Nimeishia kusoma hapo uliapoanza na "waabudu shetani"
Quora imeniharibu sana, now day sina taste kabisa na nyuzi nyingi humu Jamii Intelligence
Hakuna 'movie' iliyotengenezwa na 'serikali' ya marekani
Hakuna serikali inayotayarisha Movie
Matukio ya watu kutekwa au kutwaliwa na viumbe vya ajabu (Alien Abduction) ni visa tu ambavyo havina support yoyote ya kisayansi,ni pure invention
Zao la script writers wa Hollywood na Sci-fi movies
Ukitazama ukubwa wa ulimwengu huu tunaoweza kuutazama ( observable universe) na tofauti ya umbali kati ya sayari yetu na sayari yoyote inayoweza ku support evolution ya intelligence species wenye uwezo huo utagundua hakuna tumaini lolote la sisi kuja kukutana na kiumbe chochote kile nje ya sayari yetu
Alpha centaur nadhani, ni nyota inayofata baada ya jua
Ipo umbali wa miaka 4.5 ya mwanga kama sijakosea
Maana yake nini?, ili kuifikia tunahitaji chombo kinachosafiri kwa kasi kama ya mwanga na bado kitachukua zaidi ya miaka minne kufika , hio ni kwa nyota ya karibu tu
Nikukumbushe tu, mwanga ndani ya sekunde moja una uwezo wa kuizunguka dunia nzima...
Physics ime ondoa uwezekano wa kitu chochote kile kuzidi kasi ya mwanga
Ni sheria, inayofanya ulimwengu uwe hivi ulivyo
Plus, kitu chochote kinachofikia speed kubwa kiasi cha kukaribia hata 30% ya speed ya mwanga (Relativistic speed) mda unaanza ku 'behave tofauti'
Hio miaka minne na miezi kadhaa, inaweza kuwa mamilioni ya miaka kwa sisi tutakao baki
So mawasiliano kati yao na sisi hayatowezekana
Mwisho, Dunia imekuepo miaka mingi sana, sisi tu asili yetu ni zaidi ya mamilioni ya miaka iliyopita
Tutapita pia, halafu hakuna atakayetukumbuka,
Dunia haitokuja kuisha kizazi chetu, unless jambo baya litokee kama lilivyotokea kwa dinosaurs