Kuna tatizo gani Barabara ya mwendokasi ya mbagala?

Kuna tatizo gani Barabara ya mwendokasi ya mbagala?

Kwa ninavyofaham, barabara ya mwendokasi ya kuelekea mbagala ilishakamilika kwa 100% kwa zaidi ya mwaka sasa, lakini mpaka sasa haijaanza kutoa huduma. Badala yake, sasa imekua ndo barabara kuu ya bodaboda.

Inasikitisha na kutia hasira, kuona kitu ambacho kingetoa msaada kwa maelfu ya wananchi wa manaohangaika na usafiri, kimekaa 'idle'. Waliopewa dhamana ya kusimamia wapo wapi? nini tatizo? Hii nchi mbona inachukulia poa wananchi kiasi hiki?

Kinachozidi kushangaza, wakati project hii haijaanza 'kunfunction', project nyingine za Gongo lamboto na Tegeta nazo zimeshaanza. Huu upuuzi bogus leadership utakoma lini?
Ungekuwa dereva aliyepitia mafunzo halali ungejua kuwa barabara hiyo bado haijakamilika.
Ili barabara ikamilike inatakiwa iwe na alama zote za kuwaongoza madereva na watembea kwa mguu vitu hivyo bado havijakamilika, vikikamilika itatumika kwani wameanza kuweka taa za kuongoza madereva na watembea kwa mguu.
 
Mwekezaji ameagiza magari hayajafika mkurugenzi wa magari ya kasiiiii sasa barabara ilipokaribia kuisha ilifaa na magari yaagizwe ili ikiisha yawe yamefika Africa yetu
 
Ungekuwa dereva aliyepitia mafunzo halali ungejua kuwa barabara hiyo bado haijakamilika.
Ili barabara ikamilike inatakiwa iwe na alama zote za kuwaongoza madereva na watembea kwa mguu vitu hivyo bado havijakamilika, vikikamilika itatumika kwani wameanza kuweka taa za kuongoza madereva na watembea kwa mguu.
Acha kutetea nonsense.
Ni barabara ngapi hapa mjini zina traffic lights, lakini tunakuta askari ndo wanaongoza magari? nini kigumu kwa askari kwenda kuongoza magari kwenye njia hii mpya?
Mnahitaji miaka mingapi ili muweke hizo Taa na alama za barabarani?
 
Back
Top Bottom