Wakuu tunaomba mjitahidi kutoa huduma inayoeleweka. Sijui ni nani anaepanga route za magari maana imagine mtu unakaa kituoni lisaa lizima gari zinapita chache mno na zimejaa hakuna hata pa kusimama.
Mtu unaamua uende hadi terminal ya kivukoni au gerezani unakuta hali ndio haifai. Jitahidi kuamrisha magari yaondoke maana unakuta yamepaki tu na watu wanasubiri huduma. Kuna wakati mnajitahidi ila mda mwingi kunakua hakuna coordination nzuri.
Hebu angalia hizi picha na ni mchana tu saa nane saizi hali ni hivi.
Kama tatizo lingekua uchache wa magari basi tusinge experience hii shida muda wa mchana. Lakini imekua kinyume chake yaani mchana hali inakua mbaya zaidi.
Kama kuna tatizo ombeni serikali ichukue hatua au hadi wawachukulie nyie hatua?
View attachment 2468757View attachment 2468758View attachment 2468759