Kuna tofauti gani kati ya Hayati na Marehemu?

Marehemu kabla ya mazishi. Hayati baada baada ya mazishi
 
Hayati Ni mtu aliyefariki Na kuzikwa kitambo, marehemu Ni mtu aliyefariki Na Kama kuzikwa Ni siku kadhaa Tu!
 
Hayati hutumiwa kwa mtu maarufu siku kadhaa baada ya kuzikwa, marehemu hutumiwa kwa mtu asiye maarufu.
Note : kabla ya mazishi wote huitwa marehemu.
Vipi Kuna Hayati mpya ametokea nini?
 
Hayati ni neno la kiarabu likimaanisha uhai, kwa hiyo mtu aliyekufa na kuacha Legacy yaani bado kuna vitu alifanya kwa manufaa ya jamii au dunia na bado vinaishi huyu ndiye huitwa hayati kwa maana kafa lakini bado anaishi kutokana na legacy aliyoiacha wala siyo lazima kuwa maarufu au tajiri.

Hata Masikini anaweza kuacha Legacy, kwa mfano anaweza kusema ana eneo lake ligeuzwe kujengwa shule au hospitali au kisima au msikiti au kanisa na ikafanyika hivyo huyu ni hayati maana kaacha legacy kile alichokuwa akimiliki pamoja na umasikini wake bado kinaishi na kinainufaisha jamii aliyoiacha.

Mwingine anaweza kufundisha ujuzi vijana na wale vijana wakanufaika na ule ujuzi na ukanufaisha jamii, kwa hiyo elimu yake aliyoitoa bado inaishi na inainufaisha jamii huyu naye ni hayati.

Lakini ukifa na kashfa kibao za ufisadi wa mali, ufisadi wa mapenzi au dhulma au uchawi yaani kifo chako kikaleta nafuu kwa jamii, basi wewe ni marehemu tu huwezi kupewa heshma ya kuitwa hayati.

Kwa hiyo kila mtu ajitathmini kama yeye akifa ataitwa Hayati au Marehemu?
 
Ushauri wa bure fikiri mara mbili mbili kabla hujaandika kitu. Kwanini unakuwa na dhihaka hivi?

Tujifunze kuwa serious katika kuelimishana na sio kuleta utani na mizaha maana haisadii kitu.
Umeongea point ndugu yangu,kuna wengine wanafanya mzaha mahali sio pake,
 
Mimi nijuavyo maneno yote mawili marehemu na hayati hutumika kwa kutangulizwa kabla ya kutaja jina la mtu aliyekwisha kufariki.

Lakini tofauti yake ni kwamba neno marehemu linatumika bila kujali kama aliyefariki amefariki leo muda mfupi uliopita, wiki iliyopita, miaka kumi, miaka hamsini au zaidi iliyopita wakati hayati linatumika pale mtu anaezungumziwa habari zake alikuwa ni mtu maarufu katika jamii tena anakuwa alifariki muda mrefu kidogo uliopita pengine miaka kadhaa nyuma mfano hayati Mwalimu Nyerere, hayati Shaaban Robert na wengineo. Pengine ndiyo maana mleta mada umekuwa ukisikia akina "hayati" wachache tofauti na marehemu kwa sababu wengi tunakufa bila umaarufu wowote au kuacha legacy yoyote nyuma yetu.

Sijawahi kusikia mtu aliyefariki mfano leo asubuhi au jana akatanguliziwa jina la hayati.
 
Mara nyingi mtu anapofariki jina lake hutanguliwa na neno 'marehemu'na wachache sana 'hayati' je kuna sifa maalum ambazo zinasababisha kutanguliwa na maneno hayo? Je kwa Tanzania kuna hayati mwingine zaidi ya baba wa taifa?
Haya maneo ya Marehemu(Apate Rehema za Mungu) na Hayati(mwenye Afya,uzima)yanatoka katika lugha ya kiarabu.Neno hasa la kutumika kwa aliyefariki ni Marehemu,ukitumia neno hayati ,ni makosa kwasabau hayati ni uhai sio kifo.
Na neno marehemu mara linatumika sana kwa Muislamu aliyefariki,na Hayati linatumika zaidi kwa watu wa dini nyinginezo.Lakini maana halisi ya hayati kwa kiarabu,ni uhai.
Neno la kiarabu linatwamkwa Al marhum Fulani bin Fulani.
 
Mtu akifa amekufa tu, hakuna cha hayati wala marehemu.
 
Hayati ni neno la kiarabu likimaanisha uhai, kwa hiyo mtu aliyekufa na kuacha Legacy yaani bado kuna vitu alifanya kwa manufaa ya jamii au dunia na bado vinaishi huyu ndiye huitwa hayati kwa maana kafa lakini bado anaishi kutokana na legacy aliyoiacha wala siyo lazima kuwa maarufu au tajiri.

hata Masikini anaweza kuacha Legacy, kwa mfano anaweza kusema ana eneo lake ligeuzwe kujengwa shule au hospitali au kisima au msikiti au kanisa na ikafanyika hivyo huyu ni hayati maana kaacha legacy kile alichokuwa akimiliki pamoja na umasikini wake bado kinaishi na kinainufaisha jamii aliyoiacha.

Mwingine anaweza kufundisha ujuzi vijana na wale vijana wakanufaika na ule ujuzi na ukanufaisha jamii, kwa hiyo elimu yake aliyoitoa bado inaishi na inainufaisha jamii huyu naye ni hayati.

Lakini ukifa na kashfa kibao za ufisadi wa mali, ufisadi wa mapenzi au dhulma au uchawi yaani kifo chako kikaleta nafuu kwa jamii, basi wewe ni marehemu tu huwezi kupewa heshma ya kuitwa hayati.

Kwa hiyo kila mtu ajitathmini kama yeye akifa ataitwa Hayati au Marehemu?
Kutokana na maelezo yako mkuu je Matonya aliyekuwa maarufu kwa kuomba mgogo yule ni hayati au marehemu?! Maana kama legacy kaacha maana watu wakiomba tu huitwa Matonya means anaishi bado
 
Kwa kifupi neno hayati ni uhai wenye Afya,sio uhai wa kuwa umekufa,halafu,uitwe uko hai.
 
Tofaut ipo kwetu binadamu, marehemu mtu wa chini ktk jamii. Hayati wenzetu wenye madaraka na heshima hapa dunian
 
Hayati ni neno la kiarabu likimaanisha uhai, kwa hiyo mtu aliyekufa na kuacha Legacy yaani bado kuna vitu alifanya kwa manufaa ya jamii au dunia na bado vinaishi huyu ndiye huitwa hayati kwa maana kafa lakini bado anaishi kutokana na legacy aliyoiacha wala siyo lazima kuwa maarufu au tajiri.

hata Masikini anaweza kuacha Legacy, kwa mfano anaweza kusema ana eneo lake ligeuzwe kujengwa shule au hospitali au kisima au msikiti au kanisa na ikafanyika hivyo huyu ni hayati maana kaacha legacy kile alichokuwa akimiliki pamoja na umasikini wake bado kinaishi na kinainufaisha jamii aliyoiacha.

Mwingine anaweza kufundisha ujuzi vijana na wale vijana wakanufaika na ule ujuzi na ukanufaisha jamii, kwa hiyo elimu yake aliyoitoa bado inaishi na inainufaisha jamii huyu naye ni hayati.

Lakini ukifa na kashfa kibao za ufisadi wa mali, ufisadi wa mapenzi au dhulma au uchawi yaani kifo chako kikaleta nafuu kwa jamii, basi wewe ni marehemu tu huwezi kupewa heshma ya kuitwa hayati.

Kwa hiyo kila mtu ajitathmini kama yeye akifa ataitwa Hayati au Marehemu?

una maanisha Capt komba ni marehemu na siyo hayati kama ulivyotoa tafsiri hapo juu
 
Back
Top Bottom