Kuna ubaya kununua nyumba ya jirani inayopigwa mnada na benki?

kumsaidia, inunue then akurudishie hela yako bila condition yoyote
 
Hii kitu nimeona mtwara, mtoto ananunua kitu cha baba au baba ananunua cha mtoto na wanatambiana kabisa.
 
Nunua hiyo nyumba Kwa gharama ndo chukua hati alafu mwambie jirani yako aendelee kukaaa akupe pesa kidogo kidogo mpaka itakapoisha ndio umpe hati Ila akae kwenye nyumba yake,

Trust me hawezi kukusahau daima
Pia usitegemee pongezi wewe fanya ukitegemea malipo kutoka Kwa Mungu tu.

Then ujafa hujaumbika.
Huwenda yatakukuta makubwa na watu watakusaidia bila kutegemea
 
Kuna ubaya wowote kununua nyumba ya jirani inayopigwa mnada na bank baada ya kushindwa kulipa mkopo?
Haitaleta uhasama?
Ubaya upo..tena roho za mikosi,nuksi,balaa na ukame.
Mfano
Miaka ya themanini mwanzoni kuna jamaa alikuja na (gari) 504 kutoka nje ya nchi..sasa sijui nini kilifanyika gari likapigwa mnada...jirani yake akalinunua...kila asubuhi gari inapowashwa jamaa na wanae wanatoka nje wanaiangalia iliyokuwa gari yao kwa uchungu.....KWA KIFUPI ile gari ilipataga ajali mbaya sana( na kuwaka moto) na ukawa ndio mwanzo wa yule mnunuzi kuwa fukara........OGOPA SANA MALI ZENYE MANUNG'UNIKO NYUMA YAKE.
 
Kama umedhamiria kuinunua, nunua kwa mufumo wa inderict. Utakuja kunishukuru
 
Hapo kuna mawili tu

Kwanza, kama ni mtu unampenda na mnaheshimiana sana inunue kisha umpe

Pili, kama hamko karibu kiasi hicho inunue tu
Ainunue ampe afu aka kopee tena sio 😅😅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…