GE2025 Kuna tija gani ya kushiriki Uchaguzi chini ya mazingira yaliyopo?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Afrobaremeter imeshasema mgombea wetu anakubalika na atashinda uchaguzi kwa 82%, wameanza yale ya akina Januari na Nape kuwa Magufuli atashinda kwa asilimia 84 na kweli akashinda kwa kura fake kwa asilimia 82.
Ujinga ujinga Ujinga umeanza
Wameanza na kusema ccm ina wanachama 13m+, lengo ni ili iTally na idadi ya kura wanazotaka kupika. Kinachotakiwa ni idadi ya kuhadaa ulimwengu kuwa idadi kubwa wanamkubali kiongozi huyu na chama chake. Kitendo cha cdm kuutia shombo uchaguzi kimewaumiza mno ccm na vibaraka wake, maana wanajua itashusha sana voters turn out.

Kwa mazingira yalivyo cdm hawawezi kuzuia uchaguzi usifanyike. Lakini kampeni ya NRNE itachangia sana kushusha idadi ya wapiga kura. Idadi itakavyokuwa ndogo itashusha pia uhalali wa serekali iliyoko, kwani itakuwa kisheria, lakini isiyo na uhalali wa umma. Pia viongozi wataokakuwa madarakani hawatapa ushirikiano wa kutosha toka kwa wananchi wengi, kwani itakuwa hawakuwachagua.
 
u.s.a baby unawashwa nini na mambo yahuku wakati wewe upo majuu?
 
Baada ya kusikiliza na kutizama picha mjengeo ya yule aliyekuwa DC LONGIDO,pia ile ya aliyewahi kuwa katibu muenezi wa CCM Nape Nnauye akiwa pale mjini Bukoba sijisumbui kurudia kufanya ujinga.
 
Hapa kuna Kambi mbili;

Moja ni sisi tuliojiandaa kupiga kura aidha kwa utashi wetu au kwa matakwa ya Katiba ili LAZIMA Serikali iwepo na mambo yaende.

Pili ni ninyi ambao hamuamini katika kupiga kwasababu ya irregularities zozote mnazoziona au mnazofikiri zipo.

Ushauri wangu. Kila mtu ajitahidi kuvua samaki wengi atakavyoweza ila azingatie matakwa ya Katiba yanayosema "Ushindi wa Udiwani, Ubunge na Urais utatokana wa wingi wa kura zilizopigwa". Hili ndilo la muhimu na la kuzingatiwa.

Mimi Mtoto wa Shule Oktoba "NINATIKI"✓
 
Uchaguzi huo ambao matokeo yanajulikana utagharimu Tsh Trilioni moja

Bila ya huu Uchafuzi uitwao uchaguzi unategemea watu wale vipi na nini >?? Ugonjwa wa Bora tumbo, umewatoa ubinaadamu
 
Kuna tija gani kushiriki kwenye uchaguzi ambao utaendeshwa na kusimamiwa na tume ambayo imeundwa na mmoja wa wagombeaji urais?
Kiukweli ni upotevu wa muda na kutojali pesa za walipa kodi ambao ni wananchi tena maskini sana.
 
Hata enzi za chama kimoja watu walikuwa wanapiga kura 🤣!
 
Kwa wenye akili zao timamu, ambao hawafungamani na upande wowote...Best option siku ya uchaguzi ni kununua nyama au kuchinja mnyama na kufanya siku ya "braai"!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…