Uchaguzi mkuu wa 2025 haupo mbali!
“Voices from within” 🤣 zinaniambia CCM itashinda tu. Na ikitokea wakashinda kweli, msiache kunipa credit ya kutabiri kwa usahihi, sawa ndugu zanguni eh? 🤣🤣.
Moja ya ujinga na upumbavu wa Watanzania ni kutoa sifa kwa mambo yaliyo dhahiri kabisa.
Anaibuka mtu anasema “voices from within” zinamwambia kuwa Rais Samia atashinda uchaguzi ujao.
Na kweli, baada ya uchaguzi Samia anatangazwa kuwa mshindi halafu wanaibuka wapumbavu na kuanza kumsifia huyo aliyedai “voices from within” zilimwambia kuwa Samia atashinda!
Hao ndo Watanzania bana. Na hizo ndo akili zao.
Nikitabiri kuwa mwaka kesho, 2026, mvua zitanyesha kwenye sehemu mbalimbali nchini, na ikatokea zikanyesha kweli, kuna mazuzu wataniona mimi ni genius 🤣.
Predicting the obvious is not genius.
Sasa basi, kwa sababu wote tulio na akili timamu na tulio wahalisia wa mambo tunajua kwamba Rais Samia na CCM watashinda kwa kiwango kikubwa sana, binafsi nina swali:
Kuna tija gani katika kushiriki uchaguzi ambao matokeo yake yanajulikana?
Kuna tija gani kushiriki kwenye uchaguzi ambao utaendeshwa na kusimamiwa na tume ambayo imeundwa na mmoja wa wagombeaji urais?
Kwa nini watu washiriki uchaguzi ambao hawana nafasi yoyote ile ya wao kuweza kushinda?
Ngoja nifanye utabiri mwingine. Itakuwa hivi:
Kwa wale wataoshiriki kwenye huo uchaguzi, Rais Samia akishatangazwa kuwa mshindi, watalalamika kuwa wameibiwa kura na kwamba uchaguzi haukuwa wa huru wala haki.
Uchaguzi kutokuwa wa huru wala haki ni jambo ambalo wanalifahamu fika kabisa kabla hata uchaguzi haujafanyika.
Licha ya kufahamu yote hayo, bado wapo watu ambao watashiriki huo uchaguzi na baadaye wataanza kulalamika.
Sasa kuna tija gani ya kushiriki uchaguzi kwenye mazingira yaliyopo halafu baadaye unaanza kulialia kuwa umeibiwa kura?
I don’t want to hear any of you crying about the unfairness of the election after it’s over.
Nani anabisha kuwa Rais Samia atashinda?