Metamorphosis
JF-Expert Member
- May 27, 2020
- 206
- 358
Majini yanawasiliana.Wasalaam,.
Natumai mnaendelea salama wote, kuna taarifa inaenea sana kuwa mwezi umronekana jana maeneo ya Tandahimba na masheikh wa Bakwata, wakawapigia simu Bakwata makao makuu lakini wakazipuuza hizo taarifa na kuwatangazia raia kuwa mwezi haukuandama siku ya jana hivyo leo watu waendelee kufunga.
Hili limekaaje wakuu...?
View attachment 2208429
Biñafsi naamini nachokifahamu na kukitekeleza... nawaheshimu viongozi pia.
Ndio mtihani wa viongozi wetu wa dini tulionao, kikubwa ni kuwaombea tu Allah awasamehe makosa yao na awape hikma na uwezo wa kusimamia haki.
mkuu rudia kunisoma vizuri utanielewa vizuri mtazamo wangu.Ina maana hata kiongozi akikuelekeza jambo ambalo unaona wazi kuwa sio sahihi unatakiwa kumfuata kwa kuwa ni kiongozi...?
Tuwaachie wataalamu wa BAKWATA.
Mkuu sisi wazee wa vipedo(kama ulivyoita) tumeanza kufunga mwanzo na wala hakuna aliyesema k2amba tunafungw mwanzo kwa sababu sisi ni walafi.Mnataka ku justify ulafi wenu qa kufungua siku 29 ninyi wazee wa vipedo?
Mkuu sisi wazee wa vipedo(kama ulivyoita) tumeanza kufunga mwanzo na wala hakuna aliyesema k2amba tunafungw mwanzo kwa sababu sisi ni walafi.
Kwa hiyo na siku zikitimia tukaanza kufungua msitubeze teenaa wakati tulianza mwanzo kuliko ninyi.
Nao wana sababu zao za kuwa na utaratibu wakutangaza kuhusu kuandama kwa mwezi. Kama BAKWATA ni chombo kilicho na mamlaka (mandate) kamili ya kusimamia mambo yanayohusu Uislamu kwa Tanzania, mimi ni nani kuwapinga ?.Utaalamu gani walionao hao Bakwata mkuu...?
Mimi najaribu kuwaza kwamba huenda ikawa zamani walikuwa wanaangalia mwezi kwasababu za ukosefu wa technolojia, na urahisi wa mawasiliano, ila kwa sasa kama mawasiliano yapo na umeonekana mahali it is the matter of communication tu.
Ila ndio hivyo haya ni mambo ya Imani sio ngumu sana kueleweka;
Nao wana sababu zao za kuwa na utaratibu wakutangaza kuhusu kuandama kwa mwezi. Kama BAKWATA ni chombo kilicho na mamlaka (mandate) kamili ya kusimamia mambo yanayohusu Uislamu kwa Tanzania, mimi ni nani kuwapinga ?.
By the way utaalamu wa BAKWATA unaonekana wanapotoa maoni yao, unaweza kukubaliana na watu wa Mtwara au kusubiri siku pekee ambayo BAKWATA wataitangaza. 😇😇
Una uhalali kukubaliana nao au kuwapinga.Kuwa na mandate ni jambo moja ila kusimamia ipasavyo hiyo mandate ni jambo jingine tofauti kiongozi, mifano mingi tu tunayo kwa mfano polisi wana mamlaka ya kusimamia usalama wa raia na mali zao, lakini kiuhalisia ipo hivyo mkuu...?
Haya Mambo sijui yaliharibikia wapi..?
Kitambo ukionekana mahali popote Tanzania, unasikia hata mida ya saa nne usiku enzi hizo Radio Tanzania taarifa inatangazwa, na kulikuwa hakuna tatizo..
Sasa leo na Teknolojià hii bado hili suala la Mwezi kuonekana linaleta changamoto .
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Muamini Yesu Kristo
Upate ondoleo la dhambi ukawe na uzima wa milele
Wasalaam,
Natumai mnaendelea salama wote, kuna taarifa inaenea sana kuwa mwezi umronekana jana maeneo ya Tandahimba na masheikh wa Bakwata, wakawapigia simu Bakwata makao makuu lakini wakazipuuza hizo taarifa na kuwatangazia raia kuwa mwezi haukuandama siku ya jana hivyo leo watu waendelee kufunga.
Hili limekaaje wakuu?
View attachment 2208429