Kuna tatizo gani Barabara ya mwendokasi ya mbagala?

Ungekuwa dereva aliyepitia mafunzo halali ungejua kuwa barabara hiyo bado haijakamilika.
Ili barabara ikamilike inatakiwa iwe na alama zote za kuwaongoza madereva na watembea kwa mguu vitu hivyo bado havijakamilika, vikikamilika itatumika kwani wameanza kuweka taa za kuongoza madereva na watembea kwa mguu.
 
Mwekezaji ameagiza magari hayajafika mkurugenzi wa magari ya kasiiiii sasa barabara ilipokaribia kuisha ilifaa na magari yaagizwe ili ikiisha yawe yamefika Africa yetu
 
Acha kutetea nonsense.
Ni barabara ngapi hapa mjini zina traffic lights, lakini tunakuta askari ndo wanaongoza magari? nini kigumu kwa askari kwenda kuongoza magari kwenye njia hii mpya?
Mnahitaji miaka mingapi ili muweke hizo Taa na alama za barabarani?
 
Sasa pita ile ya kuanzia hapo JKT mgulani hadi Keko. Hapo Keko imechakaa kabisa inabidi warekebishe sana kabla ya kukabidhi.
 
Sasa pita ile ya kuanzia hapo JKT mgulani hadi Keko. Hapo Keko imechakaa kabisa inabidi warekebishe sana kabla ya kukabidhi.
Utashangaa hiyo inakabidhiwa hivyo hovyo... na mheshimiwa ataalikwa kuifungua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…