Kuna taarifa kuwa mwezi umeonekana Tandahimba jana tarehe 01/05/2022

Wasalaam,.

Natumai mnaendelea salama wote, kuna taarifa inaenea sana kuwa mwezi umronekana jana maeneo ya Tandahimba na masheikh wa Bakwata, wakawapigia simu Bakwata makao makuu lakini wakazipuuza hizo taarifa na kuwatangazia raia kuwa mwezi haukuandama siku ya jana hivyo leo watu waendelee kufunga.

Hili limekaaje wakuu...?

View attachment 2208429
Majini yanawasiliana.
 
Biñafsi naamini nachokifahamu na kukitekeleza... nawaheshimu viongozi pia.

Ina maana hata kiongozi akikuelekeza jambo ambalo unaona wazi kuwa sio sahihi unatakiwa kumfuata kwa kuwa ni kiongozi...?
 
Ndio mtihani wa viongozi wetu wa dini tulionao, kikubwa ni kuwaombea tu Allah awasamehe makosa yao na awape hikma na uwezo wa kusimamia haki.

Amin ila mambo mengine hufanyika kwa makusudi kabisa kwa jambo ambalo lipo wazi kabisa mkuu.
 
Hata uandame mikoa yote, usipoonekana Dar hautambuliki
 
Umeonekana pia Kigoma mwisho wa reli. Eid mubarak kwa Muslims wote 🕌🌙
Screenshot_20220502-123706~2.png
 
Ina maana hata kiongozi akikuelekeza jambo ambalo unaona wazi kuwa sio sahihi unatakiwa kumfuata kwa kuwa ni kiongozi...?
mkuu rudia kunisoma vizuri utanielewa vizuri mtazamo wangu.

nawaheshimu kama viongozi wenye mamlaka but naamini katika kile nachokifahamu na Kwa miongozo nayoifahamu.

Eid Mubarak .....!
 
Mnataka ku justify ulafi wenu qa kufungua siku 29 ninyi wazee wa vipedo?
Mkuu sisi wazee wa vipedo(kama ulivyoita) tumeanza kufunga mwanzo na wala hakuna aliyesema k2amba tunafungw mwanzo kwa sababu sisi ni walafi.

Kwa hiyo na siku zikitimia tukaanza kufungua msitubeze teenaa wakati tulianza mwanzo kuliko ninyi.
 
Mimi najaribu kuwaza kwamba huenda ikawa zamani walikuwa wanaangalia mwezi kwasababu za ukosefu wa technolojia, na urahisi wa mawasiliano, ila kwa sasa kama mawasiliano yapo na umeonekana mahali it is the matter of communication tu.

Ila ndio hivyo haya ni mambo ya Imani sio ngumu sana kueleweka;
 
Hana akili huyo jamaa anaongea vitu kiushabiki tu mkuu...!
 
Utaalamu gani walionao hao Bakwata mkuu...?
Nao wana sababu zao za kuwa na utaratibu wakutangaza kuhusu kuandama kwa mwezi. Kama BAKWATA ni chombo kilicho na mamlaka (mandate) kamili ya kusimamia mambo yanayohusu Uislamu kwa Tanzania, mimi ni nani kuwapinga ?.

By the way utaalamu wa BAKWATA unaonekana wanapotoa maoni yao, unaweza kukubaliana na watu wa Mtwara au kusubiri siku pekee ambayo BAKWATA wataitangaza. 😇😇
 
Haya Mambo sijui yaliharibikia wapi..?
Kitambo ukionekana mahali popote Tanzania, unasikia hata mida ya saa nne usiku enzi hizo Radio Tanzania taarifa inatangazwa, na kulikuwa hakuna tatizo..
Sasa leo na Teknolojià hii bado hili suala la Mwezi kuonekana linaleta changamoto .
 
Mimi najaribu kuwaza kwamba huenda ikawa zamani walikuwa wanaangalia mwezi kwasababu za ukosefu wa technolojia, na urahisi wa mawasiliano, ila kwa sasa kama mawasiliano yapo na umeonekana mahali it is the matter of communication tu.

Ila ndio hivyo haya ni mambo ya Imani sio ngumu sana kueleweka;

Hapana kiongozi ni suala la kukubaliana tu na kuweka ushabiki pembeni, sasa kwa hapo Tandahimba kweli na watu wameuona na wamewapigia simu Makao Makuu Bakwata kabla ya saa 4 usiku eti Makao Makuu wanakwambia wameshafunga muda wa kutangaza mwezi, kweli mkuu...?
 
Nao wana sababu zao za kuwa na utaratibu wakutangaza kuhusu kuandama kwa mwezi. Kama BAKWATA ni chombo kilicho na mamlaka (mandate) kamili ya kusimamia mambo yanayohusu Uislamu kwa Tanzania, mimi ni nani kuwapinga ?.

By the way utaalamu wa BAKWATA unaonekana wanapotoa maoni yao, unaweza kukubaliana na watu wa Mtwara au kusubiri siku pekee ambayo BAKWATA wataitangaza. 😇😇

Kuwa na mandate ni jambo moja ila kusimamia ipasavyo hiyo mandate ni jambo jingine tofauti kiongozi, mifano mingi tu tunayo kwa mfano polisi wana mamlaka ya kusimamia usalama wa raia na mali zao, lakini kiuhalisia ipo hivyo mkuu...?
 
Una uhalali kukubaliana nao au kuwapinga.
 
Haya Mambo sijui yaliharibikia wapi..?
Kitambo ukionekana mahali popote Tanzania, unasikia hata mida ya saa nne usiku enzi hizo Radio Tanzania taarifa inatangazwa, na kulikuwa hakuna tatizo..
Sasa leo na Teknolojià hii bado hili suala la Mwezi kuonekana linaleta changamoto .

Watu wamelifanya hili jambo kuwa la kiushabiki zaidi kuliko kiimani mkuu. Hakuna nchi ambayo tumepishana siku nzima (masaa 24), lakini cha kushangaza ni kwamba watu wanapisha siku nzima katika kufunga au kufungua, ni jambo la kushangaza sana mkuu.
 
Wasalaam,

Natumai mnaendelea salama wote, kuna taarifa inaenea sana kuwa mwezi umronekana jana maeneo ya Tandahimba na masheikh wa Bakwata, wakawapigia simu Bakwata makao makuu lakini wakazipuuza hizo taarifa na kuwatangazia raia kuwa mwezi haukuandama siku ya jana hivyo leo watu waendelee kufunga.

Hili limekaaje wakuu?

View attachment 2208429

Si kweli, nimeongea na waliopo huko nao wanashangaa hizo taarifa!!
 
Back
Top Bottom