Kuna ubaya kumwambia ex girlfriend wangu kwamba asinitafute maisha yake yote yaliyobaki?

Yani mimi nateseka kwa kumueleza ukweli kwamba asinitafute tena katika maisha yake ? Kwani nilizaliwa nae ? Manan angekua ndugu yangu nisingeweza kusema vile lakini yule ni girlfriend tu tena wote tumekutana ukubwani tukiwa na meno 32.

Halafu kwasasa mimi nina mpenzi mwingine ambae kamzidi kila kitu kwa uzuri mpaka tabia sasa kwanini niharibu mahusiano yangu mapya kwa kuendelea kuwasiliana na ex ambae sihitaji chochote kutoka kwake ?
Mimi sina muda mchafu wa ku entertain ma ex sababu ex kwangu is nothing but an imbecile.

Hakua bora kipindi tuko kwenye mahusiano akawe bora wakati tumeshaachana ?

Halafu niwasiliane na ex ili kugundua nini labda ?
 
Asee ikitokea manzi nimemzimia kishenzi ikatokea Tukaachana asee sitaki kumuona Tena Wala kumsikia I block everything about her halafu sijui kwann hawapend kukata mawasiliano na ex ZAO LABDA wanajisikia vizuri kucheza na hisia za wanaume

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha janja janja ya mbuzi kujambia mdomo. Huyo manzi bado unampenda ndo maana umepoteza muda wako wa thamani kuandika uzi unaomhusu. Jomba hakunaga shujaa wa mapenzi.. kwa sababu huyo manzi bado unampenda basi chukua jukumu la kukaa nae chini mmalize tofauti zenu muendelee kupeana mahaba. Kauli ya kumwambia binadamu mwenzako asikutafute kwa maisha yake yote ni kiduwanzi sana. Vipi kama atakutafuta akupe mchongo wa pesa ndefu? Acha kufanya maamuzi kwa hisia kama demu.
 
Simba la masimba ....Simba baba dangote umetoa madini mazuriiii balaaaa ⭐⭐⭐⭐🤝
 
Sijawahi kumtafuta sababu hakuna ninachohitaji tena kwake hata niwe vibaya vipi financially, kama nipo broke bora nikope hata kwa marafiki zangu lakini sio yeye.
Uku umefikia kubaya sasa.....Dunia ina meeng tumia akili sio hisia katika kufanya maamuzi
 
Usichokijua ni kwamba huyu manzi awali sikua na mpango wa kumtongoza ila ni yeye ndie aliejitonhizesha kwangu mpaka tukawa wapenzi.

Niliingia nae kwenye mahusiano kama bahati mbaya tu lakini hakuwa moyoni mwangu kabisa.

Sasa unanishangaza unaponiambia kwamba bado nampenda wakati kwasasa nina mwanamke ambae ni mzuri kuliko yeye kimuonekano na kitabia na isitoshe nishawahi hadi kumtumia picha ya mpenzi wangu mpya ili aache kunisumbua lakini wapi bado hasikii ndomana nimeona bora nimpige tofali la maisha.
 

Kama bado wampenda mrudie
 
Umeandika kama mtu mwenye jazba fulani hivi na chuki juu ya X-wako.
Umeachana naye na uliyenaye amemzidi kila kitu wala siyo hoja. Kumbuka kuna kuachana wala usifikiri uzuri wa huyo mwanamke uliyenaye wala penzi analokuonesha. Mapenzi ni ya kijinga sana.
Kumbuka mapenzi siyo ugomvi wala kuwekeana visasi.
Jifunze kusamehe, kuachilia na kupuuza. Mtu anakusalimia wala siyo issue ya mapenzi, sioni tatizo hapo. Tatizo litakuja kama mtaanza kuwasiliana kama wapenzi.
Kuwasiliana na ex kama marafiki siyo kila siku sioni tatizo
 
Kwa hiyo ulimchamba?
 
Huyu wa sasa nimezaa nae, sasa niharibu mahusiano yangu sababu yake ?
 
Huwa ananitext tu na huwaga nazijibu text zake kwa ufupi sana, ni busara tu huwa naonyesha lakini sio kama namuhitaji tena ukizingatia tayari nina mtu mwingine, ili asiniharibie ndio maana nimeona nimkataze mazima yeye kunitafuta.


Bado unampenda, usipojibu na kupokea simu zake mara 20 inatosha
 
Ni sawa ila kumbuka mapenzi siyo ugomvi.
Hapa inaonesha una kisasi naye na pia una chuki naye.
Mapenzi ya kijinga sana, kumbuka huyo unayemsifia kuna kuachana pia.
Kama ex anakusalimia yeye mwenyewe, huna mpango naye na anakusalimia kama marafiki na siyo kila siku hapo sioni tatizo.
Kama hadi namba umefuta, inapita hadi miezi 3 ndiyo anakutafuta kukusalimia hapo sioni tatizo. Kumbuka uliishi naye, ulifanya naye ngono na kuongea kwa upendo wala sioni haja ya kukusalimia.
 
Wewe ndiyo umeongea point wengine wote inaonekana wameachana kwa ubaya.
 
Huyo dem itakua ni m'bovu kwa sura na shape na ulidate nae kwa nyege tuu ndio maana mpaka sasa hajapata bwana kwasababu ni m'bovu ingekua mali safi ungeisikia kwenye bomba tuu unless otherwise uwe na ukwasi mwingi mali safi ndo inaweza kukutafuta.
 
Huyu wa sasa nimezaa nae, sasa niharibu mahusiano yangu sababu yake ?
Siyo kuharibu ndugu. Ni hivi shida inakuja km mtakuwa mnawasiliana km wapenzi halafu kila mara hapo ndiyo shida inaanza.
Ila km mtu anakaa miezi mitatu ndiyo anakutafuta kukusalimia tu wala siyo kurudiana nawe wala siyo issue ya mapenzi hapo sioni kosa lake.
Kumbuka kuna nyakati mliishi naye, mlifanya ngono na kuongea kwa upendo kwahiyo kukusalimia km rafiki hapo sioni kosa lake. Kila binadamu ana maana kubwa sana katika maisha yako
Inatakiwa uishi na mtu hata siku mkikutana barabarani msalimiane
 
Hiyo ni sawa na kutembelea muwa kama mkongojo ipo siku utautafuna.Halafu mimi kumwambia hivyo ni kama nimemsaidia tu ili awe busy na maisha yake kuliko kuhangaika na mimi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…