Kuna ubaya kumwambia ex girlfriend wangu kwamba asinitafute maisha yake yote yaliyobaki?

Hivi kumbe wanawake hawapendi kuweka chuki ndio sababu mfano pia huwa hawafuti namba? Kama Ina ukweli vile Johnny Impact ingawa hawa viumbe wana dharau, ukatili n.k
 
Hamjakutanaga na watu wenye maamuzi magumu[emoji16],
Kweli hawajakutana bado. Kuna watu ni dk sifuri inafutwa namba na wewe mwenyewe unafutwa hata mkikutana kama hakukujui.
 
Alikufanyia makosa? Kama la hasha, mpigie simu ufute kauli zako kwa faida ya baadaye... Kesho ni ya tofauti sana
 
Salamu yake mimi ya kazi gani ? Kwa siku nasalimiwa na wangapi ? Unajua madhara ya hizi salamu salamu za ma ex ?
Rafiki mbona hasira tena??? Kama ungekua unajua madhara ya mawasiliano na ex usingekuja na hili bango.
 
Kweli hawajakutana bado. Kuna watu ni dk sifuri inafutwa namba na wewe mwenyewe unafutwa hata mkikutana kama hakukujui.
Huu ndio utamaduni wangu. Sitaki unafiki. Watu wengi sana walionichukulia poa nimewafanyia hivi, yaani nilipobadilika hawakuamini kama mini ni mtu yule yule niliyekuwa-peace kwao.
 
Vijana wasiojua nini maana ya mahusiano ndio hukimbilia kujenga uadui baada ya kuachana. Life is viscous kuna leo na kesho huwezi jua Ex wako atakufaa au utamfaa vipi baadae maishani.
Mimi nawasiliana na Ex's wangu na kila mtu anaheshimu mahusiano ya mwenzake though sometimes huwa tunatania taniana kunogesha maongezi tunayokuwa nayo kwa muda huo.
Umeshauri kitu kizuri sana mkuu
 
What the heck! Kama humuhitaji hata kwa urafiki tu, acha kupokea, simu zake, dunia Ina watu bilioni 8! Wewe huwezi, kumsumbua MTU kwa miaka yote, ataweza pata aliyebora kuliko wewe na anaweza kujiuliza kwa nini alisumbuliwa na wewe!
Wadogo zangu, usitafute MTU asie kutafuta, kama mlikuwa pamoja, huo ukurasa, umepita,
Kwa sie wenye akili kubwa, ma x wetu ni marafiki zetu Sana tu, wana familia zao, tuna zetu, tunakutana kupiga deals za pesa, na kupeana michongo,
Unakuta x wako yupo wizarani,anakupa info za tender zijazo, na wewe unajipanga,
Maisha ni zaidi ya........
 
Kwahiyo wewe unawasiliana na ex zako sababu unavizia tenda wizarani sio ??? Hatuwezi kuwa sawa bro mana kila mtu ana taratibu zake katika maisha.Wakati wewe unategemea ma ex kuendesha maisha yako wengine hatupo hivyo.Unadhani mkeo anakuchukuliaje anapoona unawasiliana na ex zako ? Je na yeye akiwasalimia na ex zake wa kiume utakenua meno ?
 
NAKUMBUSHA NAMBA YA EX HAUFUTWI.
IPO SIKU UTAKUJA KUPATA DHAMANI YA X.ikakusaidia maishani
 
Kwahiyo wewe unawasiliana na ex zako sababu upo wizarani kuvia tender sio ??? Hatuwezi kuwa sawa bro mana kila mtu ana taratibu zake katika maisha.Wakati wewe unategemea ma ex kuendesha maisha yako wengine hatupo hivyo.U
NAKUMBUSHA NAMBA YA EX HAUFUTWI.
IPO SIKU UTAKUJA KUPATA DHAMANI YA X.ikakusaidia maishani
Namba ya ex ukibaki nayo wewe tu kwenye simu yako inatosha.
 
Jamaa kaongea kitu cha hovyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…