Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mtoto mdogo huyo.Cheka tu ila vita vya kiroho ni real wewe huwezi kujua
Mkuu kwani huyo alikwambia hafanyi kazi au ana shida? Hebu tujaribu kuheshimu maarifa usiyoyajua haswa kama huna ujuzi nayo.Hayaa sasa yale yalee..mkuu ebu toka kwenye hayo mawazo bas. Ebu jikitr kufanya kaz kwa bidii na umuombe MUNGU utafanikiwa.
Ikiwa kama kweli hii nchi inalaana mbona MUNGU yupo na ndo anaweza kutuondolea hizo laana.
Kama kweli laanza ipo, mbona kila kukicha viongoz wa dini zote wanakusanyika na kuliombea taifa. Na wengine wanaitisha maombi hadi ya kufunga kwa ajili ya kuondosha laana katika nchi. Mbona kila mwaka tunafunga mwez wa ramadhani kumuomba Mwenyezi Mungu atuondolee kila makosa na laana.
Kama tunafanya maombi iweje bas uendelee kuamni kuwa nchi ina laana? Kama laana iliingia nchini kwa makafara na maombi ya wachawii, bas laana imeshatoka pia kwa maombi na sadaka za wanaomcha MUNGU. Ebu tuachane na mawazo hayo..laana ni yako mtu binafs unapoacha kufanya kaz kisha unalaumu wengine kwa kufeli kwako hiyo ndo laana sasa.
Tanzania hamna cha kafara wala nn-Changamoto ya Tanzania ni katiba-Ambayo Nyerere aliipenda kwa sababu ilikuwa inampa madaraka makubwa na ambayo baadaye alikuja kuikosoa kwa sababu aliijua ni mbaya kwa sababu alihofia viongozi wengine wangeitumia kama yeye au zaidi.Makafara Nyerere aliyoyafanya Bagamoyo wala siyo sababu ya Tanganyika kupata uhuru mapema kutoka kwa wakoloni kama baadhi ya watu wanavyosema-Kiufupi ni kwamba baada ya WWII-Marekani na mataifa mengine kupitia forum mbalimbali za kimataifa walianza kupinga sana ukoloni-Hvyo waingereza na mataifa mengine kutokana na mbinyo waliachia makoloni yao mengi sana duniani.Kingine kilichopelekea Tanganyika kupata uhuru mapema ni kwamba hatukuwa na rasilimali nyingi kiivyo walizohitaji wakoloni pamoja na mambo mengineyo;Therefore Nyerere hata asingefanya makafara bagamoyo uhuru lazima tungepewa-sababu upepo wa dunia ulikuwa umeshabadilika.Hakuna taifa lolote duniani lililosimama imara bila nguvu za mkuu wa anga! Kuanzia matambiko mpaka makafara na vyama vya kishetani.
Hivi vyote vimejenga madhabahu zao kwenye kila ardhi ya kila taifa. Wananchi wake wana dini na imani zao lakini mataifa yamesimikwa kwenye hizi madhabahu viapo na makafara.
Tanzania ni taifa kama mataifa mengine duniani, nayo ina makafara na madhabahu zake za kuifanya nchi itawalike iheshimike na iwe na 'stability' kwenye kila nyanja kuanzia kiuchumi, kijamii, kimaono mpaka kiulinzi nk
Kuna makafara ya kuilinda Tanzania yanatajwatajwa sana. Kafara la Bagamoyo na kafara la Lindi! Kafara la Bagamoyo linaelezewa kwa ufasaha na wahusika wake wanajulikana. Shida ipo kwenye usiri mkubwa unaotawala kwenye kafara la Lindi
Hili limebaki kuwa fumbo na tetesi isiyothibitishwa popote. Wanaolijua ni wachache na hulisimulia kwa tahadhari kubwa sana! Lina nini ndani yake hili?
Kafara la Bagamoyo ni la moto na kiongozi wake ni Mzee mchawi marehemu Forojo Ganze na hiki ndicho alikisema kabla ya kukata roho
"Baba, sisi tunataka kuwasha Mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini mahala pasipo na tumaini, faraja palipo na huzuni, tumaini pasipo na tumaini, upendo penye chuki na heshima palipo na dharau"
Baada ya kutamka hayo mbele ya Mwl. Nyerere, Ganze alikata roho na ndipo ukaanzishwa Mwenge wa Uhuru. Kinachonishangaza hapa ni kile kipengele kisemacho"UMULIKE HATA NJE YA MIPAKA YETU". Ina maana ndani ya nchi tubaki gizani kama tulivyo sasa?
Hli kafara la Bagamoyo tunaweza kuliita kafara la mambo ya nje na lile la Lindi tunaweza kuliita la mambo ya ndani. Sasa hapa ndio penye shida ni kafara la mambo ya ndani na limebaki ndani na kuwa siri kubwa
Mwalimu Nyerere Mchonga meno kwa hakika anayajua vema makafara yote mawili na miiko yake na pengine ndio maana katika tawala zote tangu uhuru ni utawala wake pekee ndio ukifanikiwa kwa kiwango cha juu kwenye
Kuweka misingi sahihi ya uongozi, uwajibikaji na uzalendo
Kuweka misingi sahihi kijamii, kisiasa na kiulinzi
Kuweka misingi sahihi ya kimtazamo na kimaono
Mipango endelevu na dira sahihi tangu tulipoanzia, tulipofikia na tunakoenda
Baada ya hapo waliofuatia wote kila mtu alikuja na MAGAZIJUTO YAKE na sarakasi zake
Baada ya hapo kila aliyeingia alianza vizuri lakini hakuchelewa kuharibu. Kama si kipindi cha kwanza basi cha pili cha uongozi wake
Baada ya hapo waliofuatia wote waliingia kwa upole na unyenyekevu lakini mara wakageuka wajivuni, wababe, na baadhi yao dharau kujikweza na kujimwambafai kwingi...bila kusahau vitisho na ugiligili mwingine mwingi
Baada ya hapo wengine wote watakanguliza maslahi binafsi, ya ndugu zao, jamaa zao na watu wote waliokuwa na maslahi nao
Mambo yanazidi kuharibika na pengine hawaoni wametiwa upofu.. Huu ugiligili sasa ni mpaka kwa viongozi wanaowateua kuwasaidia majukumu ya kiutendaji. Sasa hivi kiongozi akipewa kipaza sauti aongee mbele ya makamera asipotoa boko basi atatoa kituko cha karne ama kuongea yasiyowezekana
Matamko ni mengi mno
Maelekezo ni mengi mno
Makatazo ni mengi mno
Maonyo ni mengi mno
Yani haya ni mengi mno mpaka yanapishana barabarani na kupigana vibega
Kuna tatizo kubwa la kiuongozi na hili lina mizizi mirefu tangu ang'atuke mwalimu. Je, kwa mtazamo wa kiroho ni lile kafara la Lindi?
Wakati utaongea. Hebu tuupe muda!
Nyerere kilichomwondoa pia ni mbinyo wa mataifa makubwa duniani kutaka nchi ifanye mabadiliko mojawapo ni kupitia SAP.Kwangu mm naweza kusema ni heri Meko kuliko Nyerere katika maswala ya udiktekta na utawala mbovu.Nyerere hajawah kuwa kabisa kiongozi wa mfano kwangu,na ninachoamin kilichomfanya watu hawamjui vyema ni kutokana na kwamba kwenye utawala wake hakukuwa na mitandao ya kijamii-hii ndo ilikuwa salama yake.Nyerere aliwaficha watz Siri nyingi Sana kupitia media control,thus aliwafanya watz maiti Ili awatawale.
Baada ya upepo wa mabadiliko ya fikra kulinda heshima aliona bora aachie.
Sasa viongozi wa ccm wanaongoza kizazi cha sasa kwa fikra za miaka ya 70,thus awatofaulu.
Mkuu kalonji tumegeeni hiyo hadithi nasiye tufaidikeNaam mkoani lindi
Kumbe mkuu kiranga aliishi ikuluni!!
Hahaaaaa kakaa sana Ikulu huyo jamaaKumbe mkuu kiranga aliishi ikuluni!!
"UMULIKE HATA NJE YA MIPAKA YETU". Ina maana ndani ya nchi tubaki gizani kama tulivyo sasa?Hakuna taifa lolote duniani lililosimama imara bila nguvu za mkuu wa anga! Kuanzia matambiko mpaka makafara na vyama vya kishetani.
Hivi vyote vimejenga madhabahu zao kwenye kila ardhi ya kila taifa. Wananchi wake wana dini na imani zao lakini mataifa yamesimikwa kwenye hizi madhabahu viapo na makafara.
Tanzania ni taifa kama mataifa mengine duniani, nayo ina makafara na madhabahu zake za kuifanya nchi itawalike iheshimike na iwe na 'stability' kwenye kila nyanja kuanzia kiuchumi, kijamii, kimaono mpaka kiulinzi nk
Kuna makafara ya kuilinda Tanzania yanatajwatajwa sana. Kafara la Bagamoyo na kafara la Lindi! Kafara la Bagamoyo linaelezewa kwa ufasaha na wahusika wake wanajulikana. Shida ipo kwenye usiri mkubwa unaotawala kwenye kafara la Lindi
Hili limebaki kuwa fumbo na tetesi isiyothibitishwa popote. Wanaolijua ni wachache na hulisimulia kwa tahadhari kubwa sana! Lina nini ndani yake hili?
Kafara la Bagamoyo ni la moto na kiongozi wake ni Mzee mchawi marehemu Forojo Ganze na hiki ndicho alikisema kabla ya kukata roho
"Baba, sisi tunataka kuwasha Mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini mahala pasipo na tumaini, faraja palipo na huzuni, tumaini pasipo na tumaini, upendo penye chuki na heshima palipo na dharau"
Baada ya kutamka hayo mbele ya Mwl. Nyerere, Ganze alikata roho na ndipo ukaanzishwa Mwenge wa Uhuru. Kinachonishangaza hapa ni kile kipengele kisemacho"UMULIKE HATA NJE YA MIPAKA YETU". Ina maana ndani ya nchi tubaki gizani kama tulivyo sasa?
Hli kafara la Bagamoyo tunaweza kuliita kafara la mambo ya nje na lile la Lindi tunaweza kuliita la mambo ya ndani. Sasa hapa ndio penye shida ni kafara la mambo ya ndani na limebaki ndani na kuwa siri kubwa
Mwalimu Nyerere Mchonga meno kwa hakika anayajua vema makafara yote mawili na miiko yake na pengine ndio maana katika tawala zote tangu uhuru ni utawala wake pekee ndio ukifanikiwa kwa kiwango cha juu kwenye
Kuweka misingi sahihi ya uongozi, uwajibikaji na uzalendo
Kuweka misingi sahihi kijamii, kisiasa na kiulinzi
Kuweka misingi sahihi ya kimtazamo na kimaono
Mipango endelevu na dira sahihi tangu tulipoanzia, tulipofikia na tunakoenda
Baada ya hapo waliofuatia wote kila mtu alikuja na MAGAZIJUTO YAKE na sarakasi zake
Baada ya hapo kila aliyeingia alianza vizuri lakini hakuchelewa kuharibu. Kama si kipindi cha kwanza basi cha pili cha uongozi wake
Baada ya hapo waliofuatia wote waliingia kwa upole na unyenyekevu lakini mara wakageuka wajivuni, wababe, na baadhi yao dharau kujikweza na kujimwambafai kwingi...bila kusahau vitisho na ugiligili mwingine mwingi
Baada ya hapo wengine wote watakanguliza maslahi binafsi, ya ndugu zao, jamaa zao na watu wote waliokuwa na maslahi nao
Mambo yanazidi kuharibika na pengine hawaoni wametiwa upofu.. Huu ugiligili sasa ni mpaka kwa viongozi wanaowateua kuwasaidia majukumu ya kiutendaji. Sasa hivi kiongozi akipewa kipaza sauti aongee mbele ya makamera asipotoa boko basi atatoa kituko cha karne ama kuongea yasiyowezekana
Matamko ni mengi mno
Maelekezo ni mengi mno
Makatazo ni mengi mno
Maonyo ni mengi mno
Yani haya ni mengi mno mpaka yanapishana barabarani na kupigana vibega
Kuna tatizo kubwa la kiuongozi na hili lina mizizi mirefu tangu ang'atuke mwalimu. Je, kwa mtazamo wa kiroho ni lile kafara la Lindi?
Wakati utaongea. Hebu tuupe muda!
Taifa letu linatakiwa kupiga watu tangia shule za awali hadi chuo kikuu. Vijana walioiva uzalendo na walio shibishwa na kushiba sababu za kwanini ni jukumu lao kuhakikisha Taifa hili linapaa katika anga za ndani na nje ya mipaka yetu."UMULIKE HATA NJE YA MIPAKA YETU". Ina maana ndani ya nchi tubaki gizani kama tulivyo sasa?
Heshima yako Mkuu Mshana, Heshima yako Mkuu wa Kilinge mstaafu...
Ama baada ya Salam nitoe ufafanuzi hapo "hata nje ya mipaka yetu" sentensi hii Ina maanisha ndani na nje ya mipaka"
Hivyo nitofautiane nawe kwenye hoja yako hapo juu!
Aidha
Naamini katika matambiko na Mila pia. Pia ni muumini wa maandalizi, Taifa letu linatakiwa kupiga watu tangia shule za awali hadi chuo kikuu. Vijana walioiva uzalendo na walio shibishwa na kushiba sababu za kwanini ni jukumu lao kuhakikisha Taifa hili linapaa katika anga za ndani na nje ya mipaka yetu.
Project hii ni ya miaka 17 hadi ishirini kisha tunaweza kuthubutu kusema nasi tuna watu wazalendo.
Umefafanua vizuri sana!Tukumbuke mfalme wa dunia ni shetani na ana namna zake kupoteza watu. Ana kuzimu yake chini ya bahari ,maziwa,mito wanakoenda kupewa utajiri,umaarufu ,nguvu za kutawala.Ila ana muda ukiisha ni hukumu na sio kwamba wanaokufa na dhambi hawapati adhabu wanapata.
Kuzimu real ni huko kunakowaka moto na ndiyo wafu wanateseka huko wakisuburia hukumu ya mwisho.Mafundisho ya uongo ya kuhusu Mahurulaini na Purgatory (toharani), imani za kishetani, mafundisho ya vyama vya Siri na kuundaa ulimwengu kuja kwenye New World Order kupitia mfumo wa kidunia yaani kiutawala, elimu na Burudani zote,Sayansi na teknolojia yanaendelea kufundishwa.
Mwili unakufa ila roho haifi hata milele, yaani mwili (body) kati kati Kuna nafsi ( soul) na then roho (spirit). Majini ,mapepo ,wakuu wa anga na viumbe vyote vichafu au fallen angels hawana miili wanategemea kutumia ya wanadamu.