatatu na hivyo momentum hupungua sana siku ya Jumanne.
Kwamba nguvu hukusanywa wikendi? Tueleze kwa kina kidogo, mkuu. Kuuliza si ujinga.
 
HAKUNAGA WATEJA SO WENGI HUTUMIA KAMA SIKU YA KUPUMZIKA
 
Back
Top Bottom