Tetesi: Kuna Tetesi za kufanyika mabadiliko ya Utawala Zanzibar

Tetesi: Kuna Tetesi za kufanyika mabadiliko ya Utawala Zanzibar

Katika hali halisi ya Zanzibar, lolote laweza kutokea...

Mimi siwezi kudharau tetesi hii kwa kuangalia ushahidi wa kimazingira.....

Mosi, mgogoro wa CUF Lipumba na CUF Seif Sharrif Hamad umepoa na ni kana kwamba na wao wanaendelea kuwekana sawa..

Pili, makeke ya siasa za pande mbili huko Zanzibar kwa maana ya CCM na CUF, si kama ilivyozoeleka. Wote hawa wako so cool na hii hali ina indications za kuwa, kuna jambo linaendelea huko...

Tatu, Zanzibar kunyimwa uanachama FIFA kama taifa linalojitegemea ni lazima liliwasononesha wazanzibari wote bila kujali itikadi zao. Ni wazi hili liliwafanya wakae na kutafakari shida na tatizo lilipo...

Nne, Maalim Seif Sharrif Hamad is so cool, hajitokezi tokezi sana kwa sasa kuzungumza zungumza kama ilivyokuwa huko nyuma...

Hata ikitokea, basi mara zote huwa ni kuwatuliza wafuasi wake na wanachama wenye munkari wa CUF wanaosubiria na kuitaka haki yao ya ya kikatiba ya tarehe 25/10/2015 walipochagua viongozi wao lakini kwa mabavu, ikaporwa....

Mara zote huwa wanataka amri ya kamanda wao ya nini wafanye kama ameshindwa kuwaresheshea haki yao kwa njia ya amani...

Hii njia ya kudai haki through violence ndiyo inayotumiwa na Raila Odinga Kenya kwa kuwaamurisha wanaomuunga mkono na wafuasi wake kuingia barabarani. This is always hasn't been a good way to solve a problem...

Kama kutatokea shida Zanzibar, hata sisi huku bara tusidhani kuwa tutakuwa salama. Lazima tu athari za kijamii na kiuchumi zitukute.....

Sasa kama hata sasa kwa makosa mengine madogo dogo tu na ya kijinga wa kujua ama kutojua ya kiutawala yanayofanywa na Magufuli na serikali yake watu tunaisoma namba, je kukitokea vurugu na kupigana mambo yatakuwaje?

Ni wazi the situation will be worse!

Hii si njia nzuri na njema hata kidogo na siku zote kushughulikia unrest political situation ktk taifa lolote. Ni njia ambayo ina madhara kijamii na kiuchumi....

Na hili likifanyika Zanzibar, vile visiwa vitakuwa na maafa makubwa sana kwa sababu hakuna CCM Zanzibar iwe hupendi kusikia hili ama vyovyote.... lakini huo ndiyo ukweli mchungu sana kwa wanaCCM...

Zanzibar inakaliwa/tawaliwa kimabavu tu na Tanganyika from Dodoma/DSM. Ndiyo maana ikitokea ishu tu huko, raslimali zote ambazo ni sharti zitumike kwa maendeleo yetu Watanganyika zitahamishiwa huko ili kuweka sawa koloni letu!

Do we want that???

Kishada, tetesi zako zinaendana na halisi ya Zanzibar . Na kwa maelezo haya, lazima kuna kitu kinaendelea huko jambo ambalo ni zuri tu kwa kweli..
 
CUF wasubiri tu .....kutokua na kitengo...imara cha ujasusi...kunawaponza Cuf
Hujuma walizofanyiwa ni nyingi lakini wenzao...chadema...wameweza kutanzua nyingi ya hujuma.
Kwa sasa Tanzania chadema wana idara ya ujasusi bora kuliko vyama vyote

Ccm baada ya waTu kama Kanali Muhando kuondoka idara ya ulinzi,usalama na maadili imeshusha kwa kasi na ni kama haina tena inteligensia na wanatumia TISS 100%
Hii inaifanya ccm kuwa chama dola...na ni hatari sana kwakuwa kimsingi wanateegemea watu ambao katiba inawataja hawana vyama na kimoyo moyo nao wana vyama vyao wanavyoviunga mkono...so as long as ccm sio...maslahi ya taifa waliyoapa kuyalinda nao wana mapenzi binafsi kama...raia huru na ndio maana wengi wanavujisha siri za ccm
 
Hospitali ya mtendeni katika ubora wake, ni kusambaza dripu tu.

Eti mambo nyuma ya Pazia.... Au CCM wanahofu, wakati kutwa wapo kisonge wanacheza bao ikifika usiku wanaandika matusi, kisha unasema wana hofu?

Labda mpaka uelewe kuwa hao ba Sefu anaowafata kuwaomba msaada wa ufumbuzi, hawako serious na wana mkono umo CCM. Ukielewe hili ndio utajua nyuma ya pazia kumbe kuna dirisha tu. Tetesi zilianza baada ya jecha kufuta uchaguzi, wiki inayofata anaapishwa sefu mpaka leo hakula kiapo. Kwaio na hizi unazozileta, ndo zile zile.

Wamezuia misaada kisha wakawa wanatoa wenyewe, kabla ya hiz tetesi!

Mzungu anafatwa anaambiwa wazanzibar wameibiwa, hawakubali, hawamtambui rais. Mzungu anafunga safari kuja kutizama anakuta shughuli zinaendelea kama kawaida, watu hawajali, TENA YEYE ATAJALI VIPI?
 
Back
Top Bottom