Kuna tofauti gani kati ya Hayati na Marehemu?

kamkoda

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2012
Posts
396
Reaction score
71
Kwa wale wajuzi wa lugha yetu tofauti ya maneno hayo ni nini hasa?

Michango ya wadau
 
Ningependa kujuzwa tofauti ya vyeo hivi wanavyopewa watu walio fariki, wengne wanaitwa Hayati na wengne Marehemu..

Mfano HAYATI JULIUS K. NYERERE, MAREHEMU STEVEN KANUMBA..
 
Nijuavyo marehemu ktk uhai wake was just a mere persön mwenye maisha ya kawaida while hayati wanakuwa na title flan ktk jamii!
 
Kaaaazi kweli kweli kiongozi.Marehemu ni jina apewalo mtu YEYOTE aliyefariki.Hayati ni mwenye uhai.
 
Kaaaazi kweli kweli kiongozi.Marehemu ni jina apewalo mtu YEYOTE aliyefariki.Hayati ni mwenye uhai.

Mmh mkuu unajua mtu anapouliza sometime anakua serious anataka kujua,sasa unapomwambia kitu kama hicho hapo cjui kama unamtendea haki,anajua wote wanakuwa wamefariki sasa wewe unamwambia hayati anakuwa hai tena duuh,,ni shidaaaah
 
Mmh mkuu unajua mtu anapouliza sometime anakua serious anataka kujua,sasa unapomwambia kitu kama hicho hapo cjui kama unamtendea haki,anajua wote wanakuwa wamefariki sasa wewe unamwambia hayati anakuwa hai tena duuh,,ni shidaaaah
Kiongozi pole kama nimekukwaza, si nia yangu.Kwa ufahamu wangu,asili ya maneno haya mawili ni lugha ya kiarabu.Al marhum,marehemu,na hayyat enye uhai.

Yapo mafuta ya kula yanaitwa hayyat bila shaka umewahi kuyaona.....lakini kumbuka kiongozi elimu haina mwisho.Wengine watatuelimisha zaidi.Karibu tafadhal.
 
Marehemu ni mtu aliye kufa lakini bado hajazikwa. Ndio maana huwa tunauliza alirehemeka lini? Hayati ndio alishafukiwa 6*6. Swali zuri.

Hayati " the late"
Marehemu " late"
 
Mh, sio haki wadau, wakiwa hai waheshimiwa, wakifa mahayati mbona wanatufisadi hadi kwenye vifo mph!!!"""
 
marehemu ni mtu aliye kufa lakini bado hajazikwa. Ndio maana huwa tunauliza alirehemeka lini? Hayati ndio alishafukiwa 6*6. Swali zuri.

Hayati " the late"
Marehemu " late"

Asante mkuu
 
Hayati linatumika kwa kiongozi au mtu aliyekuwa na hadhi katika jamii, ambaye amefariki.

Marehemu linatumika kwa mtu wa kawaida aliyefariki.
 
Mara nyingi mtu anapofariki jina lake hutanguliwa na neno 'marehemu'na wachache sana 'hayati' je kuna sifa maalum ambazo zinasababisha kutanguliwa na maneno hayo? Je kwa Tanzania kuna hayati mwingine zaidi ya baba wa taifa?
 
Ninadhani ni kama Mr. na Hon.

Kiingereza cha hayati ni nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…