Kuna tatizo mahali kwenye nafasi ya uongozi nchi hii. Je, kafara la Lindi linahusika?

Your browser is not able to display this video.
 
Mkuu kwani huyo alikwambia hafanyi kazi au ana shida? Hebu tujaribu kuheshimu maarifa usiyoyajua haswa kama huna ujuzi nayo.
 
Tanzania hamna cha kafara wala nn-Changamoto ya Tanzania ni katiba-Ambayo Nyerere aliipenda kwa sababu ilikuwa inampa madaraka makubwa na ambayo baadaye alikuja kuikosoa kwa sababu aliijua ni mbaya kwa sababu alihofia viongozi wengine wangeitumia kama yeye au zaidi.Makafara Nyerere aliyoyafanya Bagamoyo wala siyo sababu ya Tanganyika kupata uhuru mapema kutoka kwa wakoloni kama baadhi ya watu wanavyosema-Kiufupi ni kwamba baada ya WWII-Marekani na mataifa mengine kupitia forum mbalimbali za kimataifa walianza kupinga sana ukoloni-Hvyo waingereza na mataifa mengine kutokana na mbinyo waliachia makoloni yao mengi sana duniani.Kingine kilichopelekea Tanganyika kupata uhuru mapema ni kwamba hatukuwa na rasilimali nyingi kiivyo walizohitaji wakoloni pamoja na mambo mengineyo;Therefore Nyerere hata asingefanya makafara bagamoyo uhuru lazima tungepewa-sababu upepo wa dunia ulikuwa umeshabadilika.
Kuhusu mambo ya Lindi wala hayana msingi kiivyo-Kikubwa MEKO alishupaza shingo yake kwa kuamini mambo ya kale kwenye dunia ya kisasa-CORONA ikampitia.Maandiko huwa yanasema upumbavu hupelekea maangamizi na ndicho kilichotokea.
Kwenye masuala ya safu ya viongozi ukiangalia kiundani utaona kabisa MEKO alikuwa anaokoteza okoteza watu wasiokuwa na maadili wala misingi ya kiuongozi kama Bashite nk. hvyo haikuhitaji fikra kubwa sana ya kuelewa matokeo yake mwishoni ni nn-Haya Matamko ya hovyo,Maelekezo yasiyoeleweka nk uliyoyaainisha ni matokeo ya okoteza okoteza hii aliyoileta MEKO na ni matokeo ya viongozi waliokosa sifa.
Ingekuwa Taifa hili kuna sehemu ambayo makafara yangekuwa yanafanywa ili kiongozi aishi au utawala uwe mwepesi-Nadhan MEKO angekuwa anafanya kila saa kuliko kiongozi yeyote yule manake ndiyo vitu alivyokuwa anaviamini na kuviishi na utawala ulikuwa kama umeshaanza kumshinda.Na kwa jinsi alivyokuwa na chuki na mgombea urais mwenzake wa chama pinzani-nahisi angeyahamishia kabisa hayo makafara hadi ikulu ili apate access ya kuyafanya kila dakika ili amtoe roho madhabahuni mpinzani wake.Kiufupi Mkono wa MUNGU ukijitenga na nchi ni tabu sana.
 
Niwashukuru nyote mlioleta madini humu kuufumbua Umma macho, pia niwaambie kuwa lengo la mazindiko haya makubwa yaliyofanyika sehemu mbali mbali katika bahari, mito, milima, mabonde, majangwa, njia za panda kubwa, misituni nk yalikuwa na nia nzuri kwa upande wao walioyataka.

Walitaka nguvu za kiutawala (wakafanikiwa)

Nguvu za kusikilizwa (wakafanikiwa)

Nguvu za ulinzi nk nk wakafanikiwa kiasi cha kuwa na power hadi ya kuwakomboa wengine katika mataifa yao.

Tatizo limekuja baada ya baadhi ya viongozi waliofuata kutokuzingatia masharti na maagano ya awali na jambo hili ni baya hivyo wakuu wa anga wamekasirika na tutegemee haya;

Mifarakano baina ya viongozi na viongozi na mengineyo mengi mazito ambayo hayasemeki.
 
Nyerere kilichomwondoa pia ni mbinyo wa mataifa makubwa duniani kutaka nchi ifanye mabadiliko mojawapo ni kupitia SAP.Kwangu mm naweza kusema ni heri Meko kuliko Nyerere katika maswala ya udiktekta na utawala mbovu.Nyerere hajawah kuwa kabisa kiongozi wa mfano kwangu,na ninachoamin kilichomfanya watu hawamjui vyema ni kutokana na kwamba kwenye utawala wake hakukuwa na mitandao ya kijamii-hii ndo ilikuwa salama yake.
 
"UMULIKE HATA NJE YA MIPAKA YETU". Ina maana ndani ya nchi tubaki gizani kama tulivyo sasa?

Heshima yako Mkuu Mshana, Heshima yako Mkuu wa Kilinge mstaafu...

Ama baada ya Salam nitoe ufafanuzi hapo "hata nje ya mipaka yetu" sentensi hii Ina maanisha ndani na nje ya mipaka"

Hivyo nitofautiane nawe kwenye hoja yako hapo juu!

Aidha

Naamini katika matambiko na Mila pia. Pia ni muumini wa maandalizi, Taifa letu linatakiwa kupiga watu tangia shule za awali hadi chuo kikuu. Vijana walioiva uzalendo na walio shibishwa na kushiba sababu za kwanini ni jukumu lao kuhakikisha Taifa hili linapaa katika anga za ndani na nje ya mipaka yetu.

Project hii ni ya miaka 17 hadi ishirini kisha tunaweza kuthubutu kusema nasi tuna watu wazalendo.
 
Taifa letu linatakiwa kupiga watu tangia shule za awali hadi chuo kikuu. Vijana walioiva uzalendo na walio shibishwa na kushiba sababu za kwanini ni jukumu lao kuhakikisha Taifa hili linapaa katika anga za ndani na nje ya mipaka yetu.

Project hii ni ya miaka 17 hadi ishirini kisha tunaweza kuthubutu kusema nasi tuna watu wazalendo.[emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1752][emoji1752][emoji1752][emoji1548][emoji1548][emoji1548]
 
Umefafanua vizuri sana!

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…