Kuna ubaya kununua nyumba ya jirani inayopigwa mnada na benki?

Kuna ubaya kununua nyumba ya jirani inayopigwa mnada na benki?

Akikiuka makubaliano si itakula kwangu kama ameshindwa na bank kwangu si itakuwa vile vile
Wewe kama investor acha kusikiliza ushauri wa peasants. Kama huwezi inunua kwa sababu za kijamii, acha hiyo hela wekeza kwingine.

Ukitaka kutatua shida za jirani ili uombewe, utajua kwanini ameshindwa kulipa mkopo benki. Kadaiwa na taasisi inayolindwa kisheria kashindwa sembuse wewe individual.
 
Soma vizuri kichwa cha habari. Mtoa mada ameomba tu ushauri! Kwa hiyo ungejikita zaidi kwenye kutoa maoni, badala ya kutaka kutunishiana misuli.
Nimekuuliza juu ya ushauri uliotoa. Au huelewi ulichoandika.
 
Kama unauwezo basi mlipie deni jirani yako,then atakulipa taratibu
 
Haina shida yoyote ila kama unaona si utu kufanya hivyo moja kwa moja basi tumia mtu mwingine ainunue kwa niaba yako, hata akija kugundua baaada ya muda unaweza kumwambia aliyenunua alipata matatizo akanifuata nimkopeshe kwa maana ya kuweka nyumba dhamana mwishowe alishindwa kulipa akaniambia nimmalizie hela.
Pesa yako bado ujitetee, unafiki ni mbaya sana kheri anunue au asinunue ila sio kupitia mlango wa nyuma na huku anamng'ong'a kisogoni.

Kwenye kifariji jamaa akiwa anapiga ukunga kua watu hawana huruma wananunua kweli nyumba yake, na wewe utakua hapo karibu ukisema hakyanani dunia imeharibika na unaeinunua ni wewe mwenyewe.
 
Nilikuwa mnunuzi mzuri sana wa vitu vya minada.. LaKini baada ya kuanza kupata majanga nikaaza kuvifuatilia baadhi.. Kwakweli niliyokuja kukutana nayo yanatisha
Kuna vitu vimefanyiwa mazindiko na mhusika akashindwa masharti na hakutengua yale mazindiko.. Ukivinunua hivi vitu vinakuja na mazindiko yake
Kuna vitu vilifanyiwa ibada za mvuto na ulinzi halafu zikafeli.. Ukivinunua vinakuja na yale maroho yanayoshindana
Kuna vitu vimefanyiwa maapizi
Kuna vitu vimefanyiwa ushirikina.. Nk
Unaponunua kitu cha mnada sometimes ikibidi pata historia yake.. Ni muhimu sana usije kubeba ama kurithi madubwana yasiyokuhusu
ni kweli chief,kuna nyumba moja miaka ya nyuma pale magomeni kuna mtu ali inunua nyumba kutoka kwa mtu. baada ya kuinunua akaifanya zahanati.
Watumishi wa hiyo zahanati wakawa wanaona mama anakuja kutibiwa usiku wa manane akiwa na mtoto.Wanamkuta ndani.Hawajui kaingiaje huku milango imefungwa anasema amemleta mtoto kutibiwa,baadae anapotea.Na mauza uza mengine.Baadae walikuja kuita wachungaji wafanye maombi,maiza uza yalikuja kuisha baadae.

2)Hata maeneo ya ardhi tunazonunua kama viwanja ajili ya kujenga vingine vina maagano,vilikuwa makaburi,au madhabahu za kishirikina zimetolewa makafara,zina maagano,au maroho ya mauti.

3)Hata miti unayoikuta.Mfano mkoa fulani Tz kuna mtu alikuta mti nje ya kiwanja chake yake mpakani wakati ananunua kiwanja,ni mti wa miaka mingi,akajenga akahamia mti ukiwa nje ya fensi yake.Wenyeji /wazee walimsihi sana asije akathubutu asiukate.Siku moja akaamua kuukata.Baada ya kuukata akapata stroke akapoteza fahamu,akapelekwa hospitali,hakupona.
 
Kwanza kabla ya kufanya maamuzi ya kununua hiyo nyumba unatakiwa ujiulize je kama ingekuwa ndiyo nyumba yako inauzwa na bank alafu ikatokea jirani yako akainunua, Je wewe ungejisikiaje?

Kuna uwezekano mkubwa jirani yako aka feel sawa na ambavyo ingekutokea wewe.

Inunue kama unaona ni sawa tu.
 
Utatengeneza uhasama utakao kupelekea kuhudhuria kwenye vilinge au maombi kila wakati.
Kama anauza yeye mwenyewe sawa, tofauti na hapo ni vizuri kuachana nayo ki ubinadamu.
 
Mimi naona inategemea na mfumo wako wa kufikiri kama wa-kibepari au ki- jamaa… kumbuka UJAMAA SHARI.
 
Jirani anazama kwenye maji badala umtoe kumuokoa, unamkandamizia huko huko kwenye maji.
Epuka hii dhambi, mali si kila kitu kwenye hii dunia, Mingu aliagiza tuwapende majirani zetu kama nafsi zetu tunavyozipenda
 
Inunue, halafu unamrudishia huyo jirani yako hiyo nyumba yake kwa makubaliano ya kukurejeshea hela yako kidogo kidogo! Na huo ndiyo ujirani mwema.
Mkuu hapa ataingia mkenge. Kama Bank alishindwa kurejesha, saa ingine wanakulegezea mashart. Kwa mtu binafsi hataeeza. Assume huyo mtu anatolewa kwenye nyumba anayoishi na amekubali matokeo, ujue ameyumba sana kiuchumi.
 
Nakushauri kama wewe ni mwanamme kweli,inunue nā umuombe akutafutie pesa yako taratibu hata kwa miaka mi5 umrudishie nyumba yake.
Ukifanya jambo kama Hilo litakupa heshima Hutaamini.
Ivi unawaju waswahili vizuri huwa hatupendi kuwajibika, Aidha ainunue iwe yake au aachane nayo. Ubaya ubwela.
 
Back
Top Bottom