Kuna ubaya kununua nyumba ya jirani inayopigwa mnada na benki?

Kuna ubaya kununua nyumba ya jirani inayopigwa mnada na benki?

kumsaidia, inunue then akurudishie hela yako bila condition yoyote
 
BUSARA NI KUTOINUNUA.
Kwa sababu jirani yako hapo yupo amepata matatizo ni matatizo kama msiba au huzuni.

Sasa wewe kama jirani au uliyekuwa jirani yake inatakiwa uonyeshe hisia za kuonyeshwa kuguswa sympathy kusikitika pamoja,kumfariji,kulia naye pamoja ndio UTU,au ubinadamu,au good morals na hasa kwa jamii zetu sisi watanzania tunaishi kijamaa bado tuna elements za kijamaa.
Hata kama hujahuzunishwa na yaliyompata jirani yako unaweza kuigiza kumsikitikia na kumpa pole au kumfariji hata kwa kuigiza.

Pia uki inunua bado kumbukumbu za jirani yako na pengine na yeye ataweza kufikiri,umetumia ule msemo wa KUFA KUFAANA,au umetake advantage au ulikuwa unaitamani au umefurahia matatizo yake.Sidhani kama yeye jirani yako atafurahia hilo.Kwa sababu hakupenda iuzwe au haiuzi kwa ridhaa yake au kupenda au kwa kupanga.Ila inauzwa na BANK kwa kushindwa kurejesha mkopo(MATATIZO/CHANGAMOTO AMEPATA AU MAJANGA).Ni tofauti na kama yeye mwenyewe angeamua kuuza kwa kupenda.

UKIACHA BUSARA
,KISHERIA SIO KOSA,WALA HAKUNA MADHARA YOYOTE UKINUNUA.
Lakini mpaka umeamua kuuliza huku JF ina maana uko dilemma au kuna nafsi inakwambia usinunue nafsi nyingine inakwambia nunua.Ila maamuzi au umeshachagua upande moyoni mwako wa kununua au kutonunua,hapa unatafuta pengine justification au support ya kufanya kile ambacho umeshakiamua moyoni mwako.Fanya kile ambacho moyo wako utakuwa na amani na furaha,kadiri ya imani yako na utu wako na mahusiano yako na jamii yako.
Hii kitu nimeona mtwara, mtoto ananunua kitu cha baba au baba ananunua cha mtoto na wanatambiana kabisa.
 
Nunua hiyo nyumba Kwa gharama ndo chukua hati alafu mwambie jirani yako aendelee kukaaa akupe pesa kidogo kidogo mpaka itakapoisha ndio umpe hati Ila akae kwenye nyumba yake,

Trust me hawezi kukusahau daima
Pia usitegemee pongezi wewe fanya ukitegemea malipo kutoka Kwa Mungu tu.

Then ujafa hujaumbika.
Huwenda yatakukuta makubwa na watu watakusaidia bila kutegemea
 
Kuna ubaya wowote kununua nyumba ya jirani inayopigwa mnada na bank baada ya kushindwa kulipa mkopo?
Haitaleta uhasama?
Ubaya upo..tena roho za mikosi,nuksi,balaa na ukame.
Mfano
Miaka ya themanini mwanzoni kuna jamaa alikuja na (gari) 504 kutoka nje ya nchi..sasa sijui nini kilifanyika gari likapigwa mnada...jirani yake akalinunua...kila asubuhi gari inapowashwa jamaa na wanae wanatoka nje wanaiangalia iliyokuwa gari yao kwa uchungu.....KWA KIFUPI ile gari ilipataga ajali mbaya sana( na kuwaka moto) na ukawa ndio mwanzo wa yule mnunuzi kuwa fukara........OGOPA SANA MALI ZENYE MANUNG'UNIKO NYUMA YAKE.
 
Kama umedhamiria kuinunua, nunua kwa mufumo wa inderict. Utakuja kunishukuru
 
Hapo kuna mawili tu

Kwanza, kama ni mtu unampenda na mnaheshimiana sana inunue kisha umpe

Pili, kama hamko karibu kiasi hicho inunue tu
Ainunue ampe afu aka kopee tena sio 😅😅
 
Back
Top Bottom