Kuna tatizo zaidi ya bei za vufurushi: Tunaomba liangaliwe

Kuna tatizo zaidi ya bei za vufurushi: Tunaomba liangaliwe

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
5,628
Reaction score
6,411
MABORESHO YA HUDUMA ZA MITANDAO YA SIMU YASIANGALIE VIFURUSHI TU.

Wakati huu ambapo mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) inajiandaa kuboresha sheria za matumizi ya vifurushi ili kuleta ufanisi mzuri kwa watumiaji ni vizuri na masuala yanayohusu kihamisha data -kasi( broad band), muunganisho kasi wa tovuti, mtandao wa kihamisha data kasi na ukawivu viangaliwe kwa sababu tatizo siyo bei za vifurushi tu.

Kulingana na takwimu zilizotolewa na "Speed test Global index mwaka 2021, wastani wa kasi ya mtandao Duniani ni 46.94 Mbps( Kupakua), 12Mbps ( kupakia) na ukawivu ni 37 ms.

Nchi za Umoja wa falme za Kiarabu (UAE) zinaonesha kufanya vizuri sana katika suala la kasi ya mtandao kwa kuwa na kasi ya kupakua 177.16 Mbps.

Nchi ya Tanzania ni ya 134 ikiwa na kasi ya kupakua 11.72 Mbps, kasi ya kupakia 7.10 Mbps na ukawivu wa 42 ms.

Nchi ya Kenya inashika nafasi ya 87 ikiwa na kasi ya kupakua 23.90 Mbps, kasi ya kupakia 12.99 Mbps na ukawivu wa 33 ms.

Nchi ya Uganda inaonekana kuwa na kasi ya 127 Duniani kwa kuwa kasi ya ya kupakua 14.46 Mps, na kasi ya kupakia 6.4 pamoja na ukawivu wa 32 ms.

Tanbihi; Takwimu hizo zinaonesha wazi kuwa bado tupo nyuma katika kasi ya mtandao na hivyo katika kufanya maboresho yenye mawanda mapana ya kuwasaidia watumiaji ni vyema masuala haya yote yakaangaliwa.

Inaeleweka kuwa tatizo la kasi ndogo lina athari pia katika uchumi wa watumiaji.Hivyo basi, ni vyema masuala haya yote yakaangaliwa kwa pamoja.

Naomba kuwasilisha.
 
Kweli kuna umuhimu sana wa management ya TCRA kubadilishwa wafanyakazi.

Inamaana Staff nzima inafanya nini? Watanzania tunakuwa behind tu kwa kila jambo? Mimi mengine hata sikujua.

Yaani delaying ya uploading & Downloading ni kubwa wakati kwa wenzetu iko faster, okay kwanini hawakushughulikia hilo au hata hawakunotice?

Dah, Bongolalaz
 
Serikali kama ina nia thabiti na ya dhati isiangalie bei za vifurushi tu kwa sababu bei hizo hazina faida kubwa kwa mtumiaji kama ilivyo kwa mfanyabuashara hata kama zikipunguzwa endapo kasi ya mtandao ni ya aina hii tuliyonayo.

Aina ya huduma ya mtandao na ubora wake ni mambo ya muhimu sana kuangaliwa badala ya kunga'nga'na na kushuka bei tu. Hivi bei ikiwa ndogo halafu kasi ya mtandao ndiyo hii ya mwendo wa pole sidhani kama hili ndilo Watanzania tunahitaji.

Tunahitaji huduma bora kabisa ya Mtandao katika ama hizi kuliko wakati wowote ule, kasi ya mtandao siyo jambo la kupuuzia hata kidogo. Makampuni ya mitandao tumepata faida kubwa ana kwenye mauzo yao huku kasi ikiwa bado ni ndogo na anayeumia ni mlaji huku chini.

Embu angalia hii, Mwaka 2015 umoja wa mataifa ulibaini kuwa watu bilioni nne hawapati mtandao wa kabisa internet. Kaa.ni hivyo ina maana kuwa biashara inavyoendelea hapo siyo biashara bora inayoendana na malengo endelevu ya Dunia ( Sustainable Development Goals SDG's).
 
Kweli kuna umuhimu sana wa management ya TCRA kubadilishwa wafanyakazi.

Inamaana Staff nzima inafanya nini? Watanzania tunakuwa behind tu kwa kila jambo? Mimi mengine hata sikujua.

Yaani delaying ya uploading & Downloading ni kubwa wakati kwa wenzetu iko faster, okay kwanini hawakushughulikia hilo au hata hawakunotice?

Dah, Bongolalaz
Je hiyo wizara na TCRA wana wataalamu wajuayo hayo.? Kama wapo basi walikaririshwa !!
 
Tanzania ni miongoni mwa Nchi zinazotumia broadband yenye kasi ndogo lakini bado watu wanawazakuongeza bei ya vifurushi.

Simu na download mpaka inapata moto kama pasi.
 
Tatizo ni ufinyu wa ubunifu unaoendana na ushindan wa soko ulivyo ndio unaotesa viongozi na watendaji wetu wengi.
 
Hapa ni vita kati ya reactive measures versus proactive measures.
 
Tanzania ni miongoni mwa Nchi zinazotumia broadband yenye kasi ndogo lakini bado watu wanawazakuongeza bei ya vifurushi.

Simu na download mpaka inapata moto kama pasi.
Hahahaaa.... Ila kwangu jana niliona utofauti wa halotel... Ndani ya nusu dakika nilishusha file ya 60+ mb
 
Back
Top Bottom