Kuna ubaya kununua nyumba ya jirani inayopigwa mnada na benki?

Nunua ila usiende mwenyewe . kafungue company, register kila kitu , nenda kwa wakili akafanye yeye ule mchakato , gharama itazidi kidogo ila itakupa privacy in that ile kampuni ndiyo itappear on paper ila nyuma nyuma ww ndie mmiliki
 
Ni kweli kabisa kwa watu wa tanzania ambao hatueleweki kama ni mabepari au majamaa.
Sena hukawii kuinunua halafu akaomba akae kidogo na ukigoma utaonekana una roho mbaya
 
Inunue, halafu unamrudishia huyo jirani yako hiyo nyumba yake kwa makubaliano ya kukurejeshea hela yako kidogo kidogo! Na huo ndiyo ujirani mwema.
Huu ushauri ni mzuri sana ,na kama utapata neema na imani ya kuutekeleza.Basi utakuwa umefanya jambo lenye baraka,utampendeza Mungu pia utampendeza jirani yako na jamii.Mungu atakubariki,hata jirani atakuombea mema na baraka na kukushukuru,pia atamshukuru Mungu kwa ajilii yako.
Na ndio namna ya kuishi kwa upendo ambao Mungu anatufundisha,na dini zote zinatufundisha upendo kama huu.
 
Hii inaweza kuleta shida zingine.. Kama alishindwa kulipa kwa wakati huko alikokopa mpaka kufikia dhamana kupigwa mnada je kwa jirani ataweza?
 
Akikiuka makubaliano si itakula kwangu kama ameshindwa na bank kwangu si itakuwa vile vile
 
Nadhani inunue alafu umsikie huyo jirani anakuja kujaje, akiwa mjuaji endelea na maisha yako, akiwa na busara, mwambie akulipe uisitiri familia yake.

UBAYA UBWEGE
 
Nakushauri kama wewe ni mwanamme kweli,inunue nā umuombe akutafutie pesa yako taratibu hata kwa miaka mi5 umrudishie nyumba yake.
Ukifanya jambo kama Hilo litakupa heshima Hutaamini.
 
Inunue, halafu unamrudishia huyo jirani yako hiyo nyumba yake kwa makubaliano ya kukurejeshea hela yako kidogo kidogo! Na huo ndiyo ujirani mwema.
Mtu ashindwe kurejesha hela kwa benki mpaka ifikie kumtimua kwake. Ndio mtu huyohuyo aje kukulipa deni kubwa la nyumba???

Hakuna investor mpuuzi wa kufanya hivyo.
 
Nilikuwa mnunuzi mzuri sana wa vitu vya minada.. LaKini baada ya kuanza kupata majanga nikaaza kuvifuatilia baadhi.. Kwakweli niliyokuja kukutana nayo yanatisha
Kuna vitu vimefanyiwa mazindiko na mhusika akashindwa masharti na hakutengua yale mazindiko.. Ukivinunua hivi vitu vinakuja na mazindiko yake
Kuna vitu vilifanyiwa ibada za mvuto na ulinzi halafu zikafeli.. Ukivinunua vinakuja na yale maroho yanayoshindana
Kuna vitu vimefanyiwa maapizi
Kuna vitu vimefanyiwa ushirikina.. Nk
Unaponunua kitu cha mnada sometimes ikibidi pata historia yake.. Ni muhimu sana usije kubeba ama kurithi madubwana yasiyokuhusu
 
Mtu ashindwe kurejesha hela kwa benki mpaka ifikie kumtimua kwake. Ndio mtu huyohuyo aje kukulipa deni kubwa la nyumba???

Hakuna investor mpuuzi wa kufanya hivyo.
Soma vizuri kichwa cha habari. Mtoa mada ameomba tu ushauri! Kwa hiyo ungejikita zaidi kwenye kutoa maoni, badala ya kutaka kutunishiana misuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…