Kuna uhusiano gani kati ya kupokea zawadi kutoka Kwa manabii na kupoteza kimaisha?

Kuna uhusiano gani kati ya kupokea zawadi kutoka Kwa manabii na kupoteza kimaisha?

lyajody

Senior Member
Joined
Aug 16, 2024
Posts
145
Reaction score
196
Tumeshuhudia anguko la goodluck gozbert baada ya kupokea zawadi kutoka Kwa nabii mkuu...je tutarajie Nini kutokea baada ya dada yetu mpendwa shusho kupokea million kumi Kwa nabii mkuu pamojaa na kusemekana kuishi kinyumba na mtume maarufu wa kuuza mafuta ya upako

Ila spiritual life is real , tuutafute kwanza ufalme wa Mungu na mengine tutazidishiwa..tuweni makini na hawa nitumie manabii na waimbaji wa gosper flavor
 
Hiyo inaitwa nipe nikupe.
Muulize Mzee wa Upako tangu apewe zawadi ya kujengewa kanisa . Sasa hivi mahubiri yake hayajulikani ya Imani gani.
Illuminati wakikuona una kitu cha kukufikisha mbali nje ya mfumo wao wanakupa kitu (chakula), ukipokea tu umekwisha. Wahubiri wengi wameanza na Mungu wamemaliza na Ibilisi, na maanguko yao yalitokana na kupokea pesa as a support.
Kama umeokoka jifunze kusikia sauti ya Mungu. Muumini yeyote, mchungaji yeyote au askofu yeyote kama hasikii sauti ya Mungu direct kuanguka ni kitendo cha dk tu
 
NIkuibie siri yetu sisi ma prophet. Ili uwe na nguvu na ushawishi kama alionao mzee wa mafuta lazima huwe umeshaenda Nchini Ghana .kule ndo kuna Ritual kubwa wanazopewa viongozi wa dini.
Kitendo cha kumvuta mtu mwenye mafanikio kam Goodluck na kumpatia fedha zetu. Ile huwa inamyumbisha na kua kama ina mfunga kimaendeleo maana zile pesa sio za halali

Ata hao wanao jisifu kua " niliandika maombi baba na yamejibiwa. Mafanikioo hayo yanatoka kwa nguvu za giza yaan ritual. Lengo ni kukamata kijiji na kufanya wamuanini mtumishi wa kiroho na sio Mungu. Watu wamependezwa na Dini na ma prophet kufanikisha biashara zao ila sio Neno la Mungu
 
Hakuna kitu cha bure.
Naungana na wachangiaji waliopita waliosema ZAWADI tunazopokea nyingine zimekuwa zimenenewa./zinenuiziwa manuizo mabaya au zimelogezewa zimebeba au zimeambatanishwa na roho za uharibufu za kuzimu.
Unaweza UKATOA kitu wewe uliyetoa kama umetoa kwenye madhabahu ya shetani na mawakala wa shetani /kuzimu /ikiwemo hawa mitume na manabii wa uongo,waganga wa kienyeji washirikina wachawi mizimu majini. n.k
.ile zawadi uliyotoa kuwapatia hao watu washirikina wanaweza kuinuizia ikakudhuru mwenyewe Ukapata athari hasi au ikatambua /ikabadilisha hatima ya maisha yako wewe mwenyewe.
wengine wanaweza wakaiba hata kitu chako chochote hata bila ridhaa yako mfano nguo/viatu ,chakula chochote cha kwako hata nywele,kucha ,kivuli,unyayo,mate ,mkojo n.k na wakavitumia kukudhuru katika ulimwengu wa kiroho
Chochote kinachotoka kwako iwe umetoakwa kupenda au umepeka kwa hiyari au kimeibwa kutoka kwako kinaweza kutumiwa katika ulimwengu wa giza kukudhuru.

Kadhalika kwenye KUPOKEA unaweza ukapokea zawadi au kitu chochote kutoka kwa ufalme wa giza na washirika wa ufalme wa giza kuzimu ,ambacho kimetoka kuzimu au kimenenewa maagano mabaya kimeambatanishwa na nguvu za giza ushirikina ,UKIPOKEA TU tayari unakuwa umefungwa umenasa kwenye hayo maagano na madhabahu za kuzimu.
Na unaweza ukadhurika

TAHADHARI
Tuwe makini katika kupokea na kutoa zawadi.Hata kula kula vyakula vya watu ovyo ofa za vyakula iwe sherehe au misiba au kufuturishwa.Au kupewa kugawiwa nyama zinaweza zikawa nyama za kadara zimwfanyiwa matambiko ,ibada za kiluzimu, au kugawia watu nguo,viatu,n.k
wengi wamepata kuharibikiwa na kuingizwa katika maagano na kufanyiwa ushirikina hata kufa kwa ajili ya kutoa na kupokea zawadi.
Na kuna watu wanapenda kuwaalika watu kuwagawia vyakula vya bure na zawadi mbalimbali wakisema wanasaidia au wanafanya wema hisani kumbe wana siri nyuma ya hizo zawadi wanazigawa bure.

DAWA
Ni kusikiliza roho mtakatifu moyoni mwako kama ukiwa huna amani rohoni,nafsi ikisita kupokea au kutoa usifanye hivyo.
Vitu vingine hata ukiviombea havitakasiki mana ni vitu vilivyotoka kuzimu tayari vinamilikiwa na maagano ya kuzimu dawa ni kuviondoa .Ila ipo neema ya Mungu ipitayi neema zote inayoeweza kutusaidia.
Kusali kuomba Mungu na kuombea vitu unavyopokea unavyonunua .Mungu atusaidie kujua ,Roho mtakatifubatisaidie.HAKUNA MTUME NA NABII WA KWELI..TUJIHADHARI NA MANABII WA UONGO.
 
Hiyo inaitwa nipe nikupe.
Muulize Mzee wa Upako tangu apewe zawadi ya kujengewa kanisa . Sasa hivi mahubiri yake hayajulikani ya Imani gani.
Illuminati wakikuona una kitu cha kukufikisha mbali nje ya mfumo wao wanakupa kitu (chakula), ukipokea tu umekwisha. Wahubiri wengi wameanza na Mungu wamemaliza na Ibilisi, na maanguko yao yalitokana na kupokea pesa as a support.
Kama umeokoka jifunze kusikia sauti ya Mungu. Muumini yeyote, mchungaji yeyote au askofu yeyote kama hasikii sauti ya Mungu direct kuanguka ni kitendo cha dk tu
mzee wa konyagi hajawahi kuwa na kitu tangu aanzishe lile kusanyiko lake.hajawahi.
 
Back
Top Bottom