Kuna ubaya gani kwa serekali yetu kulitwaa eneo la vingunguti na kujenga makazi ya kisasa

Kuna ubaya gani kwa serekali yetu kulitwaa eneo la vingunguti na kujenga makazi ya kisasa

Mleta mada umekuja na wazo zuri. Tulishamshauri 2013 Bwana Mchechu akiwa Boss wa NHC kuhusu miradi ya aina hiyo chini ya PPP na wanachi wenye Ardhi halafu unampa apartment moja. La kufanya ni kuwapa kodi ya pango miaka mitatu baada ya kukamilika mradi wanapata makazi mazuri na hati miliki safi. Tukashauri aanzie Morogoro road pale tip-top hadi magomeni lakini bahati mbaya hakuweza kutekeleza.
Watumishi housing walijaribu pale Magomeni ndani ya miezi 2 wakajaza majengo. Magomeni Kota imejaa pia. Kuna maeneo mengi ya urban renewal lakini ndio hivo sio priority kwa our urban authorities.
 
Huitaji mongozo ya muda mrefu na ya nguvu moja, siyo baada ya miaka 10 kila mmoja anakuja na kipaumbele chake tofauti...
 
Kwanini serikali ifanye kila kitu?

Hizo ndio fursa walifaa wapewe wawekezaji msingi ni waboreshewe mazingira rafiki ya kuwekeza hiyo monopoly ya serikali kutafuta sifa kwenye ndege ndio inawaletea hasara sasa sababu fastjet na wengineo wangeleta ushindani sokoni na mtu atachagua ubora wa huduma.
 
Ipo haja ya serekali yetu kuona umuhimu wa suala hili, kwa ni eneo ambalo lipo kilometre chache sana kutoka city center, linastahili kuwa upgraded n kufanana na maeneo ya upanga na kwingineko, pia ni eneo ambalo linaeweza kupangwa tukapata kariakoo 2,mpangilio wa ujenzi ufanywe kwa wenye maeneo yao mradi utakapomalizika wapatiwe nyumba zao permanent na hati zao.
Huo mradi bora upelekwe Dodoma huko
 
Kilichofanyika Magomeni Kota inabidi iwe mwongozo. Kama waliweza kuvunja zile nyumba na wakajenga za kisasa na wakazi wa awali wakapata nyumba basi inawezekana kufanya kwingine.
Yeah. Unawajengea nyumba za kisasa halafu wanakaa free mwaka m'moja then Booom unawapa bili halisi ya kuishi kwenye flats....

Umeme, takataka, ulinzi, usafi, maji, etc, wenyewe wataomba pooo watawapisha wakishua eneo litastaarabika.....
 
Vingunguti ni eneo ambalo watu wake baadhi wana title deeds, hivyo hekima ni mwekezaji atakapopatikana kila mwenye deeds awe na haki ya kupatiwa nyumba free permanent!
 
Kama tumeshindwa kuijenga New Dar town Kigamboni basi hayo mengine sahau hayawezekani, gharama ya Kigamboni ilikuwa ni kununuwa mashamba tu ya watu, ila vingunguti ni kununuwa nyumba za watu. Huo ni mradi usiokuwa na tija.
Kiukweli kigamboni kumekaa kushoto mno ingawa wapo wanaopapenda kweli, kwa vingunguti sikumaanisha serikali inunue nyumba ya mtu, nikimaanisha serekali ichukuwe hati za wenye nyumba, ijenge majengo ya makazi na kibiashara and then kila hati iliyochukuliwa irejeshwe kwa muhusika na apartment yake. Ili ku upgrade eneo hilo., kwa utafiti wangu buguruni inaweza kuwa kariakoo 2,. Ukizingatia tayari ina njia 4 kubwa, zinazotawanyika kila pahala.
 
Dar slams hazitakuja kuisha kwani makosa bado yanaendelea huko pembezoni hivyo ukimaliza vingunguti utakuta huko mbagala,pugu,bunju zimejaa
 
... pabaki hivyo hivyo. Vingunguti na Kiwalani ndio malango ya wageni kuingilia nchini; ndege ni almost zinakuwa zimekaribia kugusa bati za mbanda ya maeneo hayo ambayo yanakuwa yanaonekana kwa uwazi kabisa kutokea juu angani.
Ukiwa ndani ya ndege ukachungulia eneo hili dirishani utaikana nchi yako kwa hizo bati zilivyo na kutu.
 
Ipo haja ya serekali yetu kuona umuhimu wa suala hili, kwa ni eneo ambalo lipo kilometre chache sana kutoka city center, linastahili kuwa upgraded n kufanana na maeneo ya upanga na kwingineko, pia ni eneo ambalo linaeweza kupangwa tukapata kariakoo 2,mpangilio wa ujenzi ufanywe kwa wenye maeneo yao mradi utakapomalizika wapatiwe nyumba zao permanent na hati zao.
Buguruni yote inatakiwa kujengwa kisasa mji umejiminya usikuwe vizuri
 
Back
Top Bottom